Thursday, June 4, 2015

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa aendelea na ziara mkoani Rukwa

Katibu mkuu wa CHADEMA DR. Wilbroad Slaa akiagana na wananchi wa Namanyere, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa baada ya mkutano wa hadhara wa kuhamasisha wananchi wenye sifa kujiandikisha kwa wingi kwenye Daftari la Wapiga Kura kwa mfumo wa BVR, uliofanyika katika Uwanja wa Ngao. Kiongozi huyo amekuwa kwenye ziara ya maeneo mbalimbali ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi ambako amekagua zoezi la BVR pamoja na maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Oktoba.

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa Akiwahutubia wananchi wa Namanyere katika Uwanja wa Ngao, juzi akiwa ametokea Mpanda.


No comments:

Post a Comment