Friday, August 21, 2015

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KWENYE OFISI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinachoungwa mkono na vyama vinne vinavyounda UKAWA kutoka Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea Urais katika uchaguzi utakao fanyika Oktoba 25, 2015. Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ndie aliyepokea fomu hizo na kutangaza rasmi kumteua Edward Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Haji Duni kuwania nafasi hizo kupitia vyama vyao.
Mwenyekiti wa Tume akisaini fomu hizo

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akizungumza.

Lowassa akitoka ofisi za NEC huku akisindikizwa na viongozi wa UKAWA
Lowassa akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu
Mheshimiwa Edward Lowassa akiongozana na Mgombea Mwenza Mh Juma Duni Hajji na mkewe mama Regina Lowassa wakati wa kurudisha fomu kwenye ofisi ya tume ya uchaguzi

Maalim Seif Shariff Hamad ni miongoni mwa viongozi wa UKAWA waliomsindikiza Ndugu Edward Lowassa wakati anarudisha fomu ya kugombea Urais
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akielekea kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi wakati Ndugu Edward Lowassa akirudisha Fomu ya Kugombea Urais kwenye ofisi za tume ya Taifa ya Uchaguzi

No comments:

Post a Comment