Friday, July 1, 2016

Kauli ya Tundu Lissu baada ya kuachiwa kwa dhamana leo 30.06.2016



Tundu Lissu akiwa Mahakamani. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana, kesi yake yaahirishwa hadi Agosti 2.

Jopo la wanasheria 17 wakiongozwa na wakili wa mahakama kuu kijana zaidi John Mallya na Peter Kibatala, tayari wapo mahakamani kumtetea Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutoa kauli za kuudhi na kichochezi.


MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesomewa shitaka lake la kutoa maneno ya uchochezi kinyume cha kifungu namba 32 cha sheria ya magazeti.

Lissu anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mnamo June 28, 2016 kwa kumuita ‘Mkuu wa Nchi ni dikteta uchwara’.

Baada ya kusomewa shtaka hilo Lissu amekana shtaka na kuachiwa huru kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 02, 2016.

No comments:

Post a Comment