Sunday, August 28, 2016

TAARIFA KWA MAKAMANDA WOTE PAMOJA NA WAPENDA HAKI KUHUSU MWANACHADEMA MWENZETU MDUDE NYAGALI


1.Taarifa zilizothibitishwa na mimi mwenyewe ni kuwa rafiki yetu na kamanda wetu Mdude Chadema Nyagali Afisa wa CHADEMA Kanda ya Nyasa amefikishwa Kituo cha polisi Ostabay Kinondoni hapa Dar es salaam akisafirishwa kutoka mbeya alikokamatwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi. Kamanda wetu Hali yake sio nzuri na ni kweli miguu yake yote imevunjika na hawezi hata kusimama tu nategemea taratibu za kisheria zitachukuliwa haraka kwa msaada wa wanasheria wa CHADEMA Makao Makuu ili mwenzetu huyu apate matibabu haraka wakati taratibu za kimahakama zikiendelea.2.Pia makamanda wetu wawili Anneth Munuo na kamanda Macho wanashikiriwa toka jana na Polisi, wakati Annet alikamatwa akiwa na Tishirt zilizo na nembo ya CHADEMA pamoja na picha inaonyesha UKUTA, Macho haijajulikana makosa yake nao pia tutaendelea kushirikiana kikamilifu na Viongozi wetu wa CHADEMA pamoja na mawakili ili wapate msaada wa sheria kama ilivyo kwa Mdude na wengine.

3.Kwa wakati huu ambao makamanda wetu pamoja na comrades wetu wanaendelea kukamatwa na jeshi la police sehemu mbali mbali nchini tunaomba makamanda pamoja na wadau mbali mbali tuendelee kushirikiana kikamilifu hususani kutoa taarifa pamoja na kuwapa msaada wa karibu kama chakula nk, kwasababu siraha yetu kubwa siku zote ni umoja wetu kupitia nguvu ya umma "Peoples Power" .

NB:Tukiendelea kusubiri maelekezo official toka kwa viongozi wetu juu ya Kesi zote hizi tuendelee kudumisha utamaduni wetu wa kujitokeza na kujitoa kwa ajili ya wenzetu hasa pale wanapohitaji msaada.

Daniel Naftal Ngogo
Dar es salaam

No comments:

Post a Comment