Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dr. Wilibrod Slaa, akiwasalimia wanachama, wapenzi, wafuasi na mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuwasili katika ofisi za wilaya za chama hicho mjini Mpanda, mkoani Katavi juzi mchana akiwa katika mwendelezo wa ziara yake maeneo mbalimbali ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi ambako mbali ya kukagua zoezi la uandikishaji wa wapiga kura amekuwa akihamasisha wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu huku pia akikagua maandalizi ya chama kinavyojipanga kuelekea uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibroad Slaa akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Mpanda, mkoani Katavi uliofanyika katika Uwanja wa Kashaulili baada ya kuwasili mkoani humo akitokea Mkoa wa Rukwa na Mbeya, ambako amepita katika maeneo mbalimbali akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa BVR, akitumia mikutano ya hadhara kuhamasisha wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, huku pia akikagua maandalizi ya chama kinavyojipanga kueleka mwezi Oktoba.
No comments:
Post a Comment