Saturday, August 22, 2015

WAZIRI MKUU MSTAAFU MHESHIMIWA FREDERICK SUMAYE AJIUNGA NA UKAWACHAMA Cha Mapinduzi, CCM, kimetikiswa tena leo Agosti 22, 2015, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mhe. Frederick Sumaye kujivua uanachana na kujiunga na NCCR-Mageuzi, moja ya chama kati ya vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Akitangaza uamuzi wake huo moja kwa moja "LIVE" kupitia runinga ya ITV katika jioni ya leo mbele ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jioni hii pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi.

Amesema kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama hichowaliokuwa wakizunguka nchi nzima walijielekeza zaidi kuishambulia serikali badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura.
"Sitoki CCM labda nina hasira na CCM, au sikuchaguliwa kwa vile sikuteuliwa, na wala sitoki CCM ili kudhoofisha Chama cha Mapinduzi, badala yake nakiimarisha."
Sumaye anakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa pili kuhama chama tawala, CCM, kama alivyofanya Edward Lowassa, ambaye naye alitangaza kujiunga CHADEMA mwezi Julai baada ya kutokuridhishwa na mchujo wa kupata mgombea Urais wa Tanzania 2015 na kufanikiwa kuteuliwa na chama chake kipya kuwakilisha vyama vinne katika kiti hicho.

Sumaye amesema kuwa, "kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli kweli" na kuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na upinzani ili kuharakisha mabadiliko hayo.

3 comments:

  1. Sawa kabisa. Mheshimiwa Rais JK anayemaliza muda wake ameshawekabwazi kabisa kuwa akiondoka madarakani hatajishughulisha na shughuli za siasa au chama ila panapohitajika ataweza kutoa mawazo na asingependa kufuatwa huko Bagamoyo alikoweka hekalu lake na mifugo atakuwa mfugaki bora na kuanzisha kitengo chabushauri ambacho naimani tayari kimeshaanza. ALILOONA NI KWAMBA CHAMA ALIYOONGOZA INAKUFA KIFO KIBAYA NA HATAKI KUJIHUSISHA. VYEMA KUSOMA NYAKATI...!

    ReplyDelete
  2. Aluta kontinua,Tanzania Revolution will be realised this year,viva ukawa.pipooooooz!

    ReplyDelete
  3. Wenyewe wanasema eti picha zime editiwa ,,na wao kwani wanashindwa?????wa edit

    ReplyDelete