Sunday, July 19, 2015

Tumrudishe Msigwa tena bungeni

Huu ni msemo ambao umetawala midomoni kwa WANAIRINGA wote wenye mapenzi mema na mkoa wetu wa IRINGA.

Huu ni msemo ambao unaleta hamasa kubwa ya kumtambulisha tena MH.MCHUNGAJI MSINGWA ambaye alikuwa mbunge wetu wa Iringa mjini!!

Ama hakika huyu ndiye Mbunge pekee ambaye wana Iringa tunaweza kujisifia,kwani alikuwa kipaumbele kuwatetea wana Iringa wote nje na ndani ya mbunge,tofauti na wabunge waliopita kama wakina Monika Ngezi Mbega,ambao hawakuweza kusimama na kuwatetea wana Iringa ndani na nje ya mbunge!!

Ni mbunge mwadilifu ambaye pia akisimama bungeni lazima bunge litikisike kwa kile atakaho kisema,wenyewe ni mashahidi kwani wote tunafahamu ni kwa namna gani hotuba zake bungeni zilikuwa zina tija gani juu ya maendeleo ya Iringa na nchi kwa ujumla!!

Ni moja ya wabunge machahali walioweza kuonyesha makali yao ndani na nje ya bunge kwa muda mfupi tuu!!

Hivyo wanaIringa wenzangu tusifanye makosa tumchague Msigwa tena kwa maendeleo ya mkoa wetu na nchi kwa ujumla!!

People's power!! MSIGWA TENA!!!

1 comment:

  1. copy and past! 'wakati wanainchi wa kata ya Nduli wakihitaji MILLION KUMI NA MBILI WAPATE MAJI,MCHUNGAJI MSIGWA AMEKODI JUKWAA LA EBONY NA MUSIC MILLION 10,BODABODA 300,KILA MOJA 40000,MABANGO NA VIPEPERUSHI NA TSHIRT VYENYE PICHA YAKE MILION 11 HARAFU ANARUDI KUTUOMBA TENA UBUNGE.EWE MWANA IRINGA FUMBUKA MKATAE MSIGWA NA CHADEMA YAKE" MWISHO WA KUNUKUU, NIMEPOKEA HIYO MSG KWA SIMU YANGU YA MKONONI ,UJUMBE HUO UNASAMBAZWA KWENYE SIMU NAWASILISHA.

    ReplyDelete