Saturday, June 6, 2015

Mke wa Kafulila, Bi. Jessica Kishoa akamatwa na Polisi

Mke wa Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa David Kafulila ambaye ni Kada wa Chadema Jesca Kishoa amekamatwa na Polisi na kuwekwa selo leo mchana mida ya saa 8 wilayani Iramba Magharibi Jimbo la Mh. Mwigulu Nchemba akiwa katika harakati za kufanya mkutano wa CHADEMA ambao ulipangwa kufanyika Kiomboi stendi ya mabasi.
Hii ni mara ya tatu ametangaza kufanya mkutano hapa Kiomboi lakini polisi wameizuia mikutano yote wakidai kuna viashiria vya kuvunja amani.
Mkutano wa kwanza ulizuiliwa mnamo mwezi wa Tatu mwishoni, mkutano wa pili ulizuiliwa mwezi wa nne katikati tena kwa mabomu ya machozi, sasa leo hii wameamua kumkamata kabisa na mabomu ya machozi yametupwa vya kutosha, watoto wametapika sana na maduka yamefungwa, pia polisi waliamua kuzuia magari yote yasitoke wala kuingia eneo hilo la stendi.
Mpaka sasa Bi. Jessica hajaachiwa na wananchi wametapakaa mtaani wakisubiri mpaka aachiliwe.

Wadadisi wa mambo wanasema kuwa kuzuiwa kwa mkutano huo ni shinikizo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni pia ni Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Mwigulu Nchemba.

No comments:

Post a Comment