Saturday, July 16, 2016

Taarifa kwa umma na waandishi wa habari

Ndugu waandishi wa habari kwanza tunawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa kuwaeleza Watanzania adhima yetu ya kwenda Dodoma, katika kuhakikisha BAVICHA tunaisimamia kauli Jeshi la Polisi na ya Mhe. Raisi, na kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote hadi mwaka 2020 tukianza na mkutano haramu wa CCM hapo tarehe 23 July 2016.

Tunaendelea na msimamo wetu kuamini mkutano huo sio halali,kwakuwa ni Mkusanyiko wa Kisiasa ambao Mhe. Raisi na Jeshi la Polisi waliikataa vinginevyo watoke hadharani kukanusha Agizo na msimamo wao ulioathiri tayari vyama vya upinzani vikiwemo CHADEMA na ACT kwa kuzuiwa kukutana.

Sisi BAVICHA tunaheshimi kauli ya Kiongozi wetu mkuu wa chama,aliyotuomba tusiende Dodoma, kauli hii imeipa nafuu kubwa CCM kwakuwa hawakuwa na ubavu wa kutuzuia tusizuie mkutano wao.

Tulijipanga kila kona ya nchi hii,na hata jeshi la Polisi lisingeweza kutuzuia katika kutekeleza azima yetu,ya kutaka haki na usawa wa Kidemokrasia katika nchi hii ya Kidemokrasia.

Sasa basi,baada ya M/kiti kutuomba vijana wake tusiende Dodoma, sasa tunaamua kuja na plan B,ambapo hatutaenda Dodoma lakini hatutaruhusu mkutano wa CCM ufanyike mpaka pale Serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za Kidemokrasia kwa kila chama,kufanya siasa maana hivi tunavyoongea CCM wao wanafanya mikutano ya hadahara na wengine wanazuiwa.

Tunayo taarifa ya Baadhi ya mawaziri na wabunge wa CCM wao wanafanya mikutano ya hadhara katika majimbo mbali mbali,na picha za matukio hayo tunazo kwa ushahidi hivyo tukashitaki wapi?

Tunazo taarifa za Wakuu wa wilaya wakifanya mikutano ya hadhara na wanachi,hivi kati ya mkuu wa wilaya na vyama vya siasa nani mwenye mamlaka ya kufanya siasa!??

Tunaomba Watanzania waone na wapaze sauiti jinsi nchi yao inavyoongozwa Kidikteta,na kukosa usawa.Leo Dodoma kumepelekwa Polisi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Singida,Dar es salaam na Iringa wakiwa na kila aina ya Vifaa vya kivita.

Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Polisi wengi wasio na Idadi wakiwa na silaha nzito za kivita wanaenda kulinda mkutano wa Kisiasa,hii haijawahi kutokea.

Mtakumbuka Polisi wamewahi kuzuia mikutano mingi sana ya CHADEMA kwa kigezo kutokea machafuko na hali ya usalama ni ndogo,lakini hii imekuwa tofauti sana kwa upande wa Ccm wao usalama ni mdogo sana kupita maelezo katika mkutano wao wa tarehe 23 July,lakini vimepelekwa mpaka vifaru vya jeshi kuimarisha usalama.

Hii ni double standard ya hali ya juu,inayooneshwa na jeshi la Polisi kwa vyama vya siasa na huwa mara nyingine tunasema Polisi wanatumika na Ccm na huu ni ushahidi wa kwanza mkubwa kabisa.

Polisi wa nchi hii wako radhi wao wafe lakini Ccm isiguswe na wapo radhi hata kuua wapinzani ili Ccm iendelee kuwa madarakani,uko wapi usawa wa Kidemokrasia??? Uko wapi weledi wa kiutendaji wa jeshi letu la Polisi?.

UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINADAMU.

Tokea BAVICHA tumatangaza kwenda Dodoma, majeshi yaliyopelekwa Dodoma kuisaidia Ccm yamekuwa yakifanya unyanyasaji mkubwa kwa raia,wamekuwa wakikamata wananchi hivyo na kuwaweka ndani bila kuwafungulia kesi,na jina la mtu aliyekamatwa tokea siku ya jumatano mpaka Leo hajafunguliwa kesi,wala kufikishwa Mahakamani na hata mawakili wanapoenda kujua hatima yake wanafukuzwa na Polisi.

Polisi wanaingia katika Nyumba vya kulala wageni usiku,kufanya ukaguzi,kinadada wanadhalilika kwakuwa wengine wanakutwa uchi wa mnyama na Polisi wa kiume,huu ni unyanyasaji mkubwa unaofanywa na jeshi la polisi Dodoma.


Sasa tunawaomba vijana wetu wote nchi nzima watulie na wasubirie maamuzi ya kikao kikubwa cha kamati ya Utendaji,kitakachokaa siku ya jumatano ya tarehe 20.07.2016 Kukutana na M/kiti wetu tukiwa tayari na Plan B ya kuipigania Demokrasia ya Taifa letu.

Imetolewa July 16

M/kiti BAVICHA Taifa

No comments:

Post a Comment