Tuesday, February 10, 2015

Mchungaji aota Ubunge wa Chadema Mvomero.

Na Bryceson Mathias, Nyandira Mvomero.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Pentekoste la Dar es salaam na Mkazi wa Turiani, Damiani Mlay, anaota kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), linaloshikiliwa na Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala.

Ukiachilia Mbali Waziri Makala, Wenye Ndoto hizo hadi sasa wapo wane, akiwemo Mkongwe ambaye ameendelea kupambana katika Masahibu ya kukitengeneza Chama hicho kwa kila Misukosuko ya hila za Chama cha Mapinduzi (CCM), Matokeo Worden.

Baada ya Chadema, kukiswaga CCM kwenye Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Mvomero, ambapo kiliwaburuza vibaya na kuwaangusha Vigogo wa Wilaya hiyo na kunyakua Vijiji vyao, akiwemo Waziri Makala, Mwenyekiti wa CCM na wa Halashauri.

Wanachama wa Chadema wilayni humo na hasa walio kwenye
Ngoma ya Chadema katika Mji Mdogo wa Madizini, ambapo walifanikiwa kuiangusha na kuchukua Serikali ya Mji huo, wamesema, Chadema kisifanye Maksa katika kura ya Maoni umpata Mgombea.

Wanachama na Viongozi walioko madarakani ndani ya Chadema Wilaya na Kata za Mvomero, wamesema wanakusudia kujiimarisha ili kuifuta (Delete) CCM, katika Kanda ya Kati na sehemu ya Pwani, ambapo Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Tanga, inajigamba kama Ngome ya CCM.

Wamedai, muda wa Chadema kuwa kamaTela la kuvutwa katika Mikoa hiyo, umepitwa na wakati, na kwamba sasa wako makini kuona Viongozi Mamluki kutoka CCM wanaotegemea kujipenyeza wakati huu kwa uroho wa madaraka, hawafanikiwi.

Chadema wilaya ya Mvomero, wakati huu, imefanikiwa kwa Kiwango kikubwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (TAMISEMI), uliofanyika mapema mwishoni mwa kwaka Jana, na hivyo viongozi na timu nzima ya ushindi huo, inajipanga vizuri kwa 2015.

No comments:

Post a Comment