Thursday, August 4, 2016

KAULI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA KUFUATIA KUKAMATWA KWA MHESHIMIWA TUNDU LISSU NA JESHI LA POLISI

Na Dr. Vecent Mashinji
Nimepokea kwa huzuni kubwa na kufedheheshwa sana na hali ya kukosekana kwa ustaarabu katika Taifa letu.

Jeshi letu la polisi limekuwa chombo cha ukamdamizaji na kuondoa staha katika jamii. Aibu hii ni kubwa mno kwa Watanzania kuweza kuivumilia. Ni fedheha kubwa kwa jeshi letu linaloongozwa na wanasheria waliobobea kufanya mambo nje ya misingi ya sheria.

Tabia ya kufanya mambo kwa kupuuza sheria, si kwamba tu yanadhalilisha taaluma ya sheria bali yanaondoa imani ya wananchi katika kuishi maisha ya kuheshimu utawala wa sheria (respect to rule of law).

Mh. Tundu Lissu ni Mnadhimu wa kambi ya Upinzani Bungeni, ni Wakili Msomi anayeheshimika duniani pote, ni Mbunge anayewakilisha jimbo na ni MTANZANIA.

Siamini kwamba polisi wangemtaka afike kituo chochote cha polisi angeweza kukaidi, lakini wameamua kumkamata na kumsafirisha kama mnyang'anyi. Aibu hii ni kubwa sana na sidhani kama itafutika machoni pa jamii yetu.

Nashukuru vijana wote waliojitoa kumsindikiza kwa kusafiri na polisi toka Singida kuja Dar. Huu ni ujumbe tosha kwa jeshi la polisi

Tanzania inamhitaji Mh. Lissu kuliko hata jeshi zima la polisi, kwa hiyo tunawataka polisi wamlinde na kumtendea kwa heshima kwani ni kiongozi mkubwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naamini kukamatwa kwake hakuhusiani na mihemko ya kisiasa iliyoletwa na huyo "populistic" leader ambaye hajui anataka kufanikisha nini.

Hatutanyamaza! Mnapoteza muda wenu tu!!!

Ni wakati wa kusonga mbele vitisho hivi vina mwisho, tusiogope leo wala kesho, ni wakati wa kujipanga na kuchukua hatua stahiki.

Mungu wetu you hai, soon tutaheshimiana tu

No comments:

Post a Comment