Wednesday, May 6, 2015

Oparesheni Ondoa CCM na Makopo yake, yavuna 200.

Na Bryceson Mathias, Dodoma Vijijini.
OPARESHENI ‘Ondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Makopo yake’, iliyoandaliwa na Chama cha Demolrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Dodoma Mjini, imeanza kwa kumevuna Wanachama 2000.

Akizungumza na Mwandishi hivi karibuni juu ya Oparesheni hiyo, Katibu Mwenezi wa Chadema wilayani humo, Juma Mtaalam, amesema Mpango kazi wa Chama chake ulioanza, April 19, mwaka huu, tayari umewapa faida ya Wanachama 200, kujiunga na Chadema.

“Oparesheni hiyo inakwenda Sambamba na Zoezi la kufanya Mambo Manne (4) ukiwemo, Uchaguzi wa Viongozi, Mikutano ya Hadhara, Mafunzo ya Kamati Tendaji za Kata 41, Kuorodhesha Wanachama na Namba za Simu za waliojiunga na Chadema” alisema Mtalaam,

Katibu Mwenezi (Mtalaam), alipoulizwa maana ya ‘Oparesheni Ondoa CCM na Makopo yake’ Mtalaam alisema, “Ni Kuing’oa CCM na Kuchagua Chadema, na Makopo yake, ni Kung’oa Viongozi wababaishaji wa CCM, ikiwemo Rushwa, Ufisadi na U-Escrow yao”.alijigamba

Mtalaam alibainisha, tayari Uongozi wa Chadema Wilaya, Mkoa na Taifa, tayari wameruhusu Watangaza Nia wa Nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais, kujitokeza kwa kufuata taratibu za mapema, kwa sababu Chama hicho hakipo tayari, kuokota makopo yatakayotoswa kwenye Kura za Maoni ya CCM.

Aidha alimtaja Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila, kuwa ndiye Kiongozi mojawapo aliyetia Nia ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, ambapo atashirikiana na Watia Nia wa nafasi za Udiwani, ambao kwa sasa wako kwenye Uwanja wa Siasa wakijinadi kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment