Friday, July 15, 2016

YAH: KUTAARIFU WANANCHI WA DAR ES SALAAM YA KWAMBA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NI *BATILI* NA HALIWEZI KUTEKELEZEKA.

YAH: KUTAARIFU WANANCHI WA DAR ES SALAAM YA KWAMBA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NI *BATILI* NA HALIWEZI KUTEKELEZEKA.




Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki Meya Isaya Mwita Charles anapenda kutoa ufafanuzi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam Juu ya agizo ka Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliyeagiza kuwe na msako wa nyumba kwa nyumba kutambua wasio na kazi maalum.

Yafuatayo ni muhimu sana kutambuliwa na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kama *haki* yao ya msingi kabla ya utekelezwaji wa Amri hii ya Mkuu wa Mkoa.

Kwanza zoezi hili ni BATILI na haliwezi kutekelezeka kwenye Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam kwa sababu za msingi zifuatazo:

*i)* Sheria ya makosa ya Jinai Inaelezea utaratibu wa kukaguliwa nyumbani kama search warrant ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na ambayo Inaelezea wanatafuta nini.

*ii)* Sheria hiyo pia inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikishia ushahidi wa uongo.

*iii)* Kamwe popote duniani Kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.

*iv)* Kwa maagizo hayo inasemekana wananchi watawekwa ndani Kwa kukataa kutii agizo hilo, hakuna sheria Tanzania inayoruhusu Mwananchi kuwekwa ndani kwasababu za hovyo Kama hizo.

Naomba nimalizie Kwa kusema wananchi wote wa Jiji la Dar wawe na Amani kabisa na wajue haki zao na wajue kuzitetea, sisi viongozi wao tupo imara kusimamia haki zao na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Asanteni sana na Mungu awabariki.

Imetolewa na,
Isaya Mwita Charles,
Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment