NENO LA SHUKRANI
Na Elia F Michael.
Kwanza kabisa napenda
kutoa shukrani zangu kwa chama wilaya ya Kakonko na Chama Taifa kuniona
kama mtu sahihi kugombea nafasi hii ya Ubunge jimbo la Buyungu.
Chama kimefanya
jitihada kubwa sana chini ya Mkurugenzi wa chama John Mrema kuanzia mwanzo
mpaka Mwisho na zaidi ya yote nimshukuru Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe Freeman
Mbowe , Naibu Katibu Mkuu Bara Mhe John Mnyika pamoja na wabunge wote
waliofanikiwa kufika Kakonko na Kuzunguka jimbo la Buyungu kuniombea kura
hadi kufika kwa wazazi wangu na kuwashukuru kwa kuzaa chema. Hakika jitihada
zenu zimezaa matunda na wananchi wametupatia kura nyingi sana.
Pili,nitambue jitihada
za Chama rafiki ACT WAZALENDO ambacho kiliamua kuungana na CHADEMA ili
kuunganisha nguvu,nawashukuru uongozi wa ACT WAZALENDO Taifa pamoja na Mkoa wa
Kigoma na zaidi yote nimshukuru Kiongozi mkuu Kaka yangu Zitto Kabwe kwa kuamua
kuniunga mkono na hakika umoja ni nguvu.
Vyama vya upinzani
vikiunganisha mipango na kumsemea vizuri mgombea, CCM ni nyepesi sana na ndio
maana tumewasinda kwa kukubalika kwa wananchi na tukawashinda kwa kura wao
wakaamua kujitangaza chini ya ulinzi mkali wa FFU zaidi ya 400 usiku wa saa
kumi huku sisi tukiwa hatuna hata jiwe mkononi. Angalau tumeweza kuwavua nguo
hawa kijani kwamba hawakubariki na uwanja wa siasa safi hawauwezi tena. Hongera
CHADEMA hongera ACT WAZALENDO.
Tatu,naomba nitoe
shukrani zangu kwa TUNDU LISSU,CLA-TZ,COSA-TZ,Mh Pamela Maasay( mbunge wa Bunge
la Afrika Mashariki),Waheshimiwa madiwani wa CHADEMA TZ na wengine wote
waliokua nyuma ya harakati hizi. Hakika mmekua sehemu ya ushindi tulioupata!
Ningependa kutoa
ushauri wangu kwa makundi yafuwatayo;
1.WANANCHI na WAPIGA
KURA.
Kundi la wananchi na
wapiga kura ndilo linalopokea huduma kutoka kwa watu wanaokuwa wametangazwa
kama washindi wa uchaguzi mbalimbali. Hili kundi lina wajibu mkubwa wa
kukumbuka wanasiasa waliwambia nini wakati wa kampeni na hili kundi pia ndilo
lina mamlaka ya kushinikiza maamuzi lililofanya yaheshimiwe na tume kwa gharama
yoyote.
2. UPINZANI.
Sisi upinzani tuko
vizuri sana na aina ya siasa tunazofanya kwenye kampeni tuko sawa
kabisa,tunapata matokeo mazuri sana. Japo baadhi ya vyama vya upinzani
vinaratibiwa na ccm lakini misimamo na maelezo tunayotoa kwa wananchi ni rahisi
kututofautisha. Kudai tutangazwe kwa nguvu ya aina yoyote ile sio wajibu
wetu,wananchi wao wana mamlaka hiyo ya kutaka chaguo lao litangazwe. Hivyo basi
vyama vya siasa hususani upinzani halisi tunao wajibu mkubwa wa kuendelea
kuwaelimisha wananchi wajue umuhimu wa kulinda maamuzi yao kwa gharama yoyote
ile.
Njia pekee ya upinzani
kulinda maamuzi ya wananchi ni kufungua kesi mahakamani endapo tu vielelezo
vinajitosheleza.
3.TUME YA UCHAGUZI.
Tume ya uchaguzi inao
wajibu wa kutoa elimu kwa wapiga kura ila haina mamlaka katika kubadili maamuzi
ya wananchi. Hivyo acheni kabisa kuwachagulia wananchi juu ya nani ashinde.
Najua pia hii yote inatokana na namna ya tume inavyopatikana pengine mwafanya
hivyo kumfurahisha mteuzi wenu ila kumbukeni wanaoumia na maamuzi yenu ni
wananchi.
4.CCM.
CCM kama chama kingine
nyie pia mnao wajibu wa kuteua mgombea mwenye sifa na asiye na madoadoa,unajua
viwili vibovu vikishindana lazima kimoja kitapata fulsa ya kuongoza watu. Hivyo
basi kumbukeni maamuzi yenu katika hatua za uteuzi yanaweza kutugharimu hata
sisi ambao sio wanachama wenu pale ambapo mgombea wenu mlie msimamisha
akishinda. Kuweni makini kwenye uteuzi,msiteue mtu kulingana na urefu wa mfuko
wake bali uwezo wa bongo yake. Ni muhimu sana. Lakini pia acheni kutumia fulsa
ya kusimamia na kuongoza serikali kuingilia vyombo vya dola ili viwasaidie
kushinda..Hatua za awali mtafanikiwa japo baadae mtapata shida sana kwa
wananchi maana kiwango cha uvumilivu kitapungua.
5.POLISI NA VYOMBO
VINGINE VYA DOLA.
Msiiogope CCM
mkaisaidia kubaki madarakani,kwenu ninyi hata ccm ikitoka madarakani nyie
mtaendelea kutoa huduma yenu kwa wananchi maana nyie ni waajiliwa na watumishi
wa UMMA na utumishi wenu hata mkataba wa ajira hausemi kwamba utakoma pale
ambapo CCM itaondoka madarakani.
5.MH RAIS.
Kwanza kabisa
nikushukuru kwa kutamka tamka kwamba unamtanguliza Mungu kwa kila jambo,lakini
pia nikushukuru kwa kuanza kuonana na viongozi wa dini na makundi mengine
yanayo kushauri na kukuelekeza kwa ufasaha.
Naomba nikushauri
haya.
1. Kipimo cha uongozi
bora ni huduma njema kwa wananchi.
2. Ukisemacho wewe na
kukiamua kinaweza kuwa sahihi au kisiwe sahihi.
3. Sikiliza wananchi
wanasemaje juu yako.
4. Endelea kuwatendea
haki wananchi.
5. Kwakua wewe ni
mwenyekiti wa CCM na unataka CCM ibaki madarakani,njia pekee ya kuifanya CCM
ibaki madarakani japo haiwezekani ni;
1. Kutoa huduma bora
kwa wananchi.
2.Kuwatendea haki
wananchi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza.
3.Kuepuka kutumia
nguvu ya vyombo vya dola kupingana na maamuzi ya wananchi,hii njia kwa hatua za
mwanzoni inaweza kukufurahisha lakini inategemea kiwango cha uvumilivu wa
wananchi wenyewe. Ipo siku hawatavumilia nadhani.
4.Kuwapa elimu ya
uraia kuliko kuwanyima elimu wananchi. Ukiwapa elimu ya uraia wataelewa kama
ulikua sehemu ya waelimishaji lakini ukiwanyima watapewa na wengine NA baadala
yake watakuchukia wewe.
5. Acha chama chako
kisemwe kwa mabaya na mazuri pia.
Elia F Michael.
Mbunge wa Buyungu nje
ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
No comments:
Post a Comment