Saturday, February 21, 2015

Chadema Kumung’oa aliyekuwa Naibu Meya, Mbiaji?

Na Bryceson Mathias, Kihonda
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Uchanguzi wa 2015, kimetangaza operesheni maalumu ya kumng’oa Udiwani, Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, ambayo kwa sasa inaongozwa na aliyekuwa Naibu Meya Morogoro, Lydia Mbiaji..

Akizungumza na Tanzania Daima, Mwenyekiti wa Chadema wa Kata hiyo, Elizeus Rwegasira, amesema, Chadema Maghorofani kinaandaa Operesheni inayoitwa jina la “Operesheni Lyidia Mbiaji Out” kwa kifupi LMO, kwa ajili ya Uchaguzi 2015.

“Tayari Chadema kimeandaa ya kuwa na mikutano ya hadhara katika Kata hiyo, ambayo itaendelea hadi wakati wa uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa mwaka huu.

"Tutatumia kila kila fursa na nafasi itakayopatikana, ambapo kila Wabunge na Viongozi wa Chadema watapokwenda na kurudi bungeni au kwenda katika Mikoa na Kanda mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha Chama, wahutubie Kihonda Mghorofani”.alisema Rwegasira.

Rwegasira aliwataka Wananchi, Wanachama na Wapenzi wa Chadema wanaopenda Mageuzi na kuondokana na Maisha Magumu kwa kila Mtanzani yanaendelezwa kupandwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha wanajiandisha kwenye Daftari la wapiga kura ili kuing’oa CCM.

Akijibu Mashabulizi hayo, Mbiaji alisema, “Mimi uchaguzi wa 2015 nimemaliza, ila nasubiri mawakala wahesabu kura, nitangazwe na kuapishwa, maana hao wanaotaka kupambana na mimi nilishawachapa tena nikiwa mgeni, wanaume walikuwa 10 na wanawake wawili, iwe leo!.

“Niliwaahidi wananchi wa Kata yangu mambo mawili, lakini kwa mshangao nimewafanyia mambo manane, hivyo operesheni ya LMO (Lydia Mbiaji Out) ni cha Mtoto, wasubiri mambo ya watu wazima”.alisema Mbiaji.

Katika uchaguzi uliopita, Mbiaji aliyepambana vikali katika kura za Maoni za Chama chake CCM, na uchaguzi Mkuu wa 2010, amesedai aliwagaragaza wanaume 10 na Wanawake wawili katika kinyang’anyiro hicho, wakiwemo Wapinzani, na kuibuka Mshindi; Hivyo haogopi!.

No comments:

Post a Comment