Sunday, February 14, 2016

TAARIFA KUTOKA CHADEMA WILAYA YA UBUNGO

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA‬ KWA VYOMBO VYA HABARI LEO 

Kwanza kabisa nashukuru kwa kufika kwenu kwenu.

Natoa pongezi zangu kwa wananchi na wilaya ya ubungo kwa majimbo haya mawili Kibamba pamoja na Ubungo kwa kuchagua ukawa kwa kura nyingi za udiwani pamoja na wabunge, Leo hii inapelekea Ccm kuwa chama cha upinzani kwenye majimbo haya kuanzia wenyeviti wa S/Mtaa/Udiwani mpaka wabunge na jiji kwa ujumla.

Kama chama na viongozi wa chama (W) ya Ubungo ikiwa na majimbo mawili.
Tumeamua kuchukua hatua hii kuzungumza nanyi ili watanzania na wanachama wetu kutambua kuwa kama chama tumeamua hatua na kutoa neno letu kwa watanzania juu ya sintofahamu iliyogubikwa katika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam.

Tukiwa kama chama tunaolinda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) tumeamua kujitokeza na kukemea na kupinga upotevu wa haki za msingi kabisa kwa watanzania wa DSM kukosa kuwa na kiongozi wao wa kisiasa katika Mkoa wa Dar as salaam, lakini kubwa ni kutoa rai kwa vyombo husika kuacha haki itendeke na kuitaka serikali na vyombo vyake kutoingilia mchakato huu wa kumpata Meya wa jiji la Dar as salaam.

‪Swala‬ la pili kubwa ambalo tumeona hatuwezi kulifumbia Macho kwa kuwa linagusa moja kwa moja mustakabali wa nchi yetu.

Ni swala la Zanzibar kuitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutopuuza msimamo wa chama cha wananchi CUF na msimamo wa wazanzibar juu ya mstakabali wa nchi yao ya Zanzibar hatuwezi kukaa na kuongelea mustakabali wa nchi pasipo kupata mwafaka wa Zanzibar,
Wito wetu ni kuitaka serikali kuacha Mara moja kuwanyima wanzibari haki yao ya katiba na kutaka aliye shinda apewe haki yake.

Kama chama tunaoamini katika demokrasia tunakitaka chama cha mapinduzi kuacha kutaka kupoteza amani ya Zanzibar.

Tukiwa kama chama ambacho kimsingi mbali ya kuwa ndio chama kikuu cha upinzani nchini lakini ndio chama kinachoongoza na kusimamia Halmashauri ya manispaa ya kinondoni , tunamtaka DC makonda kutoingilia shughuli za kiutendaji za baraza la madiwani kitendo kinachopelekea kuchonganisha baraza la madiwani na wananchi.

Tunamtaka DC makonda aache Mara moja kuwanyanyasa wananchi wa Manispaa ya Kinondononi haswa wafanyabiashara wadogo wadogo pembezoni mwa bara bara kuwa kama Manispaa imeishaandaa utaratibu wa mzuri wa kuwafanya wafanyabiashara wafanye biashara zao kwa ustaarabu na kulinda mazingira.

‪Anachokifanya‬ DC makonda tunasema no unyanyasaji na akiendelea tutamchukulia hatua za kisheria.

Siku 100 za Raisi Magufuli kama msemaji wa chama wilaya ya Ubungo nimeona siwezi acha kuzungumzia siku 100 za kushindwa kwa Raisi Magufuli maana alitoa ahadi lukuki wakati wa kampeni ikiwa kurudisha na kufufua viwanda vyote vya umma na vilivyo na ubia na serikali lakini pili ni kutoa Elimu bure kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha nne (4).

Kikubwa sio Elimu bure tunataka maboresho ya kimsingi katika sekta hivyo muhimu kw Taifa vilevile aliahidi kurejesha mashamba makubwa yaliokodiwa na watu wachache kwa manufaa yao.

Tunasema amefeli japo ni mapema kumjaji kwa siku chache lakini mwelekeo na mwenendo wa serikali yake unaonyesha wazi kuelekea kushindwa kutokana na kukurupuka kwa watendaji wake na kufanya kazi kwa misingi ya kazi husika.

Mwisho nampongeza Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacobo kwa kuanza vizuri utendaji wake kwa Manispaa yetu ya Kinondoni na kufanikiwa kupata wafadhili wa kujenga kiwanda cha takataka.

Nawashukuru wrote mliofika.

Wenu katibu wa uenezi Wilaya ya Ubungo
Perfect John Mwasiwelwa.

No comments:

Post a Comment