Tuesday, July 7, 2015

MTIA NIA UBUNGE JIMBO LA MBARALI LIBERATUS MWANG'OMBE AWASILI MWALIMU NYERERE INTERNATIONA AIRPORT TAYARI KWA KUANZA SAFARI YAKE YA KUWATUMIKIA WANA MBARALI

Akiwa anatokea masomoni Marekani, mtia nia Liberatus Mwangombe kwenye jimbo la Mbarali kwa tiketi ya CHADEMA amewasili mchana huu kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam

Mwang'ombe anatarajia kuwa na mikutano na baadhi ya viongozi wa kitaifa Makao Makuu ya CHADEMA hapo kesho kabla ya kuelekea jimboni, Mbarali, siku mbili zijazo.

Akiongea na muwakilishi wa studio za SUN SHINE kutoka Chimala punde tu alipo shuka Airport ya Mwalimu Nyerere, Mwang'ombe amesema "Hakuna muda wa kupoteza na kuanzia sasa ni mwendo wa kuijenga Mbarali Mpya Yenye Mafanikio". Zaidi ameeleza, atakuwa tayari kufanya kazi na watu wenye itikadi tofauti na mlengo tofauti ilimradi maslai ya watu wa Mbarali yanawekwa mbele.

Studi za SUN SHINE kutoka Chimala, Mbarali, zitakuwa zikikuletea habari za mgombea huyu mweledi, mwenye msimamo na asiye yumbishwa mara kwa maraNo comments:

Post a Comment