Monday, June 29, 2015

Ukawa wawasha moto wa BVR Dar.

Joto la uandikishaji wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa kutumia mashine Biometric Voters Registration (BVR) nchini, limezidi kupanda jijini Dar es Salaam baada ya vyama vya siasa kujitosa kutoa elimu kwa wananchi na wanachama.

Vyama hivyo vinavyoonekana kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanachama wake wajiandikishe kwenye daftari ni vile vilivyomo kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi na vingine visivyo kwenye umoja huo ACT- Wazalendo na CCM.

Viongozi wa vyama hivyo kwa nyakati tofauti wamekuwa wakihamasisha wanachama wao kujiandikisha kwenye daftari hilo ili waweze kupata haki ya kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema juzi jioni kuwa nguzo kuu ya kuingia Ikulu ni kupitia wanawake kwani endapo watajiandikisha kwa wingi, Ukawa wanaweza kuibuka na ushindi mnono.

Alisema kutokana na kutambua umuhimu wa wanawake kwenye uchaguzi ujao, Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha), limeanzisha kampeni ya kuwahamasisha wanawake kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari hilo ili siku ya uchaguzi waweze kupata haki ya kuwapigia kura wagombea wanaowataka.

Nayo Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Wananchi (CUF- Juce), Wilaya ya Ilala imeunda kikosi kazi cha watu 20 kuhamasisha wanawake wilaya hiyo kujitokeza kujiandikisha katika daftari hilo kazi hiyo itakapoanza jijini humo hivyo karibuni.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ania Chaurembo, alisema kikosi hicho kimepanga kuhamasisha wanawake nyumba kwa nyumba, mtu mmoja mmoja na mtaa kwa mtaa.

Alisema lengo ni kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanajitokeza kujiandikisha katika daftari hilo ili Oktoba 25 mwaka huu wamchague kiongozi bora kupitia Ukawa, ambaye wanaamini atakuwa suluhisho la matatizo yao ya muda mrefu.

Chaurembo alisema pamoja na kwamba wanawake ndiyo wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kupiga kura, lakini wanaamini bado wapo baadhi yao wanashinda kushiriki kutokana na kutokujiandikisha katika daftari hilo.

Alisema kikosi kazi hicho kitahakikisha hakuna mwanamke anayebaki bila kujiandikisha kwa kuwa wanaamini elimu watakayoitoa itawasaidia hata wale baadhi yao waliokuwa wanashindwa kujiandikisha kwa kutofahamu haki yao ya kufanya hivyo.

Aliongeza kuwa kwa mwaka huu, idadi ya wanawake waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na Ukawa ni kubwa, hivyo upo umuhimu mkubwa kwa wengi wao kujiandikisha ili wawachague wanawake wenzao siku ikifika.

"Tunaamini kwamba changamoto mbalimbali zikiwamo za afya ya uzazi zitatatuliwa tukichagua viongozi wengi wanawake."
Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuhakikisha inaandikisha wananchi wote katika maeneo iliyokwisha kufanya kazi hiyo ambao hawakuandikishwa kutokana na muda uliotolewa kuwa mdogo.

Wakati vyama vya siasa vikifanya jitihada hizo, baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wameilalamikia NEC kwa kupanga muda mchache wa uandikishaji katika daftari hilo kwa jiji hilo, wakidai utawafanya wengi wao kukosa haki ya upigaji kura katika uchaguzi mkuuOktoba mwaka huu. NEC ilitarajia kuandikisha wakazi milioni mbili wa Dar es Salaam katika BVR.
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mwasiliano (Tehama) NEC, Dk. Sisti Karia, alisema changamoto wanazokumabana nazo katika kila eneo la uandikishaji nchini, zimekuwa zikitatuliwa ikiwamo kuongeza siku kwa baadhi ya maeneo yenye foleni kubwa ya watu.

Alisema uandikishaji wa maeneo waliyokwisha kuandikisha umevuka malengo na kwamba litakuwapo dirisha dogo la uandikishaji kwa waliokosa fursa hiyo.

NEC juzi ilitoa taarifa ya kuahirisha uandikishaji kwenye daftari hilo jijini humo hadi tarehe nyingine itakayotangazwa .
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo habari, iliyotolewa na Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba, tume hiyo imeahirisha uandikishaji katika daftari hilo kutokana na kuchelewa vifa vya uboreshaji kutoka mikoani.

Vifaa vilivyokuwa vinakusudiwa kuanza kutumia jijini humo vimepelekwa katika mikoa ambayo wananchi wamejitokeza kwa idadi kubwa kujiandikisha kwenye daftari hilo.

Tume hiyo imetoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kuwa watulivu wakati vifaa vikisubiriwa kutoka mikoani.

Sunday, June 28, 2015

VIONGOZI WA CHADEMA WASHIRIKI MAZISHI YA MWANAHABARI EDSON KAMUKARA

Jeneza lililobeba mwili wa mwanahabari Edson Kamukara likiwa limewekwa tayari kwa kutoa heshima za mwisho na kwenda kuzikwa
Mwenyekiti wa CHAHDEMA Mh Freeman Mbowe akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club.
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akitoa salamu za mwisho wakati wa kuaga mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akisalimiana na Mkurugenzi wa Hali Halisi Ndugu Said Kubenea wakati wa kuaga mwili wa mwanahabari Edson Kamukara

Mh freeman Mbowe akisalimiana na mkurugenzi wa IPP MEDIA Dr Reginald Mengi.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akisalimiana na Mkurugenzi wa IPP Media Dr Reginald Mengi

MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA MARYAM SALUM MSABAHA AJITOLEA JENGO KUWA OFISI ZA CHAMA ZANZIBAR

Mbunge wa viti maalum kutoka CHADEMA Zanzibar Maryam Salum Msabaha amejitolea jengo ambalo litakuwa ofisi za chama Mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar. Jengo hilo ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi litatumika kufanyia shughuli mbalimbali za Chama. Jengo hilo litakuwa linaratibu shughuli za ofisi ya wilaya ya Mjini Magharibi na Ofisi ya Jimbo la Mpendae. Pia litakuwa na ofisi inayoratibu shughuli zote za Mabaraza yote ya Mkoa.



Endelea kwa Picha zaidi...... 

Saturday, June 27, 2015

Chadema wafurika kurudisha fomu za ubunge

Katibu wa Chadema Ofisi ya Kanda ya Pwani, Halfan Milambo akipokea fomu za mtangazania ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Ilala kupitia chama hicho, Joyce Charles (katikati) huku akimpongeza kwa kurudisha fomu hizo Dar es Salaam jana. 

Makada mbalimbali wa Chadema jana walirudisha fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho katika nafasi ya ubunge katika majimbo ambayo yanashikiliwa na CCM.
Mchakamchaka huo wa kurudisha fomu hizo ulifanyika katika maeneo mbalimbali nchini jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho.

Katika Jimbo la Monduli linaloshikiliwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa tayari makada watatu wamerudisha fomu. Waliorudisha fomu ni Mwenyekiti wa Chadema wa wilaya hiyo Josephat Sironga, Mwenyekiti Baraza la Wanawake (Bawacha) Mkoa wa Arusha, Cecilia Ndosi na Katibu Mwenezi wa chama hicho Monduli, Patrick Ngala ole Mong’i.

Akizungumza jana Mong’i alisema: “Tumechukua fomu sisi watatu na tumerejesha ili kupisha vikao vya maamuzi.”

Mkoani Mbeya makada lukuki wa Chadema mkoani humo walimiminika kurudisha fomu katika muda uliotakiwa huku wengine wengi wakitajwa kucheleweshwa na kazi ya kuweka fedha benki.

Katika Jimbo la Mbarali linaloshikiliwa na Modestus Kilufi (CCM), makada saba walirudisha fomu hadi saa 10.00 jioni muda ambao ulikuwa wa mwisho.

Katibu wa chama hicho wilayani hapo, Nicolaus Lyaumi aliwataja waliorudisha fomu kuwa ni Jidawaya Kazamoyo, Grace Mboka, Dick Baragasi, Tazan Ndingo, Liberatus Mwang’ombe, Rajab Kilemile na Machami Kasambala.

Katika Jimbo la Mbozi Mashariki, linaloshikiliwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi, wanachama 27 wa Chadema walichukua fomu, lakini hadi saa 10.00 jioni, Katibu wa chama hicho, Michael Mwamlima aliwataja waliorudisha kuwa ni Happness Kwilabya, Abraham Msyete, Anastazia Nzowa, Abdul Nindi, Gerald Silwimba, Eliud Msongole, Zablon Nzunda na Eliud Kibona.

Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Wilaya ya Vijijini, Jackson Mwasenga alisema jimbo la wilaya hiyo ambalo linashikiliwa na Mchungaji Luckson Mwanjale (CCM), waliorudisha fomu ni Daud Mponzi, Edson Jisandu, Adam Zela, Anthony Mwaselela Hadson Sheyo, Benson Mwamengo, Stephano Mwandiga, Frank Mwaisumbe Christina Kalisoto, William Msokwa, Elias Songela na Jeremiah Mwaweza.

Katika jimbo la Kwela linaloshikiliwa na Ignas Malocha (CCM), Daniel Ngogo pekee amerudisha fomu jana huku akitaja vipaumbele vinne ambavyo ni elimu, afya, kuboresha miundombinu ya barabara na ajira jimboni kupitia kilimo.

Pia katika jimbo la Sumbawanga Mjini linaloshikiliwa na Aeshi Hilal(CCM) tayari mfanyabiashara wa mjini Sumbawanga, Casiano Kaegele, maarufu kwa jina la Upendo alirudisha fomu ya kuomba kuteuliwa na Chadema kuwania jimbo hilo.

Kaegele alisema amesukumwa na mambo kadhaa kugombea ubunge katika hilo ikiwamo kuanzisha miradi ya wajasiriamali, kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana na wanawake, sambamba na miundombinu hususan uwanja cha ndege.

Katika jimbo la Morogoro Mjini linaloshikiliwa na Mohammed Abood, makada wa 11 walijitokeza kuomba kuteuliwa baadhi yao ni Marcussy Albaine, James Pawa Mabula, Batromeo Tarimo, Esther Tawete, Steven Daza, Doris Kweka, Gerard Temba, Robert Mruge.

Katika jimbo la Kibaha Mjini linaloshikiliwa na Sylivestry Koka (CCM) wanachama sita kati ya saba waliochukua fomu waliorudisha.

Katibu wa Chadema Kibaha Mjini, Michael Nkobi aliwataja waliorudisha kuwa ni Michael Mtally, Joachim Mahenga, Frank Mzoo, Henry Msukwa, Bosco Mfundo na Isihaka Omari.

Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Khalfan Mirambo alisema Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, waliorudisha fomu za Ubunge jumla yao ni 60 na kati ya hao, 56 ni viti maalumu. Hata hivyo alisema bado majimbo matatu ya Mkuranga, Rufiji na Chalinze.


KAMANDA RAJAB MSABAHA KAUZELA ARUDISHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KILOSA KWA KISHINDO

Picha Juu na Chini: Rajab Msabaha Kauzela mwenye kofia ailyechuchumaa akiwa na wakazi wa Jimbo la Kilosa waliomsindikiza wakati anarudisha fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kilosa



Picha Juu na Chini: Msafara wa waendesha bodaboda uliomsindikiza Rajab Msabaha Kauzela wakati anarudisha fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Kilosa.


Friday, June 26, 2015

SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA EDSON KAMUKARA


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA EDSON KAMUKARA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa kifo cha aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari mahiri na mhariri wa gazeti la mtandaoni, Mwanahalisi Online, Edson Kamukara, kilichotokea ghafla jana jioni katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ajali ya moto.

Kumwelezea Edson Kamukara ambaye kabla ya kuhamia Mwanahalisi Online linalomilikiwa na Hali Halisi Publishers, alikuwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima, akiwa ametokea Gazeti la Jambo Leo ambalo alijiunga nalo akitokea Gazeti la Majira, katika nafasi hii ya salaam za pole yenye ukurasa mmoja, linaweza kuwa jambo gumu sana.

Marehemu Kamukara alikuwa mmoja wa waandishi makini na mahiri ambao tasnia ya habari ingeweza kujivunia kuwa nao (wakiwa hai) kwa muda mrefu, hususan katika changamoto kadhaa ambayo taaluma hiyo adhimu inapitia kwa sasa nchini Tanzania.

Katika salaam hizi, CHADEMA kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ambayo kutokana na majukumu yake ya kila siku ilifanya kazi kwa ukaribu wa kitaaluma na kikazi na Kamukara, inaweza kutaja sifa nne kati ya nyingi alizokuwa nazo Kamukara;

1. Uthubutu wa kukataa rushwa na kusimamia maadili ya taaluma.

2. Kupenda kazi yake.

3. Nidhamu ya kazi.

4. Uwezo wa kutimiza majukumu yake kazini.

Mbali ya kumsaidia kupata zawadi katika mashindano ya tuzo za umahiri wa uandishi wa habari, chini ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), tunaamini sifa hizo pia zilimfanya Kamukara awe miongoni mwa waandishi vijana walioweza kuaminiwa na kukabidhiwa majukumu ya uhariri katika vyombo vya habari vikubwa akiwa na umri mdogo, baada ya kuwa ameandaliwa na kuiva kuchukua nafasi muhimu katika kutimiza uandishi wa habari unaowajibika kwa umma.

Zinahitajika kurasa kadhaa kuweza kumwelezea Edson. Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano, kinatoa salaam za pole na rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na msiba huu wa Kamukara.

Salaam hizi za pole pia ziwafikie wafanyakazi wenzake katika Kampuni ya Hali Halisi Publishers wamiliki wa Gazeti la Mwanahalisi Online kwa kuondokewa na mtumishi mwenzao ambaye tunaamini hadi mauti yanamkuta si tu walifanya naye kazi lakini waliishi naye vizuri.

Aidha chama kinatoa salaam za pole kwa tasnia nzima ya habari nchini hususan kwa waandishi wa habari kwa kuondokewa na mwandishi mwenzao katika wakati ambao mchango wake ulikuwa bado ukihitajika katika mapambano ya kitaaluma na kikazi.

Tunaungana pia katika maombolezo ya msiba huu na wapenzi wote wa kazi za Kamukara ambao wengi wao hususan baada ya kuwa wamesoma makala yake kwenye Gazeti la Mawio toleo la Alhamis wiki hii (jana) ambako alikuwa akiandika mara kwa mara, watakuwa bado hatawaki kuamini kuwa Edson Kamukara katutoka na hatuko naye tena katika ulimwengu huu wa kimwili.

Wakati tukimwombea mapumziko ya amani huko aliko Edson Kamukara, tunamwomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu wafiwa wote na kuwajaalia ujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu na moyo wa subira katika wakazi huu wa majozni mazito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Imetolewa leo Ijumaa, Juni 26, 2015 na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

KINABO WA CHADEMA TISHIO KIBAHA VIJIJINI; Arudisha rasmi ya fomu ya ubunge leo!

Na Mwandishi Wetu, Kibaha
HATIMAYE, Mjumbe wa Baraza Kuu Mstaafu na kada maarufu wa Chadema katika jimbo la Kibaha Vijijini, Kinabo Edward Kinabo, amerudisha fomu leo katika Ofisi za Chadema Jimbo la Kibaha Vijijini mjini Mlandizi, akiomba ridhaa ya chama chake ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kinabo, mzaliwa wa kijiji cha Ruvu Stesheni na mwenyeji wa jimbo hilo, ni mwanaharakati wa maendeleo ya vijana na wanawake akiwa na uzoefu wa kufanya kazi na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa kwa muda mrefu.

Mwanasiasa huyo aliyesomea siasa na uongozi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amewahi kufanya kazi za kusaidia wabunge wa kambi ya upinzani Dodoma katika uandaaji wa hoja,maswali na hotuba za mawaziri vivuli wa upinzani mara kadhaa.

Pia amewahi kuwa mwanahabari mwandamizi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika gazeti la Tanzania Daima

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi fomu ya ubunge, mwanasiasa huyo kijana (34) aliyekuwa moja ya nguzo muhimu katika kufanikisha ushindi wa mbunge wa sasa wa Ubungo, John Mnyika, alisema dhamira yake ni kuleta uwakilishi mpya wenye kujali matakwa na maslahi ya watu wa jimbo hilo na kuhakikisha anakwenda kuishauri na kuibana vizuri serikali katika kutenga na kusimamia fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambazo zimekuwa hazitumiki vizuri kufanya kazi iliyokusudiwa.

Aidha, alisema amedhamiria kuwatetea wananchi wengi wa jimbo hilo wenye kilio cha ardhi, kwani jimbo hilo limegeuzwa kuwa shamba la Bibi kwa vigogo wa CCM na matajiri wachache wenye uswahiba mkubwa na chama hicho kujitwalia kiholela sehemu kubwa ya ardhi na kuibakisha bila kuiendeleza, huku wananchi maskini wa jimbo hilo wakipungukiwa maeneo ya makazi na kilimo.

Aliongeza kuwa kwa miaka mingi wabunge na madiwani wa CCM wameshindwa kuboresha huduma za kijamii, hasa kutokujenga zahanati, kutoboresha miundombinu ya kielimu mashuleni na kushindwa kusukuma miradi ya maji na umeme vijijini, licha ya kuwepo bajeti ambayo ingetosha kuwapunguzia wananchi kero hizo.

"Kwa mfano, Mbunge wa sasa na madiwani wa CCM wakati wanaingia madarakani miaka mitano iliyopita, walikuta zaidi ya vijiji na vitongoji vya mamlaka ya mji mdogo 17 vikiwa havina zahanati, leo muda wao unakwisha wameshindwa kufanikisha ujenzi zahanati wa hata moja. Wananchi maskini wanateseka kusafiri umbali mrefu na kwa gharama kubwa kufuata tiba kwenye kituo kimoja cha afya cha hapa mjini Mlandizi, hali hii haivumiliki, wakati wa Kibaha Vijijini kupata mbunge makini, jasiri na mwenye uwezo wa kutosha kuwatetea na kusukuma maendeleo yao umefika, nimejitokeza kuwa mbunge wa aina hiyo, nataka kuwa faraja ya mama zangu wa jimbo hili, ya vijana wenzangu wa jimbo na wazee wa jimbo hili. Yote yalishindikana ndani ya jimbo hili chini ya wabunge na madiwani wa CCM,yanawezekana chini ya Kinabo wa Chadema na UKAWA. Nasubiria ridhaa ya chama changu", alisema mwanasiasa huyo.

Kinabo alitumia fursa hiyo kuitangaza kauli mbiu yake ya kampeni inayosema "Kinabo Atosha Kibaha Vijijini; Yaliyoshindikana, Yanawezekana"

Hali ya kisiasa ndani na nje ya Chadema jimboni hapa, inaonyesha kuwa Mwanasiasa huyo ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kupita kwenye kinyang'anyiro cha kura ya maoni kutokana na kufanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama hicho jimboni hapa na kuvuta hisia za wananchi wengi wa vijijini na ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlandizi kwa kujenga hoja nzito katika hotuba zake na zinazoonekana kufanyiwa utafiti wa kina.

Wanachama wengine wa chama hicho waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa chama hicho ni Dr Rose, Eli Achahofu, na Edita Babeiya.

Thursday, June 25, 2015

Chadema yakomba 300 toka CCM Kikombo, Chololo.

Na Bryceson Mathias, Kikombo Chamwino.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Kikombo Wilaya ya Chamwino Dodoma, kimekomba Wanachama 300 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Vijiji vya Kikombo na Chololo, huku kikimruhusu, Yona Kusaja, atangeze Nia ya kugombea Udiwani bila Mpinzani.

Katika Mikutano ya Watia Nia wa Udiwani na Ubunge iliyofanywa na Chadema nchini kote hivi karibuni; Katika Kata ya Kikombo, ilimalizika Chadema kikikomba na kuzoa Wanachama 200 toka Kijiji cha Kikombo, ambapo Kijiji cha Chololo walizoa Wanachama 100.

Mikutano hiyo, iliyofanywa na Kusaja ambaye 2010 anadai alichezewa rafu ya matokeo yake na Mashushu wa Serikali, amejigamba kuwa aliporwa haki ya Ushindi wa Udiwani wa Kata hiyo kwa hila, hivyo amewashukuru Wanachama kumwani na kutaka asiwe na Mpinzani wa Chadema.

“Najua Sisi wote tulipigika na Uongozi wa Kata uliopo madarakani, ila nashukuru wananchi wamebaini na kuelewa makosa yaliyofanyika kwa hila, na ndiyo maana Ishara ya kuonesha hasira yao, wamefanya kweli kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kushinda kwa Kishindo.

“Naomba Ushindi, na Imani kwangu, vitumike kufanyia maamuzi Magumu kwenye Uchaguzi Oktoba 25, Mwaka huu, kwa kuhakikisha tunang’oa Mizizi ya CCM na Maangamizi ya Uporwaji wa Uchumi wa Wananchi wa Kikombo, walionyanyaswa na Kuteswa kwa Miaka Mitano.alisema Kusaja.

Kata ya Kikombo, ina Mitaa Mitatu, Kikombo Makulu, Mnadani na Chololo; Lakini katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita, Chadema kilishinda Mitaa Miwili ya Kikombo Makulu na Mnadani, ambapo CCM iliambulia Kiti Kimoja, ambapo Wana CCM 100 wametimkia Chadema.

Wiki ijayo, Viongozi wa Chadema Taifa, wanataraji kufanya Mkutano Mkubwa katika Kata hiyo, ambapo Viongozi wa Kanda, Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino, watahudhuria katika Mkutano huo, ambapo kuna taarifa Wana CCM wengine warejesha Kadi na Kujiunga na Chadema.

Viongozi wa Dini; “Kikwete Simamisha Muswada wa Habari”

Na Bryceson Mathias, Dodoma
WAJUMBE wa 205 wa Kamati ya Maadili ya Amani na Haki ya Jamii ya Viongozi wa Dini nchini, wameitaka Serikali kusimamisha Muswada wa Uhuru wa kupata Habari kujadiliwa bungeni kwa madai, unawanyima haki Watanzania kupata habari, na haukustahili kuibuliwa wakati wa Uchaguzi.

Kamati hiyo imemuomba Rais, Jakaya Kikwete, ikimtaka akumbuke Kauli yake mwenyewe ya mwaka 2001 akihamasisha wadau wa habari, aliposema, kama Wananchi watakosa habari ndani ya mfumo wetu nchini, watazitafuta nje.

Akikiri kuwa na Kikao cha Viongozi hao Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, alisema mbali ya Kumtaka Kikwete asitishe Muswada huo, pia wanapinga Njama zozote zilizojificha nnyuma ya Muswada huo.

Mbali ya kusema Viongozi hao kuunga wanaunga Mkono Tamko la Wanachama wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT) la kutaka Muswada huo usingeenda kujadiliwa bungeni, Mwamalanga amedai, Muswada huo kwa Wadau ni kama ‘Petroli kwenye Moto’.

Katika Kikao hicho Wandishi hawakuruhusiwa kwa madai wataruhusiwa siku ya Mwisho ambapo Viongozi hao watataka Umma katika siku ya siku ya Nne (4) uhabarishwe, ingawa Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kunasa kilichozungumzwa miongozi mwa Viongozi wa Dini na kumhoji Askofu Mwamalanga kama ni kweli.

Miongoni mwa Maazimio Saba yaliyoazimiwa na Mashekhe na Ma-Askofu hao ambao ni Wajumbe kutoka kila Mkoa, ni pamoja na kuupinga Muswada huo na Kuiunga Mkono MOAT na Wadau wa habari katika Kilio chao.

Yaliyokuwemo ni ‘ Uhuru wa Habari si wa Vyombo vya habari, Wandishi na Wamiliki pekee yao, bali ni wa Wananchi, hivyo haikuwa haki kupelekwa bungeni wakati wa Uchaguzi kwani ulitakiwa upitiwe na wenye Ueledi ili usiwabinye wadau hao kupata habari.

Wamedai, Muswada huo utawafanya Wadau wa Habari na Wananchi, wawachukie wabunge wao, hasa kutokana na ukweli kwamba, Mchango wa Vyombo vya Habari, umechangia kwa asilimia 81% kufichua uharifu wa Rushwa, Ufisadi na kuliletea Taifa Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.


Wamesema, Vyombo vya Habari na Wanahabari vimekuwa ndiyo sehemu pekee ya Kimbilio la Wananchi wanyonge katika kupata Haki zao kwa haraka kuliko Mihimili mingine yoyote, hivyo ni wajibu Muswada huo urudishwe kwao ili wenye Ueledi na Taaluma hiyo waujadili.


Wamedai wanapinga Njama zozote zilizojificha nyuma ya Muswada huo, kwa kupelekwa kwa Muswada kwa hati dharula, kunadhihirisha kilichoko nyuma ya Pazia hilo, na kama umelenga kuwanyima Wananchi taarifa za Uchaguzi, basi wahusika wameweka Petroli kwenye Moto.

Aidha Mwisho walisema, Kuchezea Tasinia ya Habari na Uhuru wake ni sawasawa na kuchezea Petroli kwenye Moto, hivyo wanamuomba Rais Kikwete kusitisha Muswada huo na kuwasikiliza Wadau wake, kwa sababu Kuwaburuza ni kutowatendea Haki, isipokuwa kuchochea Vurugu.

Lema avutana na Polisi, NEC.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) , amemtaka Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kujiandaa kupokea mkanda wa DVD ya bomu lililorushwa katika mkutano wa Chadema, Juni 15, 2013 kabla ya Bunge kuvunjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lema alidai amechukua hatua hiyo kutokana na Sabas kutuma Jeshi la Polisi toka nje ya mkoa huo kwenda kufanya kazi maalum ya kummaliza nguvu kabla ya uchaguzi.

Alisema umma wa Watanzania anapenda wajionee polisi waliohusika kufanya unyama katika ufungaji wa kampeni za udiwani kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema.

Kuhusu uandikishwaji katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inafanya hujuma ya kusitisha uandikishwaji wakati idadi ya watu ikiwa kubwa kwenye kata zilizoanza kuandikisha.

“Walichofanya ni kuorodhesha majina ya watu waliokuwapo juzi kituoni na jana wanawamalizia hao na wanaokuja ambao ni wengi wanakataliwa kuwa zoezi limefika mwisho maeneo hayo, wakati maeneo mengi wameongeza siku tatu na siyo majiji makubwa kama Arusha,” alisema.

Alisema tayari ameagiza wenyeviti wa mitaa kukusanya idadi ya wapiga kura waliobaki kila mtaa na walioandikishwa, kisha atafanya maandamano makubwa ya kupinga dhambi hiyo.

Hata hivyo, amemwomba Rais Jakaya Kikwete kumwondoa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, katika nafasi hiyo akidai ameshindwa kuendesha vizuri kazi ya uandikishwaji na kuhatarisha amani ya Tanzania katika uchaguzi ujao.

“Huyu Lubuva anasema mimi nasababisha vurugu naingilia Tume, kumwambia watu ni wengi aongeze mashine ni kosa, ameshindwa kuleta watumishi wa Tume, mashine chache na ameweka watu wasio na sifa na kusababisha watu kulala vituoni,” alisema.

Naye Kamanda wa Polisi Liberatus Sabas, alisema Lema anatakiwa kuhamasisha wananchi wake kufanya maendeleo, badala ya kuendesha vurugu na maandamano.

“Huyu Lema watu wamemchoka na amebakiza siku chache kumaliza muda wake na kurudi kuwa raia kama wengine, hivyo amalize salama na asitafute shari, ila akileta vurugu na mwingine atakayesababisha uvunjifu wa amani katika zoezi hili, atakumbana na mkono wa dola na jeshi lipo vizuri,” alisema.

Tuesday, June 23, 2015

MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA MHESHIMIWA FREEMAN MBOWE ASHIRIKI KUFANYA USAFI JIMBONI HAI




Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai (mwenye kofia katikati) akishirikiana na wananchi wa Lukeni, Kata ya Masama-Mashariki kufanya usafi katika Soko la Masama-Mula juzi, katika kampeni ya kutunza mazingira kwenye jimbo hilo iliyopewa jina la 'Keep Hai Clean' ikitumia gari maalum la kukusanyia taka lenye uwezo wa kubeba tani 32 za taka ambalo mbunge huyo alitoa msaada kwa wananchi wake hivi karibuni.

Chadema yazindua 'Operesheni Amsha Wanawake

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua operesheni maalum ya kuwaamsha wanawake nchini kote kwa nia ya kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 na kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupiga kura nyingi za ndiyo kwa wagombea wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Aidha, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani , Mabele Marando, amewataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika daftari la wapigakura ili kufanikisha kumpeleka Ikulu mgombea atakayesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

Akizungumza katika uzinduzi wa operesheni hiyo inayofahamika kama ‘Operesheni Amsha Wanawake Tanzania’, kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam jana, Marando alisema ni vizuri wananchi wakajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuacha kusikiliza majungu ya baadhi ya watu dhidi ya Ukawa. Alisisitiza kuwa umoja huo haujateteleka na utasimamisha mgombea mmoja wa urais.

Marando alisema madai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kuchukua fomu za urais ndiyo sababu Ukawa inatetereka yasiwashitue wanachama kwa kuwa huo ni utaratibu wa chama (CUF)ambao hauhusiani na mipango ya Ukawa.

Mkurugenzi wa bendi ya wanawake, Lilian Wasira, aliwataka wanawake wajitokeze kwa wingi kwa kuwa wao ndiyo wenye mchango mkubwa katika kupiga kura.

Alisema kuwa uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umewafanya wanawake kubaki katika maisha ya kimasikini hivyo kupitia bendi hiyo itasaidia wanawake kuchagua rais kupitia ukawa na moja kwa moja kwenda ikulu na kubadirisha maisha yao kwa ujumla.

“Mimi ni mwanasheria lakini nimeamua kuimba ili wanawake wanielewe kwa sababu CCM imefilisika. Ikulu Oktoba 25, mwaka huu ni ya Ukawa,”alisema Wasira.

KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROAD SLAA AMTEMBELEA KAIMU MUFTI MKUU SHEIKH ABUBAKAR ZUBERI



Muda mfupi baada ya aliyekuwa mmoja wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa la BAKWATA Sheikh Abubakar Zuberi, kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DK. Willibroad Slaa amemtembelea nyumbani kwake kumpongeza na kumtakia majukumu mema akimhakikishia ushirikiano kama jirani na kiongozi.

Sheikh Abubakar Zuber ambaye ametangazwa leo kukaimu nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa dini ya Kiislam kwa siku 90 hadi hapo atakapochaguliwa Mufti Mkuu kwa mujibu wa taratibu za dini hiyo, anaishi Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jirani na zilipo Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA.

Mbali ya kumtakia kila la heri, Katibu Mkuu Dk. Slaa amemuahidi Mufti Sheikh Zuberi kuwa CHADEMA iko tayari wakati wowote kutoa ushirikiano atakaouhitaji katika kutimiza wajibu wake huo.

“Shehe Zubeir, jirani yangu napenda kutumia fursa hii kukupongeza sana kwa namna ambavyo wenzako wamekupatia imani kubwa na kukuteua ili uwaongoze Waislam kiroho. Ni imani kubwa ambayo binafsi naamini utaweza kuitumikia wakati mkiendelea kusubiri taratibu zingine za uchaguzi.

“Nitumie fursa hii pia kusema tukiwa majirani zako hapa Mtaa wa Ufipa, tukiwa viongozi ambao tunao wanachama, wapenzi na wafuasi wetu wenye dini tofauti wakiwemo Waislam, naomba kukuhakikishia ushirikiano kutoka kwetu wakati wowote katika kutimiza majukumu yako haya makubwa na nyeti.

“Shehe wangu kwa muda wote tumeishi pamoja hapa tukiwa majirani… ukitimiza wajibu wako uliokuwa nao nasi tukiendelea kutimiza majukumu yetu katika jamii ya Watanzania, nakutakia kila la heri katika kuwatumikia na kuwaongoza kiroho Waislam wa Tanzania,” alisema Dk. Slaa nyumbani kwa Sheikh Zuberi leo mara baada ya uteuzi wa Kaimu Mufti Mkuu wa Waislam kufanyika.

Imetolewa leo Jumatatu, Juni 22, 2015 na;
Idara ya habari na mawasiliano
CHADEMA

Monday, June 22, 2015

KADA MAARUFU WA CCM MAFIA AJIVUA GAMBA NA KUHAMIA CHADEMA

Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kigamboni wilaya ya Mafia Mohamed Makungu amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na CHADEMA. Pichani Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Mabere Nyaucho Marando akimkabidhikadi.

MTIA NIA UBUNGE JIMBO LA KILOSA KUPITIA CHADEMA RAJAB MSABAHA KAUZELA AENDELEA NA ZIARA YA UFUNGUZI WA MATAWI YA CHADEMA KILOSA






Mtia nia Ubunge Jimbo la Kilosa CHADEMA Rajab Msabaha Kauzela akitembelea maeneo mbalimbali Jimboni Kilosa kukutana na wakazi na kujionea hali halisi ya wakazi hao na matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Pichani Rajab Msabaha Kauzela akiwa na baadhi ya wakazi wa Kilosa alipowatembelea kuona hali halisi ya maisha yao ya kila siku. Kauzela alipata muda wa kuongea na wakazi hao na kujua matatizo mbalimbali yanayowakabili pamoja na kuwa na ardhi yenye rutuba na vyanzo mbalimbali vya Uchumi ikiwemo kilimo na ufugaji.

Salum Mwalim awataka wanafunzi SEKOMU WASISALITI wajibu wao.


Na Mohamed Mtoi
Naibu katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalim amewakumbusha vijana nchini hususani walio vyuo vikuu wajibu wao wa kusimamia kupatikana kwa uhuru wa pili wa nchi wenye lengo la kuwakomboa watanzania kutoka katika maisha magumu. Mwalim ameyasema hayo jana mjini Lushoto wakati akiongoza mahafali ya wanachama wa Chadema wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU)- ambapo alikabidhi vyeti kwa wahitimu.

Mwalim amesema kuna ushawishi mkubwa unaofanywa na ccm kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ili wakubalike ikiwemo kumwaga fedha na ahadi za vyeo na ajira ili kuwapupambaza vijana kuondoka katika msitari wa harakati. Mwalim amewakumbusha vijana hao kuwa kila kizazi kina jukumu lake na kwamba kizazi cha baba wa taifa Mwl Julius Nyerere kilikuwa na jukumu la kuwakomboa watanzania kutoka mikononi mwa wakoloni na kwamba kazi ya kizazi cha sasa ni kuitafutia Tanzania uhuru wa pili.

Amewapongeza vijana hao wa SEKOMU kwa kusimamia na kunadi sera za Chadema na kuwapa changamoto ya kuwania nafasi za ubunge na udiwani kwenye uchaguzi mkuu ujao wa unaotarajiwa kufanyika oktoba 25, 2015.

Amewaambia vyeo, fedha na ajira nzuri watazipata na kuzifaidi kwa haki, heshima na amani baada ya ccm kung'oka madarakani tofauti na watakapokubali kupokea sasa kama rushwa ya kusailiti wajibu wao kwa taifa. Mwalim amesema serikali ya Ukawa itatatua changamoto zilizopo- elimu ya juu katika kipindi cha kwanza cha miaka mitano kwani niza kutengenezwa na serikali ya ccm kwa masilahi yao binafsi na si kweli kwamba hazina suluhisho la kudumu.

Naye mratibu wa kanda Taifa Mohamedi Mtoi ambaye ni mtia nia wa jimbo hilo (Lushoto mjini) amewaasa wahitimu hao wasiache kuendeleza harakati na kupigania haki za watanzania wengine katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwataka wawe chachu ya kuhamasisha watu wenye sifa ya kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura linalo endelea kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.

Amewaambia wana wajibu wa kujua ratiba za maeneo yao na kuhamasisha vijana na wazee kujiandikisha kwani ndio silaha pekee ya kuung'oa utawala wa serikali ya ccm ambayo imeshindwa kutimiza ahadi ya kuwaletea watanzania maisha bora na matokeo yake gharama za maisha zimepanda na mateso kwa watanzania yameongezeka kwa kukosa huduma za msingi za kijamii.

Mahafali hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa hotel ya kakakuona na kuhudhuriwa na viongozi wa chama wa jimbo na wilaya ya Lushoto.

Chadema: Wanaoshawishi kupigiwa kura kwa rushwa kukiona

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza safari ya kwenda mikoani kuwajengea uwezo wanawake ili mafisadi wanaotumia mianya ya rushwa kuwashawishi wawapigie kura wawaogope.

Mkurugenzi wa Wanawake Band, Lilian Wasira, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia uzinduzi wa bendi ya wanawake na operesheni ya Amsha Wanawake Tanzania, itakayofanyika Kanda ya Pwani, viwanja vya Tanganyika Parkers leo.

Katika uzinduzi huo wasanii kama Christian Bella, Profesa J na Flora Mbasha wanatarajia kutumbuiza siku hiyo.

Lilian alisema bendi hiyo pamoja na operesheni ya Amsha, malengo yake ni kuwahamasisha wanawake kujitambua kuwa mabadiliko ya taifa yataletwa na wao ikiwa watakataa rushwa za vitenge, khanga na hela ya chumvi.

“Wanawake iwe mwiko kuhongwa khanga, kofia hatupo tayari kuona wanawake vijijini wanaendelea kuwa masikini mwaka hadi mwaka kwa sababu tu wanauza kura zao kwa mafisadi, tunaenda kuwaamsha wajitambue,” alisema.

Pia alisema wanaenda kuwahamasisha wanawake kutambua kuwa uuzaji wa kura zao unasababisha rasilimali ambazo ni urithi wa watoto wao unahodhiwa na wachache.

Aliongeza kuwa uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, wanaenda kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) inaenda kuchukua dola.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake jimbo la Kawe, Janeth Rithe, alisema mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo atakuwa ni Katibu Mkuu wa chama, Dk. Wilbroad Slaa.

Kaimu Mwenyekiti wa mkoa wa Kinondoni, Rose Moshi, alisema kuwa, mwanamke ni miongoni wa wale walioleta mabadiliko ya Taifa hivyo wanapaswa kuheshimiwa.

Sunday, June 21, 2015

MBOWE, NDESAMBURO NA JAPHARY WATIKISA MOSHI

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway
mjini Moshi .

Mwenyekiti wa Chadema taifa,Freman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Philemon Ndesamburo walipokutana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway mjini Moshi,wengine ni Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Kilimanjaro ,Helga Mchomu .
Mamia ya wananchi waliohudhulia mkutano huo ,wakimsikiliza mstahiki Meya,Jafary Michael (hayuko pichani).



Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Philemon Ndesamburo akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway

Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimkaribisha Mwenyekiti wa Chadema taifa ,Freman Mbowe kuhutubia wananchi katika viwanja vya Railway mjini Moshi

Endelea...


Saturday, June 20, 2015

MUSSA HASSAN ZUNGU APATA MPINZANI JIMBO LA ILALA

MUSLIM HASSANAL akizngumza na wanahabari kuhusu lengo lake kwa wana ilala.
MUSLIM HASSANAL akionyesha FORM ambayo tayari amekwishaijaza na kuirejesha leo

Mwanachama wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema jimbo la ilala Bwana MUSLIM HASSANAL leo ametangaza rasmi nia yake ya kumngoa katika kiti cha ubunge mbunge wa jimb o la ilala mh MUSA ZUNGU katika uchaguzi ujao mwishoni mwa mwaka huu.

Hayo ameyasema muda huu Jijini Dar es salaam wakati akirudisga Form ya kugombea ubunge katika jimbo hilo la ilala tukio lililofanyika katika ofisi za kanda za chama hicho Akizungumza na wanahabari mara baada ya kurejesha Form hiyo Bwana MUSLIM amesema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la ilala linarudi katika hadhi yake ya kuwa jimbo la mfano katika majimbo yote ya Dar es salaam ukizngatia kuwa jimbo hilo ndilo linalobeba Jina la Dar es salaam kwa kuwa na ofisi mbalimbali na kubwa za serikali.

“Ukizngumzia uchafu Dar es salaam lazima uitaje ilala,ukigusia ubivu wa miundombinu lazima uitaje ilala,ukitaja wananchi kuishi kwa hali duni lazima uitaje ilala,sasa sisi kama chama tumeamua kuhakikisha kuwa hali hii inafutika na tutalirejesha jimbo la ILALA mikononi mwetu kama ukawa watanipa nafasi ya kugombea katika jimbo hilo”alisema mtia nia huyo anayeonekana kujiamini sana. kinondoni Jijini Dar es salaam.

Ameongeza kuwa ukimtizama unawezaa k,udhani yeye sio mtanzania ila kwa ufupi yeye ni mzaliwa wa Tanzania na maisha yake yote amekulia kariakoo,hivyo anajua matatizo ya wananchi wa ilala kwa ujumla,na amejipanga kuhakikisha kuwa anashirikiana na chama chake kwa kupitia ukawa kuwasaidia wananchi hao.

Bwana MUSLIM HASSANAL aliwahi kugombea ubunge katika jimbo la kigoma kaskazini uchaguzi uliopita lakini hakufanikiwa kupita ambapo DAVID KAFULILA wa NCCR-MAGEUZI alishinda,ambapo akizunguzimzia hilo amesema kuwa kigoma ndipo walipo babu zake na ndio maana aliwahi kugombea huko lakini kwa sasa anadhani ni muda wa kumuunga mkono KAFULILA kwani bado anastahili kuongoza jimbo hilo.

BAWACHA kuikabili rushwa Uchaguzi Mkuu

KATIKA kuendeleza harakati za kumkomboa mwanamke kwenye vishawishi na rushwa mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kisiasa, Balaza la Wanawake Chadema (BAWACHA) limegundua mbinu mpya.

Mbinu hiyo inalenga kushawishi wanawake kuchukia na kukataa rushwa ili kuweza kuchagua viongozi wenye maadili. Harakati hizo zitafanywa kati ya BAWACHA na Wanawake Bendi.

Imefahamika kuwa, wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wanawake wanaoonekana kuwa na ushawishi kubwa, hutumia kuwapotosha wanawake wenzao na hata kupokea rushwa kutoka kwa viongozi.

Lakini pia wanawake huchukuliwa kama watu wa mwisho ambapo hufanyiwa maamuzi na wanaume hasa kipindi cha uchaguzi.

Kwa kuliona hilo, BAVICHA kwa kushirikiana na Wanawake Bendi imeanzisha oparesheni maalumu iliyolenga kuhamasisha wanawake wote nchini kuchagua viongozi bora.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa bendi hiyo ambaye ni Kada wa Chadema, Lilian Wasira amesema, lengo kuu la kuanzisha bendi hiyo ni kuchochea mori ndani ya wanawake ili watambue umuhimu wao.

“Wanawake wanatakiwa kuutambua uthamani wa kipekee walionao, hivyo wasikubali kurubuniwa na kuuza haki zao za msingi kipindi hiki cha uchaguzi,” amesema Wasira.

Aidha, bendi hiyo pamoja na “Operesheni Amsha Wanawake Tanzania” vinatarajiwa kuzinduliwa kesho katika viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe saa 7;00 mchana, ambapo Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuongoza uzinduzi huo.

Na kwamba, uzinduzi huo utahudhuriwa na wanachama mbalimbali kutoka mikoa mingine, pamoja na wadau mbalimbali wapenda maendeleo ya wanawake.

Wasira ameeleza, mara baada ya kuzinduliwa bendi itaanza ziara zake za kuhamasisha wanawake. “tutaanza kanda ya Dar es Salaam na baadaye tutasambaa mikoa mingine Tanzania nzima.”

Katibu BAWACHA Jimbo la Kinondoni, Rose Moshi amewataka viongozi wote wa chama kuhudhuria uzinduzi huo ili kuleta hamasa zaidi.

“Wanawake muda wa ukombozi umefika tujitokeze kwa wingi. Na sisi kama BAVICHA tutashirikiana vizuri na bendi hii kuhakikisha inaleta mabadiliko makubwa ndani ya nchi yetu, huku tukijiandaa kuipokea serikali mpya,” amesema Moshi.


Mwanahalisi Online

Chadema: Nape anaota ndoto za mchana.

Kauli ya Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye, kudai chama chake kitaendela kuongoza nchi hata kama ni kwa kura za wizi, chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibuka na kumjibu kuwa hizo ni ndoto za mchana.

Akizungumza na NIPASHE kwenye ofisi za Chadema Wilaya ya Chato, Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (Bavicha), Julius Mwita, alisema chama chake kipo kwenye maandalizi kamili ya kuingia Ikulu na kwamba mbinu za CCM kuendelea kuiba kura mwisho wake umefika.

Alisema kila mbinu chafu za CCM zilizoandaliwa kuhujumu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu zimeshabainika ikiwamo kuagiza magari 700 ya kutawanya wananchi kwa maji ya kuwasha, badala ya kujikita kubuni mbinu bora za kudhibiti mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe wanaouawa bila hatia.

"Nikuhakikishie kuwa mwaka huu Chadema kupitia Ukawa tunaingia madarakani...hivi sasa CCM wanaweweseka tu wasijue la kufanya ndiyo maana wamekuwa na foleni kubwa ya wagombea urais kana kwamba ni taasisi ya kuchezewa hadi na wasomi wa darasa la saba," alisema.

Alisema tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu imejionyesha kwenye uchaguzi mdogo uliomalizika ambapo Ukawa ulikishusha CCM katika viwango vya ushindi kutoka aslimia 95 hadi kufikia asilimia 64 na kwamba hatua hiyo ni wazi kwamba Ukawa wanakwenda kuchukua dola.

Akizungumza hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara wilayani Chato mkoani Geita, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdurahman Kinana, aliwataka wafuasi wa chama hicho kuikosoa serikali ya CCM inapofanya mambo yasiyopaswa na ikiwezekana wafanye maandamano kupinga badala ya kusifia kila kitu.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida Nnauye, alisisitiza kuwa CCM kitaendelea kuongoza nchi kwa kuwa ni chama makini na kwamba hata kama itakuwa kwa kura za kuiba na kudai kuwa bao ni bao hata kama ni la kidole iwapo kama mwamuzi hataweza kuona.

Kauli ya Nape ilipokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo huku wakidai ameamua kutoa siri inayowafanya CCM kupata ushindi katika chaguzi zilizopita huku wengine wakisifia kuwa ni wakongwe wa siasa na kwamba mbinu zote za ushindi wanazo.

Friday, June 19, 2015

CHADEMA; Wananchi! “Kama na Sindano tunaagiza Nje”, Ipumzisheni CCM!.

Na Bryceson Mathias Morogoro.
MTIA Nia wa Udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Kihonda Maghorofani; Msomi, Elizeus Rwegasira, amesema kama Wananchi wanashuhudia jinsi Serikali yao ianvyonunua hata Sindano, Leso na Njiti za kuchokolea Meno nje ya nchi, basi Waisaidie Chadema kukipumzisha Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rwegasira alisema hayo jana Kihonda, baada ya Tume ya Uchaguzi (NEC) Juni 16, Mwaka huu, kukwama kuanza kuandikisha Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Wilaya zake, kwa madai ya kukosa Wino (Cartridge) na Vifaa vingine; huku wakjinasifu kama vitapatikana, Uandikishaji utaanza baada ya siku tatu.

“Kilichoua Viwanda na bidhaa za Kilimo na Ngozi, (Katani, Chai na Pamba), nz ajira ya Vijana, ni hao hao ambao sasa wanahujumu Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kiharamia, ili watu wasipata Haki ya Kuchagua Viongozi makini, wataorejesha Viwanda na Kuongeza Vingine.

“Hata wanaoridhia kuongezwa kwa bei ya Mafuta ya Taa yanayotumika na Walalahoi vijijini wakiwa hawana hata uwezo wa kuyanunua, isipokuwa wanachofanya ni kuharibu Mazingiraa na kuendelea kutumia Nyasi na Vijinga kupata Mwanga ili watoto wao wajisomee”.alisema Rwegasira.

Alisema, Wananchi; jueni Wanaotaka Mafuta yaongezwe bei, wana Maslahi binafsi; Hao ndio Wanasiasa wenye Meli, Mabasi, Malori, wanaotaka Reli ife, wao wafaidike, Viwanda Vife, bidhaa za Kilimo na Ngozi za Walalahoi zikose Soko, ili wao wazinunue kwa bei Ndogo, wakauze Nje kwa bei kubwa.

Ndugu zangu, “Mnapoona hayo na Kutambua, hakikisheni mnajiandikisha, Hata kwa Kukaa katika Vituo vya Uandikishaji hadi asubuhi, ili wakitaka kuwanyima haki ya kujiandikisha wakiwa na lengo la kuzuia Mafuriko ya Ukombozi kupitia Msukumo wa CCM, Mgangamale”.alisema Rwegasira.

Amewasisitiza Wananchi wa Kata yake ya Maghorofani na Mtaa anaouongoza wa Maghofani ‘A’ ambao yeye ni Mwenyekiti aliyeshinda kwa Tiketi ya Chadema na nchini kote, wasikubali Uongo na Usanii wa kwamba hakuna Wino, wakazmuz kurudi nyumbani, bila kujizndikisha, hiyo ni mbinu ya kuwakatisha tamaa wasijiandikishe siku ziishe.

Hivi karibuni, Utawala wa Mkoa wa Morogoro, uliviandikia Vyama vya Siasa, vikiwajulisha viwaandae watu wao kushiriki Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuanzia Juni 16-Julai 16, mwaka huu; Jambo ambalo zoezi hilo lilikwama kwa kukosa Wino na Vifaa vingine.

Chadema Mvomero; NEC inafanya Zoezi la BVR kwa Zimamoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero Wallace Karia


‘Zoezi la Uandikishaji lakwama kwa kukosa Wino’!.

Na Bryceson Mathias, Mvomero Morogoro.
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ramadhani Mrisho, ameuponda Utendaji wa Tume ya Uchaguzi (NEC) akidai, Kitendo cha kushindwa kuanza kuandikisha Wapiga Kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration ((BVR) 16/6/2015, inaonesha inafanya kazi hiyo kwa Zimamoto.

Kauli Mrisho kuiponda NEC na Watendaji wake kuwa si lolote wala chochote, linatokana na Zoezi hilo lililotarajiwa kuanza katika Jimbo lake la Mvomero Juni 16 hadi Julai 16 mwaka huu, kukwama kufanyika kutokana na kukosekana kwa kitu kidogo tu, ati ‘Wino’.

“Serikali kupitia Ofisi ya Utawala wa Mkoa wa Morogoro iliviarifu Vyama kwa Barua kwamba, Viaandae Mawakala wao kama makubaliano yalivyofanywa na Vyama hivyo, lakini tunaambiwa Mashine zaidi ya 80 zimefika kwa Mshangao tunataarifiwa Wino hakuna, si Usanii huu?

“Hii inadhihirisha jinsi ambavyo NEC haijajipanga, na kwamba inafanya Zoezi hili kwa Shinikizo la Mtindo wa Zimamoto. Kwa nini Mashine ziwepo halafu Wino ukosekane kama wana Mpango Kazi wa kufahamu Idadi ya watu fulani wanatumia Wino Kiasi gani? Alisema Mrisho.

Mrisho alisema kuwa, Kutokana na hali hiyo, imefahamika kwamba, zoezi hilo lingesababisha siku tatu za Uandishaji 16-19 lisimame huku wino huo ukisubiriwa, ambapo pia imefahamika kwamba, siku tatu zitakazopotea zitaongezwa ili kufidia uzembe wa makosa hayo.

Wakizungumza na Tanzania Daaima kwa nyakati tofauti, Wananchi na Viongozi wa Vyama Vyote vya Siasa Mvomero, wakiwemo Madiwani, Wenyeviti na Watendaji wa Kata, Vjijiji, Vitongoji, Wameishushia Lungu la lawama (NEC) wakidai, kukosekana kwa Wino, inaonesha watendaji hao wasivyo wajibika, kwa kudhani kazi hiyo ni ya Mzaha.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero,Wallace Karia alipotakiwa kutoa majibu Wino huo utapatikana lini kuwaondoa wasiwasi wananchi, alipopigiwa simu yake ya Kiganjani 0754-339995 atoe ufafanuzi huo, simu yake ililia bila majibu na baadaye alijibu kwa SMS ‘I’am Driving’.

MBOWE ATHIBITISHA KUGOMBEA UBUNGE HAI 2015; AWAPA GARI LA KUZOLEA TAKA

Siku moja baada ya kuhukumiwa kulipa faini Sh1 milioni au kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la shambulio la kawaida dhidi ya aliyekuwa mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu uliopita, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.

Mbowe aliyeepuka kwenda jela kwa kulipa faini hiyo juzi, alitangaza uamuzi huo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la stendi ya zamani mji mdogo wa Bomang’ombe, Kilimanjaro.

Mwenyekiti huyo alifikia hatua hiyo baada ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo kumshinikiza agombee ubunge na kumchangia Sh800,000 za kuchukua fomu ambayo ndani ya Chadema hugharimu Sh250,000.

“Nashukuru kwa walioanzisha wazo hili lakini zaidi ninawashukuru waliojitolea kunichangia fedha. Nimekubali nitagombea ubunge katika uchaguzi ujao,” alitangaza Mbowe na kufanya uwanja kulipuka kwa shangwe.

Mbowe aliyeambata na wabunge kadhaa akiwamo Philemon Ndesamburo wa Moshi Mjini, alijinasibu kuibuka na ushindi wa kishindo yeye na chama chake katika uchaguzi ujao kuanzia jimbo la Hai na katika majimbo yote ya Mkoa wa Kilimanjaro.

“Kama sheria ingekuwa inaruhusu ningefurahi iwapo CCM ingesimamisha wagombea zaidi ya 10 katika Jimbo la Hai ili wapambane na mimi kwa sababu mgombea mmoja pekee siyo saizi yangu,” alijinasibu Mbowe.

Hukumu dhidi yake
Akizungumzia hukumu iliyomtia hatiani na kuhukumiwa faini au kifungo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema alikusudia kwenda jela kuwakilisha mamilioni ya Watanzania wanaosota huko “kwa kesi na hukumu za kipuuzi”.

“Kama kesi ya mtu mwenye dhamana ya uwakilishi wa wananchi kwa nafasi ya ubunge inaweza kuendeshwa kwa zaidi ya miaka minne na hukumu kutolewa katika mazingira tatanishi kama ilivyokuwa kwangu, Watanzania wa kawaida wanateseka kiasi gani?”
alihoji Mbowe.

Alidai kuwa baada ya kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja au faini ya Sh1,000,000, Hakimu Denis Mpelembwa amepandishwa cheo kuwa hakimu mkazi na kuhamishiwa mkoani Kagera, siku moja tu baada ya hukumu.

“Kilichokuwa kinatafutwa ni namna ya kumzuia Mbowe asigombee ubunge Hai kwa sababu CCM wanajua nguvu yangu. Wamekosea sana kwa sababu hukumu ile hainizuii kugombea. Nitaombea na nitashinda kwa kishindo,”
“Ninao wanasheria mahiri ambao baada ya kupitia hukumu yangu kwa harakaharaka, wamenihakikishia kwamba adhabu ile hainizuii kugombea na wanaendelea na taratibu nyingine za kisheria kuiomba Mahakama Kuu kuitangaza kuwa batili,” alisema.

Atoa gari la taka
Katika tukio jingine, mbunge huyo alikabidhi gari na mtambo wa kukusanya na kusindika taka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni.



“Gari hili nimelinunua kwa fedha zangu na kulipa gharama zote na ushuru baada ya Serikali kuniwekea mizengwe. Nalikabidhi kwa halmashauri kusaidia kuzoa taka ili kuweka jimbo letu katika hali ya usafi kama ilivyo kwa Manispaa ya Moshi,”
alisema Mbowe.

Wabunge wanena
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wabunge waliohudhuria mkutano huo, Pauline Gekul, Grace Kiwelu, Rose Kamili na Joseph Selasini waliwaomba wakazi wa Hai kuhakikisha Mbowe anarejea tena bungeni kutokana na uwezo wake wa kiuongozi.

“Ili tufanikishe lengo la kumrejesha Mbowe bungeni na wagombea wengine wa Chadema, mnatakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga na kulinda kura Oktoba 25, mwaka huu,”
alisema Gekul.


Mbowe amalizana na mahakama.

Ahukumiwa jela mwaka au faini milioni moja.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (53), amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Shilingi milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia Mwangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Nassir Uronu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro jana.
Hata hivyo, Mbowe alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha faini na hivyo kuepuka kwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Mbowe alikuwa akikabiliwa na kesi namba 73 ya mwaka 2011 iliyofunguliwa na Nassir; aliyedai kushambuliwa kwa kipigo akiwa katika Zahanati ya kijiji cha Nshara kata ya Machame Kaskazini Wilaya ya Hai, mwaka 2010.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya za Hai na Siha, Denis Mpelembwa, alisema mahakama hiyo imemtia hatiani Mbowe kwa kosa la kumshambulia Nassir kinyume cha kifungu cha 24 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 cha Sheria iliyofanyiwa Mrekebisho mwaka 2002.

“Mahakama imekuona una hatia katika kosa linalokukabili na inakuhukumu kulipa faini ya Shilingi milioni moja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela,” alisema Hakimu Mpelembwa.

Awali, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Issa Rajabu, aliyekuwa akisaidiana na Wakili Albert Msando; aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu mteja wake (Mbowe), kwa madai kwamba ni kosa lake la kwanza.

Kesi hiyo ya uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikivuta hisia za wakazi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga hasa kutokana na nguvu ya kisiasa aliyonayo Mwenyekiti huyo wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Katika uchaguzi huo, Nassir alikuwa Mwangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu akiliwakilisha Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Hata hivyo, Mbowe aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Hai kwa tiketi ya Chadema, aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585, akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM), kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) 258 na Petro Kisimbo (TLP) kura 135.

Wakili wa Jamhuri katika kesi hiyo, Simon Feo, ambaye ni Mwendesha Mashitaka wa Polisi, aliieleza mahakama hiyo kwamba kutokana na ukubwa wa kosa, anaiomba mahakama impatie adhabu stahiki kwa vile makosa kama hayo yanaharibu taswira ya jamii na hasa ikizingatiwa kuwa Mbowe ni kiongozi wa kitaifa.

Baada ya Hakimu Mpelembwa kumaliza kusoma hukumu hiyo, Mbowe alitolewa nje ya mahakama chini ya ulinzi mkali wa Polisi waliokuwa wameimarisha ulinzi katika viunga vya mahakama hiyo na kumshikilia kwa zaidi ya saa mbili; hadi alipofanikiwa kulipa faini ya Shilingi millioni moja na kuachiwa huru.

Akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, wanachama na wafuasi wa Chadema waliofurika mahakamani hapo, walilazimika kujichangisha na kisha kulipia faini hiyo kupitia Benki ya NMB na baadaye kuwasilisha mahakamani stakabadhi yenye namba 0317489.

Thursday, June 18, 2015

Nape Nnauye tulia, Muosha Huoshwa. Dr.Slaa alisafiri kikazi

Baada ya Dr.Slaa kurejea nchini akitokea Bara Ulaya alipokuwa kikazi kulingana na ratiba yake ya kiutendaji ,Nape Nnauye amenukuliwa kwenye mikutano ya hadhara akitoa tuhuma za uongo na uzushi kuwa ameenda Ulaya kuomba fedha za kampeni na kupewa masharti hatarishi kwa nchi yetu na kudai kuwa yeye na chama chake wanao ushahidi

Inashangaza sana katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama tawala anapojikita katika uzushi na kuropoka uongo majukwaani badala ya kunadi sera na itikadi ya chama chake ,inakua msiba zaidi kwa vijana na kwa taifa inapokua kwamba aliyefanya hivi ni kijana msomi

Anaidhalilisha serikali yake kuwa haina uwezo wa kupata taarifa muhimu za usalama wa nchi.Kama Dr.Slaa anaweza kusafiri kutoka hapa Tanzania hadi Ulaya kisha anaomba fedha na kupewa masharti hatarishi bila usalama wa taifa kujua,bila balozi zetu nje ambako kuna Mwambata wa Jeshi(Defence Attache') kwenye balozi zetu zote huko nje ,je taifa letu ni salama? Je,usalama wa nchi yetu katika mikono ya CCM ni wa kiwango gani? Mbona hajakamatwa hadi sasa na badala yake viongozi wa chama tawala wanazusha na kuhadaa watu kuwa wanao ushahidi ambao walipaswa kuupeleka kwenye vyombo vya dola?

Ni vyema watanzania hasa wale wana-CCM waaminifu kabisa wakakumbuka kuwa ni Nape huyu huyu ambaye amekua mstari wa mbele kujifanya ana uchungu sana na CCM kiasi cha kuwatukana wana-CCM wenzake akina Edward Lowassa na pia kuwafanyia fitna vijana wenzake ndani ya chama akina Mwigulu Nchemba na January Makamba wanaonekana kufanya siasa za kisomi

Anachofanya sasa ni kutapatapa baada ya kujua mradi aliokua akizunguka nao nchi nzima wa kuvua gamba sasa unamtokea puani na hali yake kisiasa na mustakabali wa nafasi aliyonayo umefika ukingoni

Amegundua kuwa kashfa zake dhidi ya makada wenzake kuwa 'Hawasafishiki hata kwa dodoki" zinaelekea kumrudia sasa anaamua kutafuta uongo na uzushi kama ilivyo kawaida ya wanasiasa waliofilisika kisiasa

Mathalani,Mwana-CCM na Mtanzania makini atajiuliza kama makada wenzake ni wachafu na wanakichafua chama chake ,je yeye aliyeanzisha chama cha CCJ na kutaka kukipasua chama cha Mapinduzi ana maadili au usafi kiasi gani cha kuwatukana wenzake kuwa ni magamba wasiosafishika kwa dodoki?

Je,kwa mradi wake wa chama cha CCJ alichokiasisi akiwa ndani ya CCM atasafishika hata kwa Msasa?

Tumshauri,tumuonye na kumuelekeza kijana huyu mwenzetu katika siasa za kisayansi na kuitendea haki fursa aliyopewa ili vijana tuendelee kuaminika na kupewa mamlaka katika vyombo vya maamuzi

Tutaendelea kukutana Mitandaoni na majukwaani sasa

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

Ben Saanane

MBUNGE WA ARUSHA MJINI MHESHIMIWA GODBLESS LEMA ALALAMIKIA UKIUKAJI WA TARATIBU KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA WANANCHI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA ARUSHA

Wednesday, June 17, 2015

MTIA NIA WA UBUNGE JIMBO LA KILOSA RAJAB MSABAHA KAUZELA AENDELEA NA ZIARA ZA UFUNGUZI WA MATAWI YA CHADEMA JIMBONI KILOSA

Mwanachama wa CHADEMA akiandaa bendera tayari kwa ufunguzi wa Tawi la Chadema Jimboni Kilosa


Mtia ni wa Ubunge Kilosa Ndugu Rajab Msabaha Kauzela akipandisha bendera kama ishara ya ufunguzi wa Tawi la Chadema katika mwendelezo wa ziara zake za ufunguzi wa matawi ili kujenga chama Jimboni Kilosa


Wananchi waliofurika kushuhudia ufunguzi wa Tawi Jipya la Chadema moto wa gesi Jimboni Kilosa
Ndugu Kauzela akihutubia wakazi wa Kilosa katika ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Jimboni Kilosa


Ndugu Kauzela akisalimiana na viongozi wa CHADEMA waliohudhuria ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Jimboni Kilosa