Saturday, August 1, 2015

CHADEMA: TAARIFA KWA WANANCHI NA WATANZANIA KUHUSU MGOMBEA URAIS KUREJESHA FOMU


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)


TAARIFA KWA WANANCHI NA WATANZANIA  KUHUSU MGOMBEA URAIS KUREJESHA FOMU


Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa baada ya hatua ya kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa ndani ya chama kugombea nafasi ya urais, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa kesho Agosti 1, 2015 atarejesha fomu yake kwa ajili ya taratibu zingine za ndani ya chama.

Shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 9.00 jioni, ambapo mgombea atakabidhi fomu yake Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chama, Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika hadhara ikayohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali.

Mheshimiwa Lowassa atarejesha fomu hiyo akiwa mgombea pekee baada ya kuwa ametimiza taratibu za kikatiba hususan kupata wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima.

Hatua hiyo ya kurejesha fomu itafuatiwa na taratibu zingine za kikatiba, ikiwa ni pamoja na vikao vya uteuzi ambavyo vitaketi kwa mujibu wa ratiba ambayo imeshapangwa na chama.

Imetolewa leo Julai 31, 2015.

1 comment: