Sunday, July 19, 2015

MTIA Nia wa Udiwani CHADEMA, Kihonda Maghorofani Morogoro

MWANDISHI wa Mtandao huu katika Pilika pilika za kuwahoji Watia Nia wa Nafasi za Udiwani wa Vyama Mbalimbali nchini, alipata Bahati ya kupata Wasifu wa Mtia Nia wa Udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwenyekiti wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Elizeus Rwegasira,
Ifuatayo ni historia yake fupi ya Maisha yake, ambayo Mtandao huu ulimhoji, ambapo bila ajizi alisema, Mimi nilizaliwa tarehe 9/2/1975 katika kitongoji cha KATAALE, kijiji cha KIKUKWE, kata ya KANYIGO, wilaya ya MISSENYI (iliyomegwa toka wilaya wa BUKOBA VIJIJINI). Ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba wa Marehemu BERNAD TIILAGA na THERESIA BYEMELWA.

Nilianza "kindergaten" au chekechea iliyohusu mafundisho ya dini mwaka 1983 na mwaka 1984 nilijiunga na Shule ya Msingi OMURUSHENYE hadi nilipofanya mtihani wa kujiunga na SEMINARI NDOGO YA RUTABO iliyoko KAMACHUMU- MULEBA mwaka 1989 hadi 1990. Mwaka 1991 hadi 1993 nilisoma katika SEMINARI YA RUBYA iliyoko IHANGIRO-MULEBA na baadaye kujiunga na kuhitimu kidato cha NNE mwaka 1994 katika shule ya SEKONDARI KANYIGO maarufu KADEA. Mwaka 1995 hadi 1997 nichaguliwa na kuendelea na masomo ya HIGH SCHOOL katika shule ya sekondari SENGEREMA, MWANZA.

Baada ya masomo ya kidato cha sita niliajiliwa na kufanya kazi katika maeneo mbalimbali; 1. DIMON Tobacco Processors LTD nikiwa QUALITY CONTROL PERSONNEL (1998-2002) na 2. APPOPO RODENTS RESEARCH PROJECT nikiwa RODENT TRAINER (Mfundishaji wa panya buku kuweza kunusa mabomu na vimelea vya TB). Hii ilikuwa mwaka 2003.

Nilijiunga na chuo cha WAMISIONARI WA DAMU YA MWOKOZI kilichokuwa kikiitwa SALVATORIAN INSTITUTE OF PHILOSOPHY AND THEOLOGY nikichukua SHAHADA ya kwanza katika FALSAFA na kuwa mwanafunzi bora (2003-2006) katika matokeo ya mwisho ambayo yalithibitishwa na chuo cha URBANIANA cha Mjini ROME, ITALY ambacho SALVATORIAN ilikuwa "affiliated to". Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza nilifanya kazi ya Ualimu katika shule ya sekondari MALATI na ST.FRANCIS DE SALES SEMINARI zote zikiwa ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Hata hivyo, nilijiendeleza kwa kusoma shahada ya pili "UZAMILI KATIKA MANEJIMENTI NA UTAWALA WA BIASHARA" katika chuo kikuu cha MZUMBE (2009-2011) na kutunukiwa shahada hiyo nikiwa MWANAFUNZI BORA KATIKA UTAFITI.

Jambo hili lilinisukuma kuanzisha kampuni yangu iitwayo EPM CO.LTD inayojihusisha na UTAFITI NA USHAURI KATIKA BIASHARA. Hivyo, nimejiajiri na kujishughulisha na kazi hiyo.

Katika mswala ya uongozi; nimekuwa Katibu wa Bodi ya Elimu Parokia ya Maria Mtakatifu- Modeko (2005-2010); ni mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Kihonda Maghorofani na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihonda Maghorofani A kupitia CHADEMA.

Nje na uongozi katika CHADEMA, nilikuwa KATIBU wa NCCR-MAGEUZI wilaya ya Morogoro (1998-2003). Wilaya ya Morogoro wakati huo ilikuwa na majimbo 4 ambayo ni Morogoro kusini, kusini mashariki, kaskazini (Mvomero) na mjini (Manispaa).

Kwa sifa na upeo wangu, nimeguswa na kuona ninafaa kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya KIHONDA MAGHOROFANI ili kwa kushirikiana na wananchi katika kata hii, tuweze kuleta maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali zilizopo na ujuzi nilionao katika kuwawezesha wananchi kuwa Wajasiria mali.

No comments:

Post a Comment