Friday, August 21, 2015

Chadema sasa yazuiwa kuutumia Uwanja wa Taifa.

Wenyewe wasema hawajapata taarifa zozote zaidi ya kusikia kupitia vyombo vya habari.

Serikali imezuia matumizi ya uwanja wa Taifa kwa shughuli za mikutano ya kisiasa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, (pichani) alisema jana kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili uwanja huo utumike kwa shughuli za michezo pekee.

“Tumeamua kuufahamisha umma juu ya jambo hili kutokana na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitafanya mkutano wa uzinduzi wa kampeni keshokutwa katika uwanja huo,” alisema Mwambene.

Alisema walipata barua ya maombi kutoka Chadema Agosti 12 wakiomba uwanja huo kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zao na kwamba walishawapatia majibu kwamba hakuna chama cha siasa kitakachoruhusiwa kutumia uwanja huo kutokana na mihemuko na hamasa za kisiasa inayoweza kujitokeza miongoni wafausi wa vyama na kusababisha uharibifu.

Alisema walichukua uamuzi huo kwa busara ili kuufanya uwanja wa Taifa ubaki kwa ajili ya shughuli za michezo tu.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, alisema hawajapata taarifa zozote kutoka serikalini zaidi ya kusikia kupitia vyombo vya habari.

Makene aliongeza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kuficha aibu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuhofia wingi wa watu watakaojitokeza kwenye mkutano wa Ukawa kwa kuwa chama tawala kitazindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani eneo ambalo ni dogo ambalo hawawezi kupata watu wengi.

“Serikali inapaswa kutambua kuwa uchaguzi unaamua hatima ya nchi husika kwa kuzingatia demokrasia, hivyo wanachokifanya ni kuvinyima vyama vya upinzani haki ya msingi kwa ajili ya shughuli mhimu kwa kigezo cha kuvunja amani kitu ambacho si sahihi,” aliongeza.

Kwa mujibu wa Makene, hawatapoteza muda kubishana na Serikali bali watatafuta eneo lingine la kufanyia mkutano huo na watatoa taarifa kwa wananchi na wafuasi wote wa Ukawa nchini.

2 comments:

  1. So mkutano utakuwa wp na lini?

    ReplyDelete
  2. Mhe. Makene na kamati nzima ya maandalizi ya kampeni big up! Msibishane na serikali kwani yote yatafanyiwa kazi baada ya October 25. La msingi tafuteni penginepo na mikakati mongi ya kuwafundisha wapiga kura wetu kutoharibu kira siku ya kuingia kwa box la kura alama moja na sio mbili. Twende kazini MuMumgungu tubariki. Hao waliowekwa na chama ya ulaji wote ni walewale na wana madhambi wasijifanye wasafi. Hata Rais anaposema kununua madaraka Je wao hao watu 32 kwenye kamati kuzunguka mikoani wamewagawia fedha kiasi gani ni nyingi sana!! Haiwezekaniki na pili kitendo alichodaai Mh. Kiongozi wa NEC cha kutangaza matokeo baada ya siku tano huu ni uchakachuaji. Mawasiliano yapo wazi sana na kwa kuwa BVR imetumika hatuoni kigezo cha kutokutoa matokeo ya awali kuanzia siku inayofuata kupiga kura! Hesabu za kila kituo kwenda wilaya mkoa hadi makao.makuu shida iko wapi. Hii nintechnolojia mpya tuache kurudishana nyuma. Sivyo pia waziri anayehusika na mawasiliano naye hafanyi kazi yake ipasavyo. Kabilianeni na hayo. Kampeni njema.

    ReplyDelete