Na Bryceson Mathias, Bukene
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Wilaya ya Nzega, Shekhe Omari Omari, amekituhumu Chama cha Mapinduzi (CCM) na Viongozi wake Kisiasa wilayani Bukene, akidai wamebaini njama za kuwabambikizia Kesi wanachama wa Chadema ili kuwatisha.
Akizungumza na Tanzania Daima Shekhe Omari ambaye pia ni Shekhe wa Wilaya ya Bukene na Diwani wa Kata Bukene (Chadema) alisema, kutokana na CCM kuanza kuweweseka na Ushindi wa Chadema kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wameanza Mchezo Mchafu wakizua Kesi.
Amesema, Usiku wa kuamkia jana, Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Mwamala Dickson Mosha (CHADEMA) , amekamatwa na Polisi Mtendaji wa Kijiji, huku mtendaji wa Kijiji hicho, Madua Said, akiwaongoza, na kutupwa ndani bila kutaja kosa lake ni nini?,
Omari alisema, Mtendaji wa Kijiji (Said) kama Mlinzi wa Amani, anayefahamu kuwa Mosha ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Kijiji, asingekubali Polisi wamchukue Mjumbe huyo kwenda kutupwa ndani Polisi, bila yeye kufahamu amekosa nini!
“Katika Kikao cha Ndani cha Serikali ya Kijiji, Mtendaji Said, aliwahi kumtamkia kuwa atamfanyia Kitu mbaya ambayo hawezi kuisahau, Hivyo kwa tukio hilo, Chadema tunaamini Kauli na Mkakati ule vinatekelezwa, kutokana na Wajumbe wetu kukibana CCM”.alisema Omari.
Mtendaji wa Kijiji Said, alipoulizwa kuhusika na Tuhuma hizo aliruka Kimanga na kukiri kwamba, alifuatwa na Polisi usiku, wakimuulizia Mtuhumiwa,na kuwaonesha alipo, wakamkamata na kuondoka naye! ‘Lakini sijui kosa lake ni nini”.alisema Said. Jambo lililopingwa na Mwenyekiti wa Chadema, ni njama za kukihujumu Chadema.
Kutokana na Ushindi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), inadaiwa hujuma mbalimbali zimekuwa zikifanywa na CCM ili kuwatia Hofu, ikiwa ni pamoja na kuwabambikizia Kesi wapinzani wao, ili kuwakomoa UKAWA.
Hii si jambo geni kwa serikali ya ccm kuwabambikia watu kesi. Hata mimi ninakesi heti nikiwa kwenyemaandamano nilijaribu kumnyang'anya polisi bunduki.
ReplyDelete