Tuesday, June 9, 2015

KATIBU MKUU DK. WILLIBROD SLAA ZIARANI BARANI ULAYA


TARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



KATIBU MKUU DK. WILLIBROD SLAA ZIARANI BARANI ULAYA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini Jumamosi Juni 06, 2015 kuelekea Bara la Ulaya ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nane.

Akiwa ziarani Dk Slaa anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambapo pia atakutana na jopo la wataalamu wa masula ya uchumi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika kupata mifumo sahihi na kujenga taasisi za kusaidia uwajibikaji na kusukuma maendeleo ya watu katika nchi za Afrika hususan zile zenye rasilimali nyingi kama Tanzania ili kuziepusha na kile ambacho kimezikumba nchi nyingi duniani yaani 'laana ya raslimali' (resource curse).

Aidha, akiwa na viongozi wa nchi za Ulaya, Dk Slaa atajadiliana nao kuhusu hali ya Demokrasia, utawala bora na hali ya haki za binadamu nchini hasa kwa kipindi hiki ambapo Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Katika ziara hiyo, viongozi hao wa Ulaya watapata fursa ya kujadiliana na Dk. Slaa hali ya siasa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dk. Slaa ameambatana na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene.



Itakumbukwa kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa amekwensa ziarani barani Ulaya akiwa ametoka kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kagera, Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa mfumo wa BVR huku pia akiwahamasisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuhakikisha wamejiandikisha. Alitumia pia ziara hiyo kukagua maandalizi ya chama katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Dk. Slaa atarejea nchini tarehe 15.06.2015.

Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa - Chadema

No comments:

Post a Comment