Wednesday, June 3, 2015

MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROAD SLAA MKOANI RUKWA

Pichani chini: Wanachama, wafuasi, mashabiki na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa wakimsindikiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibroad Slaa baada ya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji huo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ndua. Barabara za mji huo zililazimika kufungwa kwa muda na shughuli kusimama wakati wananchi wakiwa katika shamrashamra ya kumsnikiza kiongozi huyo ambaye yuko katika ziara ya kikazi kukagua uandikishaji wapiga kura kwa BVR, kuhamasisha wananchi wajiandikishe kwa wingi huku pia akikagua maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi mkuu.



No comments:

Post a Comment