Saturday, September 19, 2015

CCM YASAMBALATIKA KOROGWE,VIONGOZI WAKE WATIMKIA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA

Viongozi wote wa CCM wa kata ya mkomazi na pamoja na wapiga kura 1,400 wa eneo hilo wilayani Korogwe wamejiunga na CHADEMA huku baadhi yao wakiamua kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwa tiketi ya chama hicho.

Wakizungumza katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika kijiji cha mikocheni kilichopo kata ya mkomazi wilayani Korogwe baadhi ya viongozi hao pamoja na wengine wa CCM katika kata sita waliokatwa majina yao katika zoezi la kura za maoni kwa tiketi ya CCM wamesema wameamua kujiunga na chadema pamoja na wapiga kura wao ili kuongeza nguvu kupata wawakilishi wa wananchi katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Korogwe

Kwa upande wake katibu wa CHADEMA jimbo la Korogwe Bwana.Salim Sempoli amemuomba mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Korogwe kuharakisha malalamiko ya wapiga katika baadhi ya vituo ambapo sehemu kubwa ya majina ya wapiga kura katika jimbo la Korogwe vijijini hayaonekani na hadi sasa hakuna utaratibu uliofanywa kusaidia tatizo hilo kwa sababu linaweza kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani wakati wa zoezi la kupiga kura.

Kufuatia hatua hiyo mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Emmanuel Kimea amewataka wananchi kuwachagua viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya taifa,ubunge na udiwani kwa sababu ndani9 ya chama kikoja changamoto zinazowakabili katika kata ya mkomazi ikiwemo ya migogoro ya ardhi haiwezi kumalizika kama hawatafanya mabadiliko.

No comments:

Post a Comment