Wednesday, July 8, 2015

TAARIFA YA POLE KWA WABUNGE MWANAMRISHO ABAMA NA JOSHUA NASSARI

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA YA POLE; WABUNGE MWANAMRISHO ABAMA NA JOSHUA NASSARI

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe ametuma salaam za pole na kuwatakia uponaji wa haraka majeruhi wa ajali mbili zilizotokea maeneo tofauti leo, moja ikihusisha helkopta nyingine ikitokana na ajali ya basi.

Katika salaam hizo, Mwenyekiti Mbowe ametoa pole kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassar, Mjumbe wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Wilaya Eva Kaaya, Katibu wa Mbunge Elisa Mungure pamoja na rubani William Silaa kutokana na ajali ya chopa iliyotokea eneo la Leguruki wakati mbunge na viongozi hao walipokuwa kwenye ziara jimboni humo.

“Wakati tukiwa kikaoni hapa tumepokea taarifa mbaya zinazohusu ajali mbili, ajali moja imewahusisha Mbunge Nassar pamoja na viongozi wengine wawili wa chama ambapo chopa waliyokuwa wakitumia kufanya ziara jimboni kwake ime-crash.

“Taarifa za awali zimetuhakikishia kuwa wamenusurika katika ajali hiyo na wamekimbizwa Hospitali ya Serian mjini Arusha ambako wanaendelea kupata matibabu kutokana na majeraha waliyopata...hali zao zimeelezwa kuwa si mbaya sana.

Tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali za majeruhi hao ambao wamepata ajali wakiwa kwenye mapambano.

“Mbunge wetu Mwanamrisho Abama naye amenusurika kwenye ajali iliyotokana na basi alilokuwa amepanda akiwahi kuja kwenye kikao hiki…basi hilo limepinduka wakati likitoka Dodoma kuja Dar es Salaam. Mheshimiwa Abama naye pia anaendelea vizuri.

Tuwatakie uponaji wa haraka wote waliopatawa na ajali hizo zote mbili na Mwenyezi Mungu awapatie wepesi katika hali hiyo,” amesema Mbowe.

Imetolewa leo Jumanne, 7 July 2015 na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

No comments:

Post a Comment