Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu hali ya kampeni inayoendelea kwa baadhi ya vyama kushindwa kufanya kampeni za kiistarabu leo Ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Afisa Habari wa Chama hicho,Tumaini Makene.
Kauli hiyo ilitolewa katika kampeni za Urais mkoani kigoma na mmoja kati ya viongozi wa chama hicho ndugu ABDALA BULEMBO ambapo alisema kuwa hakuna njia inayoweza kuwaondoa ikulu na chama cha mapinduzi hakiwezi kuachia IKULU kwa njia yoyote kauli ambayo imeanza kuibua mijadala mbalimbali nchini Tanzania.
Akizungumza na wanahabari mchana wa leo mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA ndugu FREMAN MBOWE amesema kuwa kauli hiyo imewashtua sana wao kama vyama vya upinzani na kuanza kuwa na wasiwasi kama uchaguzi huo utakuwa na amani kwa kuwa chama chenye serikali kimeapa kufanya njia yoyote ili tu kisiachie ikulu.
Mh MBOWE amesema kuwa kauli hiyo inaweza kuchukuliwa kawaida lakini ni kauli nzito na yenye mafumbo makubwa ambayo yanaweza kusababisha vurugu kubwa na hadi sasa hakuna mtu yoyote wa chama hicho wala tume ya uchaguzi aliyejitokeza kutolea ufafanuzi kauli hiyo.
Amesema kuwa kama kauli hiyo ni kauli ya chama cha mapinduzi ni ukweli kuwa vyama vya upinzani havitaweza kuwa na imani na uchaguzi huo kwa kuwa tayari chama tawala kimesema hakiko tayari kuachia ikulu huku akienda mbali na kusema kuwa kwa kauli hizo hakuna haja ya kuendelea kuwa na uchaguzi ambao chama tawala kinangangania ikulu.
Mh MBOWE amesema sasa UKAWA unaitaka tume ya taifa ya uchaguzi kukitaka chama cha mapinduzi kutolea ufafanuzi kauli hiyo kwani kama ndio kauli yao watangaze kabisa kuwa hakuna uchaguzi kwa kuwa utakuwa ni upotevu wa rasilimali za taifa wakati tayari chama tawala hakiko tayari kukubali matokeo..
MGOGORO WA NCCR MAGEUZI.
Mh MBOWE amesema sasa UKAWA unaitaka tume ya taifa ya uchaguzi kukitaka chama cha mapinduzi kutolea ufafanuzi kauli hiyo kwani kama ndio kauli yao watangaze kabisa kuwa hakuna uchaguzi kwa kuwa utakuwa ni upotevu wa rasilimali za taifa wakati tayari chama tawala hakiko tayari kukubali matokeo..
MGOGORO WA NCCR MAGEUZI.
Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa chadema amesma kuwa sakata linaloendelea ndani ya chama cha NCCR MAGEUZI ni mwendelezo wa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo kuendelea kufika bei ya kutaka kuisaliti ukawa na hakuna lingine.
Hivi juzi viongozi kadhaa wa chama cha NCCR waliibuka na kudai kuwa chama chao kimekuwa kikiyumba kutokana na mwenyekiti wao kufanya kazi za chadema kuliko za chama huku wakidai kuwa wamekosa majimbo mengi ambayo walikuwa wanayatarajia ambapo Mh mbowe amesema kuwa hiyo sio hoja kwani lengo la UKAWA sio chama kuwa na majimbo mangapi bali ni kuhakikisha kuwa wanaibuka na majimbo mengi bila kujali vyama vyao.
Mh mbowe amesema kuwa swala la mgawanyo wa vyama lilienda sambamba na kuangalia uwezo wa chama husika katika jimbo na kusimamisha mtu ambaye anakubalika katika eneo husika ili kuweza kupata ushindi katika majimbo mengi na sio kutoa majimbo hata kwa watu ambao hawakubaliki katika majimbo hayo.
MPANGO WA KUMSHAMBULIA MBATIA
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameibua swala ambalo amesema kuwa wamelipata kuwa kuna mipango ya vijana kutoka chama cha mapinduzi kujifanya ni vijana wa CHADEMA na kumpiga Mbatia wakidai kuwa hawamtaki katika chama hicho jambo ambalo amesema ni mipango mfu kwani tayari chama hicho kimezipata.
Mh mbowe amesema kuwa mipango kama hiyo imekuwa ikipangwa na chama cha mapinduzi na na imekuwa wazi na wamekuwa wakiripoti sana kwenye vyombo vya dola lakini kumekuwa hakuna msaada wowote wanaoupata lakini wamejipanga kiulinzi kwa viongozi wao wote na wanahakikisha kuwa wanakua salama salimini.
MBOWE KUTOROKA NCHI
Akizungumza huku akicheka kwa mshangao mkubwa Mh MBOWE amesema kuwa kuna baadhi ya propaganda ambazo zimekuwa zikienezwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi na maadui wa UKAWA kuwa yeye ameikimbia nchi na haonekani katika kampeni za Mh LOWASA ambapo amesema kuwa ni utaratibu wa kupokezana kazi na sasa Ilikuwa zamu ya MH LISSU na baadae atapokea Mh WENJE ili kupeana nafasi za kufanya kazi za majimbo yao.
Mh mbowe amesema kuwa kuna baadhi ya jumbe za kutengeneza za EMAIL zikimuonyesha MBOWE akiwasiliana na Dk SLAA ambapo amesem ni uongo uliotukuka na hajawahi kufanya hivyo na hajatoka nje ya Tanzania kwenda popote kama wanavyosema huku akisema kuwa kuzushwa kwa mambo hayo ni kutokana na wapinzani wao kuishiwa sera na kuanza kuwadanganya watanzania.
HABARI ZAIDI......
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kila chama kifanye kampeni za kistaarabu ili kila mtu aende Ikulu pasipo kuvuruga amani.
Mbowe ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuelezea masuala ya kampeni zinazoendelea kwa vyama vyote vya siasa, pia amesema kuwa kuna kauli za viongozi wa baadhi ya vyama ambazo haziridhishi katika kupigakwao kampeni.
Mbowe amasema kauli ya watu hao ni ya kichochezi na haiwezi kuvumilika lakini chama husika hakikuweza kufuta kauli hiyo.
Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekaa kimya kwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyama kuwa hawawezi kuachia watu wakatawale Ikulu.
Amesema kumekuwa na changamoto katika umoja wa katiba ya wananchi lakini hadi sasa mgogoro wa majimbo hauzidi 10 ambapo ni hatua nzuri kwa umoja huo nia yao ni kwenda Ikulu na sio kuwagwana majimbo kama sadaka.
Mbowe amesema tatizo la viongozi waandamizi NCCR-MAGEUZI, inatokana na kutaka majimbo wasimame licha kutambua mtu anapewa kugombea kutokana na sifa alizonazo pamoja na uwezo wa mtu kushinda katika uchaguzi mkuu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Freeman Mbowe leo makao makuu ya ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo
No comments:
Post a Comment