Friday, February 19, 2016

WAFANYABIASHARA WA MANISPAA YA KINONDONI WAPEWA SIKU SABA

Manispaa ya Halmashauri ya Kinondoni inavyanzo vya mapato 46, na mwaka wa bajeti 2015 – 2016, Manispaa ilikuwa imekisia kukusanya bilioni 46 kutoka vyanzo hivyo vya mapato, Pia Manispaa ina vyanzo vidogo vidogo vya mapato sita (6), 1. Ushuru wa huduma tukitegemea kukusanya bilioni 15, milioni 942 kutoka ushuru wa huduma. 2. Kodi ya Majengo (Property tax) ilikadiriwa kukusanywa bilioni 7 , milioni 646. 3. Leseni ya biashara na vileo, walipanga kukusanya bilioni 7, milioni 443. 4. Ushuru wa nyumba za kulala wageni walipanga kukusanya milioni 781. 5. Uwekezaji Manispaa ikiwa na sehemu zake ilizowekeza walipanga kukusanya kodi kiasi cha shilingi bilioni 1,milioni 320. 6. Ushuru wa mabango ambapo ilikadiriwa kukusanywa kiasi cha bilioni 2.5. Jumla ya mapato hayo katika Manispaa ya Kinondoni walipanga kukusanya bilioni 35, milioni 904 katika bajeti ya mwaka 2015 – 2016”.

Hayo ni maelezo ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob wakati akiongea na waandishi wa habari leo Jumanne 16/02/2016 katika ofisi za Meya zilizopo Magomeni Kinondoni jijini Dar es salaam.

Mpaka sasa Manispaa imeshakusanya zaidi ya bilioni 14, kwa makusanyo hayo yamempa Meya wa Kinondoni tumaini kwamba wataweza na watafikia malaengo katika ukusanyaji wa mapato, lakini kwa kipindi ambacho Meya ameingia ofisini katika ushuru wa mabango amegundua udanganyifu mkubwa unaofanywa na walipaji wa ushuru wa mabango.

Mstahiki Meya Mhe. Boniface Jacob amewaeleza waandishi wa habari udanganyifu huo waliougundua “Kwa awali utaona Manispaa tunaposema tulikuwa tunakusanya bilioni 2.5, ni wazi mwaka uliopita ulikuwa unakusanya chini ya hapo tukasema tuongeze kiasi kikubwa, lakini tumegundua ukusanyaji hata robo ulikuwa haufiki, hayo mabango mnayaona barabarani kulikuwa na udanganyifu wa vipimo, na idadi ya kila kampuni, tumereview mabango yote ya Manispaa ya Kinondoni, sasa idadi yao tunayo, na tumeyapima, upana mara urefu, tumegundua tulikuwa tunapoteza bilioni 11.5, hiyo ikiwa ni kwa mabango makubwa, lakini pia kuna makampuni madogo madogo, tulikuwa tunapoteza milioni 662” amesema Mstahiji Meya Mhe. Boniface Jacob.

Kwa maana hiyo walipaji wa ushuru wa mabango walikuwa wakiidanganya Halmashauri, akitolea mfano kampuni ya A1 Outdoor inadaiwa bilioni 1, milioni 394, kampuni hiyo na mabango yake yaliyopo Kinondoni ilikuwa ikilipa milioni 500 peke yake kwa hiyo kulikuwa na milioni 894 zilikuwa zikipotea kutoka kwenye kampuni hiyo pekee.

Manispaa imegundua mabango 74 ya A1 Outdoor yaliyopo Kinondoni ambayo wameyapima upya, ambapo mwanzo vipimo vilidanganya na idadi ya mabango ilikuwa chini, hiyo ni kampuni moja tu ya A1 Outdoor. Kampuni za mabango idadi yake ni 40, na kampuni kubwa tu zikilipa kodi kama inavyotakiwa wanategemea kupata bilioni 11.
Kampuni ya Continental Media ina idadi ya mabango 90 katika Manispaa ya Kinondoni Ikidaiwa milioni 825, na mabango yote yamepigwa picha yakieleza na sehemu yalipo.Kumekuwa na ukwepaji mkubwa wa ulipaji wa kodi katika Manispaa ya Kinondoni ambapo imekuwa ikiisababishia Manispaa kupoteza mapatoa mengi ambayo yangetumika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kinondoni kwa kupata huduma bora za kijamii n.k.

Kuna idadi ya makampuni makubwa 12 ya mabango yakiilipa Manispaa, itapatkana bilioni 11, milioni 951, Kampuni ndogo ndogo za mabango ambayo idadi yake ni 33, yakilipa kodi kikamilifu Manispaa itapata kiasi cha milioni 662.

Manispaa ya Kinondoni imeshakaa na kuamua kwamba inachukua hatua za kisheria kwa kampuni ambazo zimekwepa kulipa kodi, na Manispaa inategemea kupata pesa hizo ndani ya muda mfupi, Halmashauri itatoa muda kwa kampuni hizo kulipa madeni yao, wasipolipa kwa muda uliopangwa na Halmsahauri itajulikana nini kitafuata. Meneja wa Mabango Manispaa ya Kinondoni ameshaondolewa kutokana na udanganyifu na upotevu mkubwa wa mapato aliyoikosesha serikali kwa kipindi kirefu, na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika katika kuikosesha serikali mapato, na hatua hiyo ya kinidhamu zitatoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari Mhasibu wa Manispaa ya Kinondoni Bwana Max Luonwa ameeleza kwamba Manispaa imetoa siku 7 kwa wote waliokwepa kulipa kodi katika Manispaa ya Kinondoni hususani wamiliki wa mabango yaliyoko katika Manispaa ya Kinondoni wakitegemea kuingiza bilioni 11 baada ya kodi hiyo ya mabango kulipwa, na muda wa siku 7 ukiisha watawachukulia hatua za kisheria dhidi yao.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob, ametoa wito kwa wote wanaodaiwa kufika ofisini na kupata makaratasi ambayo yanaonyesha takwimu ya kiasi cha kodi wanayodaiwa wafike ofisini kwa Mhasibu wa Manispaa, ili wapatiwe na waweze kulipa kuanzia kesho Jumatano 17/02/2016, wasijidanganye kwa kutaka kufanya ujanja ujanja kwa watu kama hao hawatavumiliwa tena.

Kwa Mfanyabishara yeyote ambaye anaona kwamba labda vipimo vimekosewa ikiwemo na kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa anayo nafasi ya kwenda kupinga na kuhitaji marekebisho kama yapo na kuweza kueleweshana ili kila mtu afanye wajibu wake unaostahili.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni amesema hadhani kama serikali ya awamu ya tano itaweza kuwakingia kifua watu wa aina kama hii wanaokwepa kulipa kodi na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Ifatayo ni orodha ya makampuni yanayodaiwa ushuru katika manispaa ya kinondoni

ORODHA YA MABANGO KAMPUNI KUBWA NA KIASI WANACHODAIWA
A1 OUTDOOR 1,394,002,900/=Tshs
MASOKO AGENCY 200,158,200/=Tshs
CONTINENTAL MEDIA 8,259,910,400/=Tshs
ALLIANCE MEDIA 535,566,320/=Tshs
TAN AUTODOOR 309166050/=Tshs
BROCKCLINE MEDIA 452,898,240/=Tshs
SPARK OOH 1,616,588,700/=Tshs
GLOBAL SYSTEM 116,308,800/=Tshs
SYSCOPE MEDIA 17885736/=Tshs
LABEL PROMOTION 111,731,400/=Tshs
ASHTON MEDIA 218,975,740/=Tshs
PLATINUM MEDIA 172,984,340/=TshS



ORODHA YA MABANGO KAMPUNI NDOGO NA KIASI WANACHODAIWA

KUNDUCHI HOTEL 1,960,200/=Tshs

SKY OUTDOOR 56,628,000/=Tshs

SABODO 3,920,400/=Tshs

SLIMING CENTER 5,227,200/=Tshs

EAGLE OUTDOOR 52263200/=Tshs

PROMOTION SOLUTION 5,227,200/=Tshs

CITY FURNITURE 7,840,800/=Tshs

MOUNTDOOR Q 13,068,000/=Tshs

TRACTOR PROVIDER 1,960,200/=Tshs

BRAND ACTIVE 73,620,000/=Tshs

BANGO 3,920,400/=Tshs

FRONT MEDIA 13,612,500/=Tshs

RUNNERS 40,510,800/=Tshs

SOLAR POWERED 3920400/=Tshs

MELSTONE INTERNATIONAL 40,380,120/=Tshs

No comments:

Post a Comment