Monday, March 16, 2015

CHADEMA Yasambaratisha CCM uchaguzi serikali za mitaa Mbezi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimeisambaratisha vibaya Chama cha Mapinduzi -CCM katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika leo katika mtaa wa Kingazi Kwembe Mbezi DSM

Katika matokeo yaliyotangazwa  kituoni Chadema kimepata ushindi wa kimbunga wa kura 500 huku CCM wakiambulia kura 180

Ushindi huu ni aibu kubwa kwa CCM iliyopiga kampeni kufa na kupona kwa kutumia wabunge na baadhi ya mawaziri.

Ni shangwe kuu zimetanda kila mahali huku mamia ya wananchi wakipeperusha bendera za Chadema.

1 comment: