SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini na James ole Millya, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, leo wamesimamishwa vikao vya Bunge, anaandika Walfrom Mwalongo.
Sugu amesimamishwa kuhudhuria vikao 10 vya Bunge, Kubenea vikao vitano na Milya vikao vitano.
Adhabu hiyo imetolewa leo na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambapo Sugu ametolewa hukumu hiyo kwa madai ya kunyoosha juu kidole cha kati cha mkono tafsiri iliyojengeka kuwa ni matusi.
Kubenea amesimamishwa kwa madai ya kusema uongo bungeni kwa kulihusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na waziri wake, Dk. Hussein Mwinyi kwenye ugawaji wa ardhi kwa Kampuni ya Henan Guiji Industry.
Kubenea alifikishwa mbele ya Kamati ya Bunge, Maadili na Madaraka iliyo chini ya George Mkuchika hivi karibuni kujibu mashtaka hayo baada ya Dk Mwinyi kulalamika wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Dk. Mwinyi aliliambia Bunge wakati akihitimisha bajeti ya wizara hiyo kuwa yuko tayari kujiuzulu uwaziri iwapo Kubenea atathibitisha tuhuma hizo mbele ya Bunge.
Mara kadhaa Kubenea amekuwa akitoa ufafanuzi na namna vifungu vya kanuni vnavyokiukwa katika ‘kushughulikia’ wapinzani.
Hata hivyo, Dk Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge alimwagiza Kubenea kupeleka uthibitisho katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ukachunguzwe. Pamoja na Kubenea kutekeleza agizo hilo, ushahidi wake umetupiliwa mbali.
Dk. Mwinyi aliliambia Bunge wakati akihitimisha bajeti ya wizara hiyo kuwa yuko tayari kujiuzulu uwaziri iwapo Kubenea atathibitisha tuhuma hizo mbele ya Bunge.
Kufuatia ombi hilo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alimwagiza Kubenea kupeleka uthibitisho katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ukachunguzwe.
Vyama vya upinzani vinaeleza kusikitishwa na namna Bunge linavyoendeshwa hususan Dk. Tulia anapokuwa amekalia kiti cha spika.
Kumekuwepo na madai kuwa, Upo na mkakati wa Serikali ya Rais John Magufuli kuua vya vyama vya upinzani nchini kabla ya uchaguzi mkuu 2020.
Kumekuwepo na matukio kadhaa yanayoakisi dhamira hiyo ikiwa ni pamoja na viongozi wa Ukawa kukamatwa mara kwa mara.
Wabunge waliokwishaadhibiwa kwa kufungiwa kuingia bungeni hadi sasa ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Halima Mdee (Kawe), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), John Heche na Esther Bulaya (Bunda).
No comments:
Post a Comment