Wednesday, July 8, 2015

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MHESHIMIWA JOSHUA NASSARI APATA AJALI YA HELIKOPTA LEO

Mbunge wa Arumeru Mashariki,mkoani Arusha Joshua Nassari amepata ajali ya helkopta aliyokua anaitumia kufanya ziara katika jimbo lake.
Habari za awali tulizozipata ni kwamba mbunge huyo wa Chadema Joshua Nassari amenusurika kufa baada ya Helkopta aliyokuwa anaitumia kuanguka baada ya kunasa kwenye mti baada ya kupotea kwenye mawingu.
Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo kwa Tiketi ya Chadema, na rubani wake walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanila la Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha.No comments:

Post a Comment