Tuesday, February 10, 2015

Shekhe; Niliupata Udiwani wa Chadema kwa Mbinde.

Na Bryceson Mathias, Bukene.
Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) smbsye ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Nzega na Shekhe wa Wilaya ya Bukene, Shekhe, Omari Omari, amesema pamoja na Njama za Chama Tawala (CCM) kumfanyia Mizengwe, aliupata Udiwani wa Chadema kwa Mbinde.

Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima na mwandihi wa Habari hizi, Omari ambaye pia ni Kiongozi waBaraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) alisema, kuupata Uongozi ndani ya Chama cha Upinzani unaposhindana na CCM ni Mbinde, maana wana Mchezo Mchafu.

“Uelewa wa Wananchi wa Bukene juu ya Demokrasia ya Vyama Vingi, Mvuto wa Chadema na Sera zake, na kukubalika kwangu japo nilishindana na Mtu Tajiri mwenye Magari, nilishinda kwa ushindi Mnono”.alisema Omari.

Kuhusu Uchaguzi wa Madiwani, Ubunge na Urais kwa mwaka 2015, Diwani Omari amesema, Chama chake cha Chadema kipo vizuri na hasa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), na kusema hana Mashaka Ushindi Mkubwa upo.

Alisema sababu za kusema hivyo ni kwamba, Umoja huo unakubalika, na kwamba jinsi CCM kinavyojichanganya kikitumia Jeshi la Polisi kuwatia Hofu wananchi, ndivyo ambavyo wananchi wanaelimika kiasi cha Kujua Kudai haki zao.

Adha aliwaasa Viongozi wa Dini zote wasiache Kugombea Uongozi wa Kisiasa, kwa sababu Uadilifu wa Viongozi wa wengi nje ya Dini umeporomoka, na Unanuka, hivyo Ukombozi wa pekee umebaki kwa Viongozi wa Dini, ndio watakaowapa wananchi Matumaini.

Aliwatia Moyo wasiogope kupigania haki za wananchi kutokana na Vitisho vya Nguvu ya Dola vinavyotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), bali wajue kuwa wana Wanajibu Mkubwa kuisaidia Jamii, kwa sababu Mwisho wa yote Nguvu ya Umma itashinda.

No comments:

Post a Comment