Thursday, April 23, 2015

Mchungaji TAG; Nimepata Wito kuitumikia Chadema.

Na Bryceson Mathias, Morogoro vijijini
MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Morogoro, James Samson Mabula (Power Mabula) amesema, baada ya kuitwa na Mungu kwenye Uchungaji, ndani mwake Mungu amempa Wito wa kukitumikia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza katika mikutano ya kujinadi baada ya kutia nia ya kutaka kugombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa Tiketi ya (Chadema), Mabula ambaye aliwahi kuteuliwa na Askofu Mkuu wa TAG, Barnabas Mtokambali, kuwa Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la Bethel Revival alisema,

“Nilipata Wito wa kukitumikia Chadema katika Siasa na kujiunga nacho mapema kabisa, kwa sababu ndicho Chama pekee nilichoona kina nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania, na sasa ukiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

“Nikiwa Chadema, baada ya kuona baadhi ya Wabunge wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ambao hawamo katika Umoja wa UKAWA si waadilifu na hawana Mzigo wa kuwatumikia wananchi; Nimepata Wito wa kutia Nia ya kugombea Ubunge Morogoro, Chadema kinifikirie”.alisema Mabula.

Mabula alisema, iwapo Chadema kitampa ridhaa kusimama katika kinyang;anyiro hicho akashinda Ubunge; Moja ya mambo kati ya Matano Makuu atakayofanya akishirikiana na Chama chake, ‘Ni kuhakikisha anarudisha kwa Wananchi Viwanda 11 vilivyouawa na Serikali ya CCM.

Aidha amesema, Hatua hiyo itakwenda Sambamba na kuhakikisha Huduma ya Maji inavifikia Vijiji vyote 29 vya Manispa ya Morogoro, huku akihakikisha anaungana na Wabunge wenzake watakaoshinda, kuilazimisha Serikali kulinda rasilimali za Wananchi zinazoporwa kila kukicha.

Wanachama 11 wa Chadema, wametanagaza nia ya kutaka kuwania Jimbo la Morogoro Mjini, ambalo kwa sasa linaloongozwa na, Abdul-Aziz Mohamed Abood, (CCM), ambapo kati yao yumo Mwanasheria Bathromeo Tarimo tayari wanapiga Jalamba katika Kata 29 kujinadi kwa wanachama, ili wakubaliwe Chama.

No comments:

Post a Comment