Sunday, December 27, 2015

DIWANI WA CHADEMA AKATAA KUPOKEA POSHO ZA VIKAO

Diwani wa kata ya Gangilonga, Iringa Mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Daddy Igogo amesema hatapokea posho za vikao vyote vya baraza la madiwani katika kipindi chake cha miaka mitano na badala yake ametaka zitumike kuwasaidia watoto wanaoshi katika mazingira magumu katika kata yake.

Diwani huyo mdogo kuliko madiwani wote wa halimashauri hiyo ambaye pia ni Mwalimu katika Chuo Kikuu cha Ruaha, Iringa anakuwa diwani wa kwanza nchini kukataa posho hizo huku baada ya Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu (CCM) naye kukataa kupokea posho kama hizo katika kipindi chote atakachokuwa mbunge wa jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya kata ya Gangilonga Igogo alisema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili kusaidia yatima na kuunga mkono ilani ya chama chake ya uchaguzi wa 2010 na 2015 ya kukataa posho ya vikao na kwamba ameshamuandikia mkurugenzi barua inayompa maelekezo ya wapi posho hizo zipelekwe.

Igogo alisema kuwa posho ya vikao ni ugonjwa wa ufisadi unaolitafuna taifa kila kukicha hususani kwa watendaji wa mashirika ya umma ,watendaji wa serekali kuu huu na kumpongeza Raisi John Magufuli kwa kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa fedha nyingi zaidi zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Alisema posho za wabunge zinalingana na bajeti ya sensa ambapo Taifa lilikwenda kukopa baadhi ya fedha ili kuendeshea zoezi hilo huku wastani wa posho kwa za madiwani na watendaji katika manispaa ya Iringa kwa mwaka zinauwezo wa kusomesha zaidi ya wanafunzi 400 wa shule za sekondari kwa ada ya shilingi eflu 20,000 kwa kila mmoja na fedha zikabaki

Hata hivyo Igogo aliwaomba madiwani wa chama chake na mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Piter Msigwa na wabunge wote wa viti maalumu kuwa sehemu ya kupinga uendelezwaji wa posho zisizo za msingi ili kuonyesha dhamira ya dhati katika kuwatumikia watanzania

Katika vhatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Iringa mjini ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi amesema uamuzi aliochukua diwani huyo ni mzuri na ni maamuzi yake ila yeye hana mpango wa kugomea kuchukua posho hizo.

Friday, December 25, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU MIKUTANO YA HADHARA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU
KAULI YA WAZIRI MKUU MIKUTANO YA HADHARA



Tumeona kupitia vyombo vya habari na njia mbalimbali za upashanaji taarifa kwamba Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amenukuliwa akitoa kauli inayoonesha Serikali ya CCM inataka kuzuia shughuli za kisiasa hususan mikutano ya hadhara.

Kupitia kauli hiyo, Waziri Mkuu amenukuliwa zaidi akisema kuwa Uchaguzi umekwisha hivyo sasa si wakati wa siasa bali maendeleo.

Hii ni kauli ya ajabu kutolewa na mtu anayesimamia utendaji wa shughuli za kila siku za serikali inayotaka kuwaaminisha kuwa itakuwa tofauti na serikali zingine zilizopita za CCM.

Kupitia taarifa hii, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tunailaani na kuipinga kwa nguvu zote kauli hiyo yenye chembe za udikteta iliyotolewa na Waziri Mkuu Majaliwa.

Inaonekana imetolewa na mtu ambae ameanza kulewa madaraka mapema sana huku akisukumwa na utashi wa kisiasa wa kuiokoa CCM kwenye kasi ya kufa kisiasa na kulinda udhaifu wa serikali yao ambao umeshaanza kuonekana wazi kupitia kila hatua wanayochukua na matamko wanayotoa.

Kama wao (CCM) ndiyo walioshinda kama ambavyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema na kwamba wanaendelea kutekeleza wajibu waliokabidhiwa na wananchi, tunahoji hofu yao nini hasa wakiona au wakisikia CHADEMA wanapanga kwenda kuongea na wananchi? Wanaogopa nini?

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa imekuja siku chache tu baada ya kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ambaye anatazamiwa kuwa mtumishi wa Watanzania wote bila kuwabagua kwa itikadi za kisiasa, kabila wala dini, kuwa ametoa upendeleo kwa chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM kuhutubia na kufanya siasa kwenye mkutano wake mjini Lindi, ambapo Nape Nnauye alitumia jukwaa hilo la kiserikali kuzungumza kama kiongozi wa CCM akiwajibu viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA.

Matukio haya yanaanza kumdhihirisha Waziri Mkuu Majaliwa ni kiongozi mwenye uelekeo wa namna gani hivyo kuanza kuifunua Serikali ya Rais John Magufuli chini ya CCM kwa miaka mitano ijayo itawapeleka wapi Watanzania.

Ni dalili za wazi za watu waliolewa madaraka na
kuchoka kuwa viongozi na sasa wanataka kuwa watawala wenye kudhani kuwa fikra zao ndizo zinazongoza nchi badala ya misingi ya inayokubalika miongoni mwa jamii nzima kupitia Katiba, Sheria, Kanuni na taratibu mbalimbali.

Tunatumia fursa hii kusisitiza kauli yetu kwamba walioko madarakani wanapaswa kutambua kuwa siasa haina msimu wala haianzi na kuishia wakati wa uchaguzi kwa sababu siasa ni mfumo wa maisha ya binadamu kila siku. Si suala la kupenda au kutokupenda.

Uchaguzi pia ni mchakato. Mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine kwa haraka kwa wadau wote, vikiwemo vyama vya siasa na vyombo vingine au taasisi zingine zote zinazohusika. Kuendelezwa kwa fikra za namna hiyo za Waziri Mkuu ndiyo kunasababisha Serikali na taasisi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuvunja sheria za nchi kwa kushindwa kuandikisha wapiga kura kama inavyotakiwa baada ya uchaguzi kumalizika.

Aidha kuheshimu misingi ya demokrasia, ikiwemo ushindani wa (hoja, sera, mikakati, mipango) wa vyama vingi, si suala la utashi wa walioko madarakani bali ni haki ya msingi ya kibinadamu na kikatiba na matakwa ya wanananchi wanaotoa dhamana ya watu kukaa madarakani kuongoza kwa niaba ya wengine.

Je Waziri Mkuu anataka kuwaambia Watanzania kuwa anatofautisha siasa na maendeleo? Je anataka kusema kuwa haki ya vyama vya siasa kukutana na kuzungumza na wananchi itabakia kwa CCM tu kwa miaka mitano ijayo? Anajua hilo halitakubalika.

Ni vyema Waziri Mkuu akatambua kuwa nchi hii haiko kwenye fikra wala mfumo wa chama kimoja tena.

Imetolewa leo Alhamis, Desemba 24, 2015 na;

Idara ya Habari na Mawasiliano

CHADEMA

Tuesday, December 22, 2015

MALALAMIKO KUHUSU UKANDAMIZAJI WA DEMOKRASIA KATIKA CHAGUZI MBALIMBALI ZINAZOENDELEA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Masuala 2

1. Sintofahamu katika chaguzi za kuwapata wenyeviti/makamu wenyeviti wa halmashauri na Mameya/manaibu meya katika maeneo ambayo UKAWA umeshinda.

2. Ukandamizaji wa demokrasia jimboni kwa Waziri Mkuu.

Kumekuwa na kila dalili za uminywaji na ukandamizaji mkubwa wa demokrasia katika maeneo yote ambako vyama vinavyounda UKAWA vimeshinda idadi kubwa ya madiwani na kuwa na uhalali wa kuongoza halmashauri/manispaa au jiji.

Kilichotokea katika uchaguzi wa kumpata Meya wa Jiji la Tanga juzi Jumamosi, Novemba 19, 2015 ni mwendelezo wa njama na hujuma za makusudi zinazopangwa na watawala wakiwatumia wakurugenzi na vyombo vya dola, kwa namna ile walivyofanya wakati wa Uchaguzi Mkuu, kupora haki za raia Watanzania wanyonge walioamua kuchagua UKAWA, wakiamini katika mabadiliko ya kweli dhidi ya maneno tupu ya CCM.

Hujuma za namna hiyo za watawala ndizo zimefanyika maeneo mengine ambayo wananchi wamechagua UKAWA uwaongoze, mf; Kyerwa-Kagera, Kilombero, Ilala, Kinondoni n.k ambako hadi sasa uchaguzi bado uko kwenye sintofahamu kubwa kwa kile ambacho kinaonekana wazi ni kutaka kuibeba CCM kwa nguvu baada ya kuwa imekataliwa na wananchi katika maeneo husika.

Ni suala linalofikirisha sana kwamba hujuma hii dhidi ya demokrasia ambayo kimsingi ni ubabe dhidi ya wananchi waliotumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka, inafanyika huku Ofisi ya Rais, ambayo ndiyo inasimamia Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa kupitia Wizara ya TAMISEMI, ikiwa kimya jambo ambalo linaashiria mambo matatu;

1. Kuwa sintofahamu inayosababishwa na hujuma hizo ni matokeo ya maelekezo au ina baraka kutoka ofisi hiyo.

2. Wizara hii tayari imemshinda Rais John Magufuli kiasi cha watendaji walio chini yake, hususan Wakurugenzi kujifanyia mambo kadri wanavyotaka kwa ajili ya kuibeba CCM, jambo ambalo ni kero nyingine kwa wananchi katika maeneo mbalimbali. Vinginevyo ni vigumu kuelewa kwamba mathalani hadi sasa takriban mwezi mzima na zaidi eti Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshindwa kumpata DED wa Halmashauri ya Kyerwa, Kagera (au DED huyo amegoma) ili tu athibitishe kama kweli CHADEMA ina madiwani wengi kuliko CCM ambayo ina madiwani wachache lakini 'imezawadiwa' na NEC madiwani wengi wa Viti Maalum, kinyume kabisa na utaratibu, ili kuongeza kura za hujuma kisha iongoze Halmashauri ya Kyerwa badala ya CHADEMA ambayo ndiyo yenye madiwani wengi.

3. Mganga hajigangi, hivyo Rais Magufuli ameshindwa kutumbua jipu ambalo liko ofisini kwake. Kushindwa kusimamia shughuli zilizoko chini ya TAMISEMI, tena nyeti kama hiyo ya kuwapata viongozi wa serikali za mitaa watakaosimamia shughuli za maendeleo ya wananchi katika maeneo wanayoishi, ni jipu kubwa linalohitaji mtumbuaji. Tunataka kujua nani atakuwa anatumbua majipu yanayobainika kupewa nafasi ofisini kwa Rais?

2. Uminywaji wa demokrasia jimboni kwa Waziri Mkuu.

Siku ya jana na leo tumepata taarifa kutoka kwa viongozi wa chama katika maeneo ya Jimbo la Ruangwa ambalo anatokea Waziri Mkuu Majaliwa Kasimu Majaliwa, kuwa kumekuwa na operesheni ya kushusha bendera na kuvunja vijiwe (ngazi ya misingi) vya CHADEMA hasa katika maeneo ya Nandagala, Mnacho n.k.

Mbali ya kusikitishwa na jambo hilo, tunalaani vikali hatua hiyo ambayo tumeambiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkurugenzi kwenda kwa Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Kata, hususan wakati huu ambapo Waziri Mkuu yuko ziarani Mkoa wa Lindi ambayo itamfikisha nyumbani, huko Ruangwa.

Tunawataka watendaji wa Serikali katika eneo hilo kuacha mara moja ukiukwaji huo wa demokrasia hasa kwa kukilenga CHADEMA huku wakiacha CCM ikiendelea kufanya kazi zake za kisiasa.

Tunatoa wito kwa Waziri Mkuu kuona fahari demokrasia ikishamiri katika jimbo lake na yeye akubalike kwa uhalali wa kisiasa kutokana na kukubalika kwake kwa wananchi badala ya vitisho kutumika kuua ushindani wa demokrasia ya vyama vingi kwa kuhujumu chama kinachoonekana kutishia uwepo wa CCM jimboni na hata nyumbani kwake. Tunamuomba asiache kumbukumbu mbaya kama ya aliyemtangulia, Mizengo Pinda, ambaye baada ya kuona CHADEMA ina ushawishi mkubwa katika mtaa wa nyumbani kwake hapa Dar es Salaam na hata kijijini kwao huko Katavi, aliingilia uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana ili tu atangazwe Mwenyekiti wa Mtaa anayetokana na chama chake hata kama hakupewa ushindi na wananchi.

Tunaamini kuwa kama demokrasia ni moja ya misingi muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote, viongozi wa serikali wanapaswa kuwa watu wa kutiliwa mfano kuiheshimu kwa maslahi mapana ya Watanzania na hawataweka matakwa ya CCM mbele.

Imetolewa leo Jumatatu, Desemba 21, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Monday, December 21, 2015

OMBI LA WABUNGE NA MADIWANI WA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI KUIOMBA IKULU (OFISI YA RAIS) IUNDE TUME HURU


LEO MADIWANI NA WABUNGE WA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI
tumeiomba Ikulu (OFISI YA RAIS) iteue TUME HURU YA UCHUNGUZI "a free and independent inquirery Commission" dhidi ya tuhuma za mkurugenzi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zake 3:-

(i) Uduni wa ubora wa barabara zilizo jengwa manispaa yabkinondoni na kushindwa kuwaadhibu wahandisi wahusika

(ii) Kushindwa kusimamia idara ya ardhi na mipangomiji ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi,


(iii) Kukosa uadilifu katika ubinafsishwaji wa fukwe za cocobeach

UKAWA MANISPAA YA KINONDONI,tumegundua kuhusishwa na siasa za baada ya uchaguzi,kwa kuwakomoa,kufitinisha na kuadhibu wakurugenzi walioshindwa kuzuia UKAWA tusitangazwe kwenye uchaguzi mkuu 2015,sasa kwakubambikiwa tuhuma na kuhusishwa na ufisadi au uzembe......pia tumekiri ambapo tume itagundua mkurugenzi alikuwa na hatia ya ufisadi au uzembe pia awajibishwe kulingana na alichokitenda kwakuwa si dhumuni letu kutetea ubadhirifu au ufisadi

Tumekataa TAMISEMI kuhusika na hatua zinazofuata kwa uchunguzi kwakuwa wanajua kila kitu kinachoendelea katika UFISADI wa fukwe za COCOBEACH,kwakuwa ukweli wanaujua ila wameuficha na kumzunguka mheshimiwa Rais na kubambikia wengine.

TUMEUWEKA HADHARANI MAKATABA WA COCOBEACH,wananchi waone waliobinafsisha fukwe yaCOCOBEACH 2007, NA Majina ya waliotia saini mkataba huo mwaka 2007,wakati mkurugenzi Eng MUSSA NATTY,Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa KINONDONI 2013.

Ukweli huu wa kusingiziwa swala la cocobeach uwe chachu ya Tume kutafuta ukweli halisi wa tuhuma zingine,kwa kuwa TAMISEMI walihusika kila hatua ya uuzaji wa fukwe hizo.

TUPAMBANE KUTETEA HAKI YA MKISI NA WATU WA VWAWA.


Malisa GJ

Naandika haya nikiwa na uchungu mwingi nafsini. Kuna mambo yanayofanywa na serikali ya CCM yanatia hasira, yanaudhi, yanakatisha tamaa. Naomba nitumie fursa hii kumshauri Rais Magufuli kuwa akiendelea kukaa kimya kwenye mambo haya wananchi watapoteza hata ile imani kidogo waliyoanza kuionesha kwake.

Vitendo vya ukiukwaji wa wazi wa demokrasia ktk chaguzi mbalimbali ni mambo ya kawaida sana kwa viongozi wa CCM. Kuanzia uchaguzi mkuu hadi chaguzi za Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri tumeona namna CCM wanavyotumia nguvu kubwa kupora madaraka.

Jambo kubwa nililojifunza ktk uchaguzi huu ni kuwa ili uweze kuishinda CCM inabidi ushinde kwa kura nyingi sana. Ukishinda kwa tofauti ya kura chache ujue umeumia. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa rafiki yangu Fanueli Mkisi MBUNGE HALALI wa jimbo la Vwawa.

Mimi na vijana wenzangu wa CHADEMA tulifanya ziara nchi nzima tukinadi wagombea Ubunge, Udiwani na Rais ktk majimbo 19 nchini. Kati ya wagombea 19 wa Ubunge tuliowanadi, 16 walishinda kwa kishindo na watatu hawakutangazwa washindi japo kiuhalisia walishinda. Mmojawapo kati ya hao watatu ni Mhe.Fanuel Mkisi Mbunge halali wa Vwawa.

Moja ya majimbo ambayo nilijua tutashinda mapema sana ni pamoja na jimbo la Vwawa kwa Mkisi. Na ndivyo ilivyotokea. Katika vituo vyote vya kupigia kura Mkidi alikua anaongoza kwa kura nyingi sana dhidi ya Japhet Hasunga wa CCM. Hata fomu za matokeo walizosaini mawakala zinsonesha hivyo.

Kwa hiyo hata kabla matokeo rasmi hayajatangazwa wananchi wa Vwawa walikua wameshaanza kushangilia barabarani na maeneo mengine ya wazi. Lakini katika hali isiyotarajiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi akatangaza kuwa Japhet Hasunga (CCM) alishinda kwa kupata kura 36,705 dhidi ya Fanuel Mkisi (CHADEMA) kura 35,400. Tofauti ya kura 1,200.

Huu ulikua wizi wa mchana kweupe na wananchi wa Vwawa hawakua tayari kuuvumilia. Hivyo wakafunga barabara na kushinikiza mshindi halali (Mkisi) atangazwe. Lakini Polisi wakaishia kuwapiga mabomu na wakamsaidia Mkurugenzi kutoroka baada ya kutangaza matokeo hayo "feki".

Zipo taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alipewa maagizo kuwa ahakikishe anamtangaza Hasunga kuwa Mshindi wa Vwawa kwa kuwa jimbo pacha la Mbozi tayari CCM walikwishapoteza.

Taarifa nyingine zinadai kuwa Ofisi ya Mkoa ilipewa maagizo kuwa ihakikishe CCM wanashinda zaidi ya nusu ya maJimbo ya mkoa Mbeya ili kupunguza nguvu ya upinzani. Ndio maana majimbo mengi CCM waliyotangazwa washindi wameshinda kwa tofauti ya kura chache sana. Hii ni dalili ya wazi kuwa hawakushinda kihalali.

Kwa sababu mgombea wa CCM akikushinda kwa kura moja anandikiwa 10. Ndio maana Lowassa alisema njia pekee ya kuishinda CCM kwa Katiba ya sasa ni kupata kura nyingi hadi washindwe kuiba. Yani wakiiba waone aibu. Kwa mfano ukipata kura 20,000 na mgombea wa CCM akapata kura 350 hapo anaibaje? Lakini ukipata kura 20,000 na CCM 19,000 ujue hapo atakayetangazwa mshindi ni CCM. Hivyo ndivyo Tume ya Uchaguzi isivyoheshimu demokrasia ya watu wake.

Kwahiyo Mkisi alishinda kwa zaidi ya kura 3000 lakini AKAPORWA USHINDI na Hasunga wa CCM akatangazwa mshindi. Karatasi za matokeo zilizosainiwa na mawakala zinaonesha Mkisi ndiye mshindi, karatasi zilizobandikwa nje ya vituo zinaonesha Mkisi ndiye Mshindi. Masanduku ya kura yanaonesha Mkisi ndiye Mshindi. Sasa Mbona ametangazwa mwingine? Haya ni maswali ambayo kila mpenda demokrasia anajiuliza.

Lakini kwa kuwa vipo vyombo vya kudai haki, Mkisi akaamua kwenda Mahakamani kudai haki yake. Akafungua Shauri Mahakama kuu kanda ya Mbeya akiwa na Jopo la Mawakili wanaomtetea akiambatanisha vielelezo vyote muhimu vinavyoonesha kuwa yeye ni Mshindi halali wa ubunge jimbo la Vwawa.

Lakini ktk hali ya kusikitisha Mahakama nayo inaonekana kutaka kuzuia haki ya Mkisi na wananchi wa Vwawa. Ktk hali isiyotsrajiwa Mahakama hiyo imeweka gharama kubwa sana za kusikiliza kesi hiyo (Cost for Security) kinyume na maombi ya mlalamikaji (Mkisi).

Mkisi aliomba Cost for Security iwe Tsh. Milioni 3 kama ambavyo wagombea wengine wamefanyiwa. Lakini Mahakama imekataa ombi lake na kumtaka alipe Tsh. Milioni 9 ndani ya siku 14 ili kesi yake iweze kusikilizwa.

Hizi ni dalili za wazi kuwa Mahakama imetumika kisiasa. Haiwezekami wagombea wengine watozwe Mil.3 then Mkisi atozwe Mil.9. Bila shaka Mahakama imetoa maagizo haya baada ya kuona kuwa wakitaja fedha ndogo Mkisi atazilipa na kesi yake itasikilizwa na ATASHINDA.

Kwa hiyo njia rahisi ya kumnyang'anya HAKI yake ni kumtajia kiasi kikubwa cha pesa ili ashindwe kulipa na hivyo kesi hiyo itupiliwe mbali. Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha ukiukwaji wa misingi ya utu ktk mchakato wa demokrasia.

Nimezungumza na rafiki yangu Mkisi leo amesema hadi sasa amefanikiwa kupata Mil.4.7 tu. Ikumbukwe deadline ni jumanne ya tarehe 22 mwezi huu, na bado mil.4.3 kufikisha Mil.9 zinazohitajika na Mahakama.

Nichukue fursa hii kwa moyo wa unyenyekevu kabisa niwaombe ndugu jamaa na marafiki watakaoguswa kutoa chochote kumsaidia Mkisi afikishe kiasi hicho kinachohitajika na Mahakama ili kesi yake iweze kusikilizwa.

Nina uhakika kuwa kesi hii ikisikilizwa Mkisi atashinda na atatangazwa kuwa MBUNGE HALALI WA VWAWA.

Biblia inasema katika kitabu cha Mithali 10:3 kuwa "BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali."

Kwa scenario ya Vwawa "mwenye haki" ni Mkisi na "mtu mwovu" ni Hasunga. Tusiiache nafsi ya Mkisi ikaangamia bali tuisukumie mbali tamaa ya mtu mwovu (Hasunga). Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefanya kazi ya kitume na thawabu yake ni kubwa.

Pia nitoe wito kwa Wabunge wote wa Mkoa wa Mbeya washikamane kuwasaidia kina Mkisi na wengine wanaodai haki zao Mahakamani baada ya kuchakachuliwa. Joseph Mbilinyi (Sugu), Pascal Haonga, Silinde Ernest David, Frank Mwakanjoka, yangu Sophia Hebron na wengine naomba muwashike mkono kina Mkisi.

Kwa atakayeguswa na kupenda kuchangia chochote ili kuhakikisha haki ya Mkisi na watu wa Vwawa haipotei atume mchango wake moja kwa moja kwa Fanuel Mkisi kupitia namba 0766800090.

Kumbuka kesi imepangwa kusikilizwa jumanne tar.22, this means tuna siku moja tu kutafuta mil.4.3 ili kutimia mil.9 zinazohitajika. Otherwise HAKI ya watu wa Vwawa itakua imepotea.

Asanteni sana na Mungu awabariki,
Malisa GJ.!

Sunday, December 20, 2015

Lowassa afurahia tuzo

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ameishutumu serikali kwa kuwakataza kufanya mikutano ya kuwashukuru wananchi na ameifananisha hatua hiyo sawa na uoga usio na msingi.

Akizungumza kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Aboubakary Liongo, Lowassa alisema kuzuiwa kwake na upinzani kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wapiga kura ni uoga wa CCM na serikali yake kwa kisingizio cha vurugu.

Lowassa amerusha makombora hayo wakati akishukuru tuzo ya amani duniani anayotarajiwa kupewa na taasisi 1,200 duniani kutokana na utulivu aliouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Aliitaka serikali kuacha mabavu na uonevu na badala yake ijenge nchi kwa kuheshimu Demokrasia na haki za binaadamu huku akisisitiza kwamba tuzo aliyopewa na taasisi hizo za dini ni uthibitisho wa kutosha kwa uongo wa CCM na serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.

"Wamekuwa wakitumia mabavu kutugandamiza kwa kisingizio cha kuwa sisi ni watu wa vurugu..angalia kule Mwanza wakati wa mazishi ya Mawazo jinsi walivyotumia mabavu kuyazuia..ujinga mtupu" alisema Lowassa.

Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu,hata siku moja hataweka mbele maslahi binafsi na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.

"Baada ya kuona jinsi walivyoporwa ushindi wao wananchi na baadhi ya viongozi wazito tu..walinitaka nitoe tamko la kutaka nguvu ya umma itumike kudai ushindi wao,lakini nilikataa sikuwa tayari kuona Watanzania wakipoteza maisha..siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu,nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo," alisisitiza Lowassa ambaye alikataa kuyatambua matokeo.

Alisema anapokea kwa unyenyekevu na furaha tuzo ya amani duniani anayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini hizo.

Taasisi hizo katika Kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyounesha kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Taarifa ya Mwenyekiti wa kamati ya maadili, Amani na haki za binadamu kwa jamii Mchungaji, William Mwamalanga, ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 walioshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa amani mwaka 2015 ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.


Nipashe

MKUTANO WA MWISHO WA UKAWA WA KUFUNGA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO WA MASASI

Selemani Bungala (Bwege) wa Kilwa Kusini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) akihutubia maelfu na wakazi wa masasi jioni ya leo
Idadi kubwa ya wakazi wa jimbo la Masasi na Viunga vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa mti wa mwiba jimboni hapo katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge ndani ya Jimbo hilo la Masasi
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Jijini Dar es salaam kutoka chama cha wananchi CUF ndani ya umoja wa vyama vya UKAWA Mh MAULID MTULIA akiwahutubia maefu wa wafuasi wa vyama hivyo katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge ndani ya jimbo la Masasi ambapo uchaguzi huo unafanyika kutokana na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo EMANUEL MAKAIDI kufariki dunia wakati wa uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mh HAMIDU BOBANI akiwahutubia wakazi maelfu waliojitokeza katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Wabunge wote wa upinzani kutoka Lindi,na mtwara Pamoja na wabunge wa zanzibar pamoja na mbunge wa kindondoni Jijini Dar es salaam
Polisi wakifanya doria wakati wa mkutano  wa kufunga kampeni katika jimbo la masasi


Mbunge wa Jimbo la ndanda Mh CECIL MWAMBE akiwahutubia maelfu ya wafuasi wa vyama vya Ukawa katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la masasi,Mkutano uliofanyika katika uwanja wa mti wa mwiba Jimboni humo

Kauli ya Mbowe baada ya MCC kuzuia Trilioni 1 kwa serikali ya Tanzania

Muda mfupi baada ya Bodi ya MCC kutoa taarifa inayoonesha Tanzania haitapata msaada kutoka shirika hilo kama ilivyotarajiwa kwa ajili ya mwaka 2016, Mwenyekiti wa Chama Chadema, Freema Mbowe ametoa kauli nzito juu ya suala hilo akisema kuwa kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC.

MCC imeahirisha msada huo wa USD Mil. 472.8 ambazo ni takriban trilioni moja kwa fedha za Tanzania zilizolengwa kusaidia sekta ya nishati ya umeme hususan ule wa vijijini, katika kuunganisha wateja wapya, mabadiliko ya kimuundo ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ili lifanye kazi na kutoa huduma kwa ufanisi katika sehemu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.

Fedha hizo pia zilikusudiwa kusaidia kuanza kwa mpango mkubwa wa kuboresha sekta ya umeme nchini.2014-2024.

Mbowe amemtaka Rais John Magufuli kuchukua hatua za haraka za kiuongozi kumaliza mtanziko wa kisiasa Zanzibar kwa mshindi wa nafasi ya urais kutangazwa kutokana na uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu.

Aidha amesema kuwa Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ambayo ni mojawapo ya sababu zilizotumiwa na MCC kuahirisha msaada huo kwa Tanzania hadi itakapokuwa imefanyiwa kazi, ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano na kuzuia upashanaji wa habari miongoni mwa jamii ambayo ililenga kuweka makosa ya kijinai ili kudhibiti wapinzani wa CCM katika uchaguzi mkuu na kukipatia mazingira ya ushindi chama hicho.
“Sasa imethibitika kuwa Bodi ya MCC iliyokaa tarehe 16 Dec 2015 imeahirisha rasmi kuidhinisha msaada wa Millenium Challenge uliokuwa umekusudiwa kwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016. Sababu kuu mbili zilizosababisha uamuzi huo ni:

1. Mkwamo wa Uchaguzi wa Rais na Wawakilishi Zanzibar na

2.Matumizi mabaya ya she ria ya makosa ya mtandao hususan kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa 2015.”

“Ubabe wa baadhi ya viongozi wa CCM ni janga la Taifa. Kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC,” amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;
“Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano. Aidha, kwa makusudi kabisa inafifisha uhuru wa kupashana habari na ni dhahiri ilitungwa kwa nia mbaya ya kuthibiti kijinai uchaguzi mkuu.

“Tuliipinga sheria hii Bungeni na ikapitishwa usiku wa manane kwa ubabe wa wabunge wa CCM na hata tulipomtaka rais Kikwete asiisaini aliisaini kibabe akijua anaandaa mazingira gani ya “kihalifu”, “ amesema Mwenyekiti Mbowe.
Ameongeza kusema kuwa sheria hiyo ilitumika kuvamia vituo vya CHADEMA vilivyokuwa vikitumika kukusanya matokeo ya kura za rais na wabunge na hadi leo vijana zaidi ya 161, wakiwemo wanafunzi, wana kesi za “kubumba” mahakamani.

Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa Sheria hiyo hiyo ilitumika kuficha dhana ovu iliyotumika kuhalalisha kuvamia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilichokuwa kikiratibu watazamaji wa uchaguzi wa ndani kwa kibali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Vile vile Sheria hii imetumika kuwakamata na kuwaweka ndani na hata kuwanyima dhamana vijana wetu ambao walituunga mkono katika uchaguzi mkuu.

“Namtaka rais Magufuli achukue hatua za kiuongozi na kiutawala kwa kufanya yafuatayo:

“Kwanza aumalize mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa mshindi halali anatangazwa.

“Pili achukue hatua ya kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya makosa ya mtandao katika bunge lijalo. Aidha wale wote waliobambikiwa kesi amuamuru DPP kuzifuta kesi hizo mara moja,” amesema.

Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa Rais Magufuli hana budi kuchukua hatua hizo za haraka ili kulinusuru taifa na hasara ya kupoteza mabilioni hayo ya MCC na zaidi kuepusha kuporomoka zaidi kwa biashara ya utalii nchini Zanzibar.

Amesema katika taifa ambalo sekta ya umeme inakabiliwa na matatizo makubwa katika uzalishaji, usambazaji na usafirishaji huku wananchi wa kipato cha chini wakibebeshwa mzigo mkubwa wa kumudu nishati hiyo na wengine wakilazimika kutumia nishati mbadala kama mkaa unaotokana na miti hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira, serikali inayojua wajibu wake yenye viongozi wanaothamini uwajibikaji, haikupaswa kushindwa kuchukua hatua stahiki kutimiza vigezo vya msaada huo ambao umeshaisaidia Tanzania katika miradi mingine kadhaa.

Imetolewa Ijumaa, Desemba 18, 2015 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

CHADEMA

Saturday, December 19, 2015

Lissu awagalagaza wapinzani wake

JAJI wa mahakama kuu ya Dodoma jaji Seheni, ametupilia mbali maombi ya Jonathan Njau (CCM) ya kutaka apunguziwe gharama ya uendeshaji wa keshi ya kupinga uchaguzi nafasi ya ubunge dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).


Katika kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2015 Njau aliomba asitoe kiasi cha shilingi milioni 15 ambacho kipo kisheria kutokana na kutokuwa na hela kwa madai kuwa hela hizo ni nyingi na hawezi kuzipata kutokana na ukata alionao baada ya uchaguzi.

Akisikiliza kesi hiyo jaji Sheheni alisema haiwezekani kupunguza gharama hiyo kwani hipo kisheria.

Awali Lisssu aliweka pingamizi kwa madai kuwa maombi pamoja na viapo vyote vimekosewa na kuna kila sababu ya kupeleka fedha hizo ili kukithi matakwa ya kisheria.

Akizungumza nje ya Mahakama Lissu amesema: “Watu walileta maombi ya kusamehewa kulipa fedha za gharama za kesi sh milioni 15 yule bwana anayetishia wapiga kura wangu kuwa yeye ni bilionea alileta maombi ili asamehewe kwa madao ameishiwa ,sasa ameleta maombi na viapo vimekosewa na hajatimiza masharti ya kisheria.

“Kwa hiyo nilimwekea pingamizi kuwa maombi na viapo vilivyo letwa mahakamani havijafuata sheria na tukaomba yafutiliwe mbali na jaji ametukubalia kwa hiyo hakuna maombi hapa” amesema Lissu.

Amesema kutokana na kufutiliwa mbali maombi hayo sheria inaeleza kwamba isipopelekwa sh.milioni 15 kesi hakuna.

Lissu amesema kutokana na hali hiyo hakuna kesi ya msingi hakuna hadi hapo itakapokuwa imepelekwa fedha hiyo.

Lissu anasema kuwa Njau kamtuhumu kuwa aliwaonga viongozi wa dini, alinywesha watu pombe,alihonga mashuleni na kuwapiga wapiga kura.

Amesema tuhuma ambazo Lissu ametuhumiwa zinalenga kumzuia kufanya siasa kwa kipindi cha miaka 10. Hata hivyo alisema wakili Wasonga ambaye anamtetea mteja wake ambaye aligombea ubunge kupitia CCM alisha wahi kufanya makosa yale yale katika kesi ya mwaka 2010.

“Mwaka 2010 Wasonga alileta makosa yale yale yenye makosa yale yale kama haya ambayo yameletwa leo yenye makosa ambayo yamefutwa,” amesema.

MwanaHalisiOnline

Friday, December 18, 2015

TAARIFA YA JOHN MNYIKA KUHUSU KUTORIDHISHWA NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA WAZIRI WA MAJI


TAARIFA KWA UMMA

Sijaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Waziri wa Maji alipofanya ziara juzi na kunukuliwa na vyombo vya habari jana. Hivyo, naomba Waziri Mkuu achukue hatua zifuatazo:

Mosi, atake Wizara ya Maji impatie nakala ya ripoti ya uchunguzi kuhusu kukatikakatika mara kwa mara kwa maji katika mitambo na maeneo ambayo yanahudumiwa na mitambo ya Ruvu juu. Baada ya kupata ripoti hiyo atembelee katika DAWASA/DAWASCO na ‘kutumbua majibu’ ya ufisadi na udhaifu uliopo.

Pili, atembelee ujenzi unaoendelea kwenye chanzo cha Ruvu juu ambao ulipaswa kukamilika toka 2013 lakini haijawa hivyo, na katika mkutano wa mwisho wa Bunge la Kumi Wizara ya Maji iliahidi ungekamilika Agosti 2015 na haijawa hivyo pia.

Tatu, atembelee eneo la ulazaji wa Bomba kubwa jipya kutoka Mlandizi mpaka Kimara na ujenzi wa matenki mapya ambao ulipaswa kukamilika 2013, lakini haijawa hivyo, na katika mkutano wa mwisho wa Bunge la Kumi Wizara ya Maji iliahidi ungekamilika Septemba 2015 na haijawa hivyo pia.

Nne, ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji katika maeneo yasiyokuwa na “mabomba ya mchina” katika kata za Kibamba, Kwembe, Mbezi, Msigani, Saranga, Goba haujaanza kabisa. Naomba ufuatilie mchakato wake wa mkataba na vyanzo vyake vya rasilimali ili kazi hiyo ianze sanjari na bomba kuu linalolazwa ili yakamilike kwa pamoja wananchi wapate maji.

Achukue hatua zingine za ziada kwa kurejea hoja binafsi niliyoiwasilisha Bungeni tarehe 4 Februari 2013 (nimeambatanisha nakala) ambayo maelezo yake na mapendekezo yake bado ni muhimu yakafanyiwa kazi.


John Mnyika

Mbunge wa Kibamba

16/12/2015





HOJA BINAFSI YA JOHN MNYIKA KUHUSU SUALA LA MAJI



MABADILIKO KATIKA HOJA  KUHUSU HATUA ZA HARAKA ZA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA USHUGHULIKIAJI WA MAJI TAKA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
(Kwa mujibu wa Kanuni 55 (10) ya  Kanuni za Kudumu za Bunge)
Kwa kuingiza maneno:
“KWA KUWA, Programu ya Maji Safi na Mazingira Vijijini ikiwemo katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam ilipaswa kutekelezwa kuanzia mwaka 2005/2006 na kukamilika mwaka 2010/2011 kwa kugharimu dola za kimarekani milioni 292 hata hivyo tathmini ya miaka miwili na nusu ya utekelezaji (mid term review) imebanisha kasoro nyingi katika utekelezaji.
KWA KUWA, Kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 Serikali ilitekeleza Mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotumia dola milioni 164.6 hata hivyo mpaka sasa katika maeneo mengi mtandao wake maarufu kama mabomba ya wachina hautoi maji huku kukiwa na upungufu katika uzalishaji, upotevu wakati wa usafirishaji, udhaifu katika usambazaji na tuhuma za ufisadi katika matumizi.
NA KWA KUWA, Wizara ya Maji iliandaa waraka maalum wa kuiomba Serikali kutenga kiasi cha shilingi bilioni 653.85 Mpango Maalum 2011-2013 wa kuboresha huduma za majisafi na uondaji wa majitaka katika Jiji la Dar es salaam na kupitishwa na Baraza la Mawaziri mwezi Machi 2011 lakini utekelezaji wake unaelekea kucheleweshwa mpaka mwaka 2016.
NA KWA KUWA , katika mwaka wa fedha 2011/2012 na 2012/13 Serikali haikutenga kiwango kamili cha fedha kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioidhinishwa na Bunge na kwa kuzingatia mgawanyo wa Mpango Maalum wa Maji Safi na Maji Taka katika Jiji la Dar Es Salaam na kauli ya Serikali ya tarehe 7 Novemba 2012.
NA KWA KUWA, kwa mujibu wa ibara ya 62 (2)  na (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 , Bunge ndicho chombo kikuu chenye madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu.
NA KWA KUWA, kwa mujibu wa ibara ya 63(3) katika utekelezaji wa madaraka yake bunge laweza kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutunga sheria pale utekelezaji unapohitaji kuwapo sheria.
NA KWA KUWA, Malengo ya Kitaifa yalikuwa ni kuwapatia wakazi wa Mjini maji kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2010 na kwamba malengo hayo kwa Jiji la Dar es Salaam yamesogezwa mbele na kuwekwa malengo mapya ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kufikia asilimia 90 na uondoaji wa maji taka kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
KWA HIYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali ichukue hatua za haraka zaidi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam:
NA KWAMBA, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi  maalum wa matumuzi ya fedha matumizi ya bilioni 96.4 za mradi wa maji safi na mazingira vijijini katika Jiji la Dar es salaam na Halmashauri zingine na kuwezesha hatua za ziada kuchukuliwa.
NA KWAMBA, Kufuatia kauli iliyotolewa bungeni tarehe 7 Novemba 2012 kuhusu Mpango Maalum wa kutatua tatizo la maji katika Jiji la Dar es salaam uliopitishwa mwezi Machi 2011 Serikali izingatie makisio ya awali ya gharama za mpango huo na kuingiza mahitaji yaliyobaki kwenye Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2013/2014 na Bajeti ya mwaka 2013/2014.
NA KWAMBA, Mpango wa dharura wa kupunguza kero ya maji ulionza kutekelezwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DAWASA kuanzia Juni 2010 unaohusisha uchimbaji wa visima 29 uliopaswa kukamilika Oktoba 2011 uwekewe muda wa ukomo wa kukamilika kwa dharura katika maeneo ambayo miradi haijakamilika mpaka hivi sasa ikiwemo iliyozinduliwa Oktoba 2012 yenye kuhitaji miundombinu ya ziada kufikia wananchi zaidi.
NA KWAMBA, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi wa thamani ukilinganisha na ufanisi (Value for Money) wa Mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) kwa kurejea ukaguzi wa kiufundi (technical Audit) uliofanywa na kampuni ya Howard Humphreys.
NA KWAMBA, EWURA ifanye ukaguzi wa kiufanisi (performance audit) wa miradi ya visima vya maji takribani 200 ambavyo vilichimbwa na serikali na kukabidhiwa kwa DAWASCO, jumuiya za wananchi na taasisi mbalimbali lakini haitoi huduma inavyostahili kwa kadiri ya malengo ya awali.
NA KWAMBA, EWURA iharakishe kukamilisha mchakato ulioanza wa kutunga kanuni za udhibiti wa ubora na bei ya huduma ya maji kwa upande wa sekta binafsi katika Jiji la Dar es salaam.
NA KWAMBA, Kamati husika ya Bunge ijadili taarifa ya ukaguzi wa ufanisi kuhusu usimamizi wa usambazaji wa maji katika maeneo ya mijini (performance audit report on the management of water distribution in urban areas) ya Januari 2012 ili maoni na mapendekezo yazingatiwe wakati wa kujadili na kushauri kuhusu mapendekezo ya mpango wa taifa na bajeti ya nchi.
NA KWAMBA, Serikali iwasilishe bungeni haraka iwezekanavyo muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za majisafi na majitaka (Water Supply and Sanitation Miscellaneous Amendment Bill) ili kushughulikia upungufu uliojitokeza katika utekelezaji wa sheria zilizopo na kuweka mfumo thabiti wa usimamizi wa sekta ya maji nchini.”
Naomba kuwasilisha.
…………………
John John Mnyika(Mb)
Jimbo la Uchaguzi-Ubungo
04/02/2013

Wednesday, December 16, 2015

Kesi ya Kubenea, Makonda yaahirishwa

KESI iliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda dhidi ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea katika Mahakama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, imeahirishwa. Anaandiaka Yusuph Katimba … (endelea).

Akiahirisha kesi hiyo, hakimu anayesimamia kesi hiyo Thomas Simba amesema uchunguzi umekamilika na kwamba upande wa mashitaka na kwamba imepangwa kuanza kusikilizwa tarehe 29 Desemba mwaka huu.

Kwenye mahakama hiyo, Makonda amefungua madai matatu dhidi ya Kubenea ambayo ni lugha ya matusi, kuitwa mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa.

Kubenea ameweka mawakili sita katika kesi yake ambao ni Peter Kibatara, Rugemereza Nshara, Nyaronyo Kicheere, Frederick Kihwelo, Teremia Ntobesya pamoja na Omary Msemwa.

Hata hivyo, Kubenea yupo nje kwa dhamana, waliomdhamini ni Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest na Mbunge wa Kinondoni, Maulidi Mtulia ambapo kila mmoja aliweka dhamana ya Sh. 300,000.

Kesi hiyo imefunguliwa ikiwa ni siku moja baada ya Makonda kuagiza askari wa Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo kwa madai ya kushindwa kutii agizo lake kama Mkuu wa Wilaya.

Tukio la kukamatwa Kubenea lilitekelezwa jana jijini Dar es Salaam, baada ya viongozi hao kukutana katika mgogoro wa wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Tooku Tanzania.

Kwenye mgogoro huo, Kubenea alikuwa wa kwanza kufika ili kukutana na wafanyakazi hao na kuangalia namna ya kutatua mgogoro wa wafanyakzi na viongozi wa kiwanda hicho.

Katika mgomo huo Kubenea, alisikiliza kero za wafanyakazi ambao walikuwa wakivutana na menejimenti ya kiwanda hicho na baada ya makubaliano yaliyohusisha pande mbili, walikubali kuendelea na kazi.

Hata hivyo, wakati mbunge huyo pamoja na viongozi wa kiwanda hicho wakiwa katikati ya mazungumzo, Makonda aliwasili katika eneo hilo la kiwanda kilichopo ndani ya Mamkala ya Uwekezaji EPZ, Mabibo External.

Baada ya kufika, Makonda hakutaka kuhoji kuhusu kilichoendelea kwenye mgomo huo wa wafanyakazi na kutaka kuanza upya kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi licha ya Kubenea kuupatia ufumbuzi kwa mazungumzo yaliyohusisha pande zote.

Kutokana na hatua hiyo, Kubenea hakupinga hatua hiyo ingawa Makonda alipomaliza kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho, alifunga mkutano bila kuruhusu hoja yoyote kutoka kwa mbunge huyo.

Hali hiyo ilimfanya Kubenea kuhoji sababu ya kutopewa nafasi ya kuzungumza wakati ndiye alikuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio saa nne asubuhi na kulimaliza suala hilo.

Pamoja na hali hiyo Makonda, alipinga hoja ya Kubenea kuzungumza na wafanyakazi hao na kusema kwamba tayari amekwisha kufunga mkutano, hivyo haruhusiwi mtu mwingine kuzungumza kwa kuwa ndiye alikuwa mzungumzaji wa mwisho na tayari alikuwa amefunga.

Hatua hiyo ilizua mabishano makali baina ya Kubenea na Makonda kwa kila mmoja kusimamia kile anachokiamini.

Wakati hayo yakiendelea, Kubenea aliendelea kuwasihi wafanyakazi hao watulie, lakini Makonda akasisitiza hatozungumza hali iliyosababisha polisi waliokuwapo katika eneo hilo na baadhi ya viongozi wa kiwanda kuingilia kati kusuluhisha mzozo huo.

“Huwezi kufunga mkutano nisiongee na wafanyakazi ambao ni wapiga kura wangu, nimekuja hapa tangu asubuhi nimepambana hadi tukafikia hapa na niliwaahidi nikitoka kwenye kikao cha utawala nitawapa mrejesho (yaliyojiri).

“Inakuwaje wewe umekuja sasa hivi unazungumza na kufunga mkutano kwa ubabe?,” alihoji Kubenea huku Makonda akiendelea kusimamia msimamo wake kwamba tayari amefunga mkutano.

“…mimi hawa wamenipigia kura, wewe umepata kura ngapi, huwezi kunifanya lolote wewe,” alisema Kubenea. Baada ya mabishano hayo, Makonda aliamuru Kubenea akamatwe pamoja na kuamuru mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Star TV kunyang’anywa kamera yake.

Polisi walimtaka Kubenea kupanda kwenye gari lao la polisi (Defender) lakini kukatokea mabishano makali, kwani Kubenea alipinga kupanda gari lao umuazi waliokukubali na hatimaye askari wawili wenye silaha na mmoja ambaye hakuwa na silaha waliingia kwenye gari la mbunge huyo hadi Kituo cha Polisi cha Magomeni.


MwanaHalisiOnline

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA KUFANYA ZIARA YA KUWASHUKURU WAPIGA KURA

KUHUSU ZIARA YA MH. EDWARD LOWASSA KUSHUKURU WATANZANIA



Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Ndugu Edward Lowassa atazungumza na wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tanga, siku ya Alhamis, Desemba 17, 2015.

Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama na UKAWA kwa ujumla ambao watakwenda maeneo mbalimbali nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na agenda nzima ya MABADILIKO katika uchaguzi mkuu uliopita na wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo imara wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.

Itakumbukwa kuwa mbali ya Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na UKAWA na kuongeza nguvu kubwa ndani ya bunge hususan kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali yao mbadala huku wakiviamini vyama hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka.

Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia UKAWA.

Katika ziara hiyo ya Tanga, Ndugu Lowassa ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa UKAWA ukiwa ni mwanzo tu wa ziara kubwa itakayokwenda nchi maeneo mbalimbali nchi nzima.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 15, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Tuesday, December 15, 2015

CHADEMA yalaani kukamatwa kwa Mbunge wa Ubungo Kubenea

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi.

Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii.

Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo;

1. Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa yamefafanuliwa kisheria na kuwekewa mipaka yake ambayo Makonda amedhihirisha kuivuka katika nyakati tofauti sasa, Mkuu huyo wa wilaya hana mamlaka ya kisheria wala ya kisiasa kuhalalisha amri aliyoitoa ya kumkamata mbunge, tena aliyekuwa anatekeleza wajibu wake, tunamtaka DC Makonda amwachie Ndugu Kubenea mara moja huku tukitoa wito kwa mamlaka zilizomteua kumwangalia kwa makini kama bado anazo sifa za kuwa kiongozi wa ngazi hiyo.

2. Kwa kuwa amri hiyo si halali kwa sababu haina msingi wowote wa kisheria, tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kumuachia Ndugu Kubenea ili aendelee na uhuru wake huku akitekeleza wajibu wake wa kuwawakilisha wananchi wa Ubungo badala ya kumsumbua kwa mambo yasiyokuwa ya msingi.

3. Halikadhalika, Jeshi hilo liwarudishie waandishi wa habari vifaa vyao vya kazi vikiwa katika hali salama na bila athari yoyote ama ya vifaa vyenyewe au materials yaliyoko ndani yake.

4. Tunalitaka Jeshi la Polisi kutoa kauli ya kuwahakikishia usalama waandishi wa habari na vifaa vyao kila wanapotimiza wajibu wao kwenye matukio yanayomhusisha Makonda kwa sababu tayari ushahidi unaonesha anaweza kuwa tishio kwao binafsi na vitendea kazi vyao hususan pia wanapokuwepo polisi.

5. Kwa kitendo cha DC Makonda kuamuru kiongozi wa wananchi akamatwe bila kuwepo kosa lolote la kisheria, CHADEMA tutachukua hatua za kisheria dhidi ya DC huyo ili liwe fundisho kwake mwenyewe, wakuu wa wilaya wengine na utawala mzima wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli, ili watambue kuwa suala la kuongoza nchi kwa kuzingatia Haki, Katiba, Sheria na taratibu si suala la kupenda bali ni lazima kuzingatiwa kwa ajili ya amani na utulivu wa kweli.

Tutachukua hatua hizo huku tayari kukiwa na kumbukumbu za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBU) ambayo hivi karibuni ilimuonya DC Makonda na wakuu wa wilaya wengine na wakuu wa mikoa ambao wameanza tabia ya kuendesha nchi kwa amri ambazo hazina uhalali wowote zikiwa nje ya mamlaka yao ya kisheria kufanya hivyo.

Tuliamini angalizo hilo la THUB ambacho ni chombo huru cha serikali, lingeweza kuwa mwongozo sahihi kwa viongozi wa serikali na kwamba kosa la awali la Makonda kuwaweka mahabusu watumishi wa Wilaya ya Kinondoni walioko chini yake lingechukuliwa kama fundisho kwake, lakini bahati mbaya watawala wanaweka nta masikioni linapofika suala la haki za binadamu na uongozi bora.

Imetolewa leo Jumanne, Nov. 15, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Mbunge wa Ubungo mbaroni kwa amri ya Makonda

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amekamatwa na polisi eneo la viwanda (EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda cha nguo cha TZ TOOKU ambao walimpigia mbunge wao aende kutatua mgogoro huo.

Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.

Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.

Ilipofika saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.

Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.

Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Mbunge asihutubie kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo Kubenea alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.

Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea, kwa madai alimwita yeye Kibaka.

Katika tukio hilo, Mwandishi wa habari wa Star Tv aliyekuwa anarekodi tukio hilo alinyang’anywa kamera na Polisi aliyejulikana kwa jina moja tu la Denis.

Mwandishi wa habari hii alijaribu kumsaidia mwenzake ili arejeshewe kamera lakini Polisi wa kituo cha Magomeni walimtisha, na kumtaka kuondoka haraka huku wakiondoka na aliyenyang’anywa kamera.

Baada ya Kubenea kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya saa tano na kuandika maelezo chini ya mwanasheria wake, Fred Kihwelo aliachiwa saa 4 usiku kwa dhamana.


Wafuasi wa Ukawa wakiwa nje ya kituo cha Polisi Magomeni wakisubiri hatma ya mbunge wao.
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akipinga amri ya Makonda ya kukamatwa.
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha TZ ROOKU huku Makonda akiwa amevamia mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (mwenye fulana ya mistari) akimtaka Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea asiongee na wafanyakazi.

MwanaHalisiOnline

GODBLESS LEMA AREJEA BUNGENI

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amechaguliwa tena kwa mara ya pili kuongoza Jimbo la Arusha Mjini.

Akimtangaza Mbunge huyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini, Juma Idd alisema Lema ameshinda kwa kura 68,848 sawa na asilimia 65.7.

Alisema mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Philemon Mollel (Monban) amepata kura 35,607 sawa na asilimia 34 huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Zuberi (849),Navoi Mollel wa (ACT) 342 sawa na asilimia 0.3 huku chama cha NRA (43).

Alisema Idadi ya wapigakura ni 317,814 ,waliojitokeza ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 huku kura halali zikiwa ni 104,353 na zilizoharibika 1447.

Sunday, December 13, 2015

Fredrick Sumaye Atangaza Rasmi kuwa Mwanachama wa Chadema.........Akabidhiwa Kadi na Mbowe

Waziri mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye jana alitangaza rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) na akakabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe.

Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa CCM na kudai kuwa anaunga mkono mageuzi yanayofanywa na vyama vinavyounda katiba ya wananchi (UKAWA) bila kuweka wazi kuwa yuko kwenye chama kipi kati ya hivyo amesema sasa ameamua kujiunga na CHADEMA.


Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya Baraa, Sumaye alisema anataka kuungana na wanamageuzi wenzake katika kuendeleza harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado zinaendelea.


Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe alisema chadema na vyama washirika wa UKAWA bado viko imara na vimeendelea kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi azma yao ya kuleta ukombozi nchini iko pale pale.


Awali aliyekluwa mgombea uras wa CHADEMA akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa ameendelea kuwataka watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani bado kuna fursa yakufikiwa kwa malengo yao .

Chadema yamtumia salamu Muhongo

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.

Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.

Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.

“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.

“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.

Thursday, December 10, 2015

Muasisi wa Chadema ampa tano Rais Magufuli

WATANZANIA wa Kada mbalimbali wamempongeza Rais John Magufuli kwa kuokoa mamilioni ya shilingi ambayo yangetumika kwenye maazimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Tanzania, Anaandika Faki Sosi…(endelea).

Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia Muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, amesema kuwa uamuzi wa Rais Magufuli wa kufuta sherehe za uhuru utakuwa umeleta tija kubwa kwa taifa ambapo miaka mingi taifa limekuwa likichezea mabilioni ya shilingi bila faida kwa taifa.

Mtei alimesema kuwa sherehe hizo zilizokuwa zikifanyika kwa shamrashara ambazo zilikuwa zinagharimu fedha za walipa kodi kwa anasa za kula,kunywa na kulewa huku watanzania wakikosa huduma muhimu.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba ameshauri kuwa sherehe hizo zifanyeke mara moja kila baada ya miaka mitano ambapo zisihusishe matumizi mabaya ya fedha za wananchi kama zilivyokuwa za awamu iliyopita kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Naye spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa kitendo hicho kinapaswa kuungwa mkono kwa kila ambaye anayeitakia mema Tanzania. Sherehe hizo zimewaunganisha waatanzania wote kwa kufanya jambo moja ambapo sherehe hizo zilikuwa zikifanyika Dar es Salaam pekee kwa gharama kubwa lakini sasa zimekuwa za nchi nzima na zenye maslahi na taifa.

MwanaHalisiOnline

BULAYA AONGOZA WANANCHI KUFANYA USAFI BUNDA










Wednesday, December 9, 2015

MBUNGE WA MIKUMI MH. JOSEPH HAULE AKARABATI BARABARA JIMBONI MIKUMI







MBUNGE WA CHADEMA JIMBO LA UKONGA MH. MWITA WAITARA AFANYA UKARABATI WA BARABARA JIMBONI UKONGA

Mbunge wa Jimbo la Ukonga mh Mwita Waitara akiwa kwenye ziara ya kukagua ukarabati wa barabara za Jimbo lake la Ukonga. Mpaka sasa barabara za mitaa katika Kata tano ambazo ni Msongola, Kivule, Gongolamboto, Majohe na Zingiziwa zimeshafanyiwa marekebisho. Kazi itaendelea kwa kata zingine nane zilizobaki. Kazi Hii inafanyika kwa msaada wa Mbunge wa Ukonga.





Mnyika amkumbusha Magufuli ufisadi DART, bomba la Mchina

MBUNGE wa Kibamba, John Mnyika amemuomba Rais Dk.John Magufuli kuingilia kati mradi wa maji wa Ruvu Chini maarufu ‘Bomba la Mchina’ pamoja na wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) kuwa ni majipu sugu yanayotafuna fedha za walipa kodi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mnyika alisema siku 32 za Rais Magufuli kukaa Ikulu ametumbua vipele na si majipu kama inavyoelezwa.

Alisema tatizo la maji nchini ni kubwa ambako awali kulikuwa na nyumba inazuia mradi wa maji imebomolewa kwa sasa lakini hicho kilikuwa ni kipele na si jipu.

Katika mkutano huo, Mnyika alisema mradi huo wa mabomba ya Mchina na mradi huo wa mabasi ni majipu ambayo yanahitaji kutumbuliwa na Dk. Magufuli.

Mbunge huyo ambaye zaidi ya miaka mitano amekuwa akizungumzia tatizo la maji Dar es Salaam, alisema zaidi ya Sh bilioni 260 zimepotea katika mradi huo lakini hadi leo mabomba hayo ya Mchina hayatoi maji.

“Ni vema wahusika wachukuliwe hatua kwa vile wamesababisha maeneo yanayopata maji Ruvu Juu kama Kibamba, Msigani, Kwembe, Kimara , Tabata na kwingine kuendelea kuteseka na shida ya maji hadi leo hii,”alisema Mnyika.

Mbunge huyo alisema usambazaji wa maji ya Ruvu Juu ni ufisadi kwa kuwa kila kukicha wahusika wanasema pampu za maji zinaharibika na ripoti ya uchunguzi hadi leo imefichwa.

Usambazaji wa mabomba makubwa kutoka Mlandizi hadi Kimara ambao uligharimu Sh bilioni 89.8 hadi leo haujakamilika.

“Haya ni majipu matatu, maji ya Mchina, ripoti ya siri ya ukataji maji, ulazaji mabomba ya chini ni vema yakatumbuliwa mapema vinginevyo tutayapeleka bungeni kujadiliwa upya,”alisema Mnyika.

Kuhusu DART, Mnyika alisema mradi huo ulikuwa chini ya Ofisi ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Alisema mradi huo ambao umejaa udanganyifu ukiwamo kujengwa kwa ofisi zaidi ya 20 na kwamba mapato yatakusanywa kwa mfumo wa eletroniki, kauli hizo hazionekani kuzaa matunda.