Saturday, July 9, 2016

Lowassa awafunda Mameya wa UKAWA

Akizungumza katika mkutano wa mameya na wenyeviti wa Halmahauri watokanao na CHADEMA unaofanyika East Africa Hotel Arusha leo, Mh Lowassa amesema..

Tunataka halmashauri zetu ziwe za mfano Tanzania kwakuwa na Agenda ili tujue nikipi kipaumbele cha kuwatumikia wananchi, pia tuangalie Ni kitegauchumi kipi katika halmashauri husika kinaweza kuwapa wananchi wetu ajira.

Pili Tunataka kuimarisha Chama chetu kwa kushuka chini hadi ngazi ya Msingi ambapo ndipo walipo wanachama watu, (Grass Root.)

Pia nataka niwashauri Mameya wetu kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kutekeleza ahadi ya Mabadiliko na Maendeleo.

Katika kikao hicho maalumu cha mkakati, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vincent Mashinji na Katibu wa Kanda ya Kaskazini wampata fursa ya kutoa mafunzo mkakati na nasaa zao.
No comments:

Post a Comment