Wednesday, August 12, 2015

CCM yakwama Kuihujumu Chadema-Morogoro.

Na Bryceson Mathias, Morogoro.
MBINU na Mizengwe ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kihonda Morogoro, kimekwama kuuhujumu Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai Mgombea wa Chadema, Elizeus Rwegasira, kwamba hana Mke, wakati ana Mke na watoto watatu Sekondari.

Hujuma hizo zilifanywa na Wapambe wa Watia Nia wa Udiwani wa CCM, waliofanikiwa kupenyeza Mamluki wa Chadema kwenye Kinyang’anyiro hicho, ili kumnyima nafasi Mgombea wa Chadema, Rwegasira, ambaye alionekana ni Tishio kwa CCM, Kielimu na kukubalika.

Katika kutengeneza Uongo na Uzushi huo, Wapambe hao walieneza kwamba, Mgombea wa Chadema, Rwegasira, ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kihonda Maghofani, wakati ana Watoto watatu, na wote wanasoma Sekondari.

Rwegasira alipoulizwa alikanusha, alidai hizo ni Siasa za Maji Taka tu hahangaiki nazo, isipokuwa anahangaika na kuwakomboa watanzania walio wengi, kutokana na Shida, Kero, Dhuluma, Manyanyaso, Mateso na Hujuma nyingi wanazofanyiwa Wananchi wa Morogoro na Tanzania nzima..

“Nina Mke na Watoto watatu, Agnes Elizeus Rwegasira, anayesoma Kidato cha Sita (Isimila High School), Antidius Elizeus Rwegasira, anayesoma Kidato cha Tatu (Educare Secondary School) na Erasto Elizeus Rwegasira, anayesoma Kidato cha Kwanza (Educare Secondary School)”.

Pamoja na Mizengwe iliyojiri, uchaguzi wa Kura ya Maoni Chadema ulifanikiwa kufanyika jana, chini ya usimamizi wa Katibu wa Wazazi wa Wilaya ya Morogoro, Omary Mvambo ambapo Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kihonda Maghorofani, Rwegasira, aliibuka Mshindi, kwa kupata Kura (28), Gabriel Temba (14), Frank Makomolo (11), na Wilbert Machimu (7).

Awali Gazeti hili lilikataa kupotoshwa, ili lipokee matokeo yasiyo sahihi yaliyotolewa na Mgombea mmoja aitwaye, Frank Makomolo badala ya Msimamizi, Katibu wa Baraza la Wazee la Chadema wilaya ya Morogoro, Omary Mvamba, na kungoja Matokeo ya Mvamba, ambapo alipotosha akidai, Rwegasira, aliibuka Mshindi kwa kupata Kura (34), Gabriel Temba (26), Frank Makomolo (16), na Wilbert Machimu (7).

Mwandishi alipomkanusha Mgombea kwa kusema Uongo, Makomolo, alikiri ni, Ni kweli, ila kumbuka zimepigwa kura za aina tatu (3), hizi ni za Wajumbe wa Mkutano Mkuu, na pia za Kamati Tendaji ya Kata, na zile za wenyewe kwa wenyewe, ambapo Mvamba kwa upande wake, aliwataka wagombe kuwa na Umoja.

No comments:

Post a Comment