Saturday, March 14, 2015

Katibu Mkuu Dk. Slaa ziarani kesho wilayani Kahama, Shinyanga

Katibu Mkuu wa Chama, Dk. Willibroad Slaa anatarajiwa kufanya ziara katika Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga kwa ajili ya shughuli za kijamii ambapo pia atapata fursa ya kukutana na wananchi kwa ajili ya masuala ya ujenzi wa chama.

Katika ziara hiyo itakayofanyika Jumamosi ya Machi 14, mwaka huu, Katibu Mkuu atafika katika Kijiji cha Mwakata, wilayani Kahama, kuwajulia hali na kuwapatia pole wananchi waliopatwa na janga la mvua kubwa ya mawe hivi karibuni, hali iliyosababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali na makazi.

Katibu Mkuu pia atapata fursa ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika eneo la Isaka, Jimbo la Msalala, wilayani Kahama.

No comments:

Post a Comment