Saturday, June 6, 2015

CHADEMA yatikisa Arusha, Mb. Nassari azitambulisha Ambulance 2 kwa jimbo lake

Umati wa wananchi waliouthuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akitambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake

Profesor Jay akihamsisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIO MATUMAINI"

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amewataka watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa Miaka Mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura" Pia ametambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ambaye pia ndiye aliyeteuliwa na Chadema Kanda Ya Kaskazini kuwa kiongozi wa kampeni za Hamasa ya kujiandikisha kanda ya kaskazini amewaambia wananchi wa Arusha kuwa safari ndio imeanza sasa kuelekea majimbo yote 33 ya kanda ya kaskazini kuhakikisha Watanzania wanajiandikisha kwa wingi ili October tufanye maamuzi sahihi

Mbunge wa Rombo Joseph Selasini" WATANZANIA WENZANGU HUU NDIO MUDA MUAFAKA WA KILA MMOJA WETU KUJIANDIKISHA ILI IKIFIKA OCTOBER TUWE TUNAFANYA MAAMUZI YA UHAKIKA NA SIO SAFARI YA MATUMAINI"

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mh Pauline Gekul awataka Watanzania kujiandikisha na kuhamasishana kwa wingi wetu kwa kutumia simu mitandao ya kijamii vikao vya kijamii ili ifikapo October tuiondoe CCM madarakani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Cecilia Daniel Paresso amewataka Vijana na Akina Mama kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili ikifika October waweze kufanta maamuzi ya UHAKIKA na sio ya maamuzi ya MATUMAINI.

No comments:

Post a Comment