Tuesday, August 2, 2016

Tundu Lissu:Rais Magufuli anapotosha kuhusu "Magwangala",ajifunze kwa Rais wa Bolivia

Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.
Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine. 

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally. Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu. 

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently. Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.
TUNDU LISSU 
Mwanasheria mkuu 
CHADEMA

No comments:

Post a Comment