Sunday, July 19, 2015

KUNDI LA 4UMOVEMENT DAR LATANGAZA KUUUNGA MKONO UKAWA

TAARIFA RASMI - 4U MOVEMENT TANZANIA

4u movement Tanzania inajipambanua katika mabadiliko chanya kwa nchi yetu, tumeongoza Kuyasaka mabadiliko Kupitia balozi wetu wa mabadiliko Mh Edward Lowassa ndani ya CCM. Mchakato wa Kidemokrasia wa kudai mabadiliko ndani ya CCM umefungwa bila balozi wetu kuwa mpeperusha bendera hio na si kwa kushindwa , bali haki haikutendeka kwake na kwa wagombea wengine kwa kufinyangwa kanuni za chama katika Mchakato.


Tuliahidi kuto rudi nyuma na kamwe hatuwezi saliti nchi yetu, Mwl Julius Kambarage Nyerere muasisi wa Chama Cha Mapinduzi na Baba wa Taifa alituasa, tukiyakosa mabadiliko ndani ya CCM tuwe radhi kuyatafuta nje ya CCM.

4u movement Kama vuguvugu la mabadiliko hatusimami kuyadai mabadiliko ndani ya nchi yetu.

Tunaanza rasmi safari ya kudai mabadiliko nje CCM kwani si dhambi na ni haki yetu ya kikatiba. Tunawaomba wana 4umvt kwenda kushiriki kikamilifu uchaguzi wa 2015 kwa kuchukua fomu mbali mbali za uchaguzi, Kujiandikisha kWa wingi na kuwa hamasisha wenzetu wajiandikishe ili kwenda kutafuta mabadiliko YA kweli na kuingoa CCM madarakani.

Kwa picha na Taarifa za kikao pitia hapa.
Ahsanteni

Mr Hemed Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)

Kiongozi wa Kundi Vijana wa 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Hemed Ali akizungumza na waandishi wa habari jjini Dar es Salaam leo Julai 18, 2015 kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWA


Vijana wa Kundi la 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, washangilia baada kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWA.


1 comment:

  1. Please chadema you must be careful, hao ni wasaliti siku moja pia watakuja kuwasaliti.lengo lao ni madaraka na si kuwatumikia wanainch.be careful with this team usaliti, wenzenu wanawakataa ninyi mnawapokea doa hilo.nawasilisha

    ReplyDelete