Tuesday, August 14, 2018

KAMATI KUU CHADEMA KUKUTANA

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA 

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana katika kikao chake maalum, siku ya Jumatano Agosti 15, mwaka huu, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali muhimu kuhusu chama na taifa kwa ujumla.

Kikao hicho kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, kitajikita katika masuala mawili; kupokea taarifa na kujadili kwa kina juu ya chaguzi za marudio za ubunge na udiwani na hali ya siasa nchini.

Wanachama wa CHADEMA na umma wa Watanzania kwa ujumla utatarifiwa kuhusu maazimio baada ya kikao hicho.

Imetolewa leo Jumanne, Agosti 14, 2018 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

No comments:

Post a Comment