Saturday, February 21, 2015

CHADEMA kufuta nafasi za Ukuu wa Wilaya

Naibu katibu Mkuu CHADEMA (Zanzibar) Mh. Salum Mwalimu akihojiwa na Star TV amesema CHADEMA itafuta nafasi za Ukuu wa Wilaya kwani hazina majukumu ya kiutendaji na nigharama kwa wananchi zisizo na lazima.

Akiendelea kuongea na Star TV amekanusha kuwa kuna mgogoro ndani ya UKAWA juu ya mgombea wa Urais; na UKAWA haija vunja vyama, vyama vipo pale pale, bali kila chama kina wajibu wa kuendelea kujijenga na kuimarika kama chama ili kila mmoja aweze kuwa mshirika imara na mwenye nguvu kwenye UKAWA.

Pia Mh. Mwalimu ameelezea kuhusu ziara ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, kanda ya Nyanda za Juu Kusini kuwa inalenga kuwahimiza waTanzania kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura; na kuimarisha uongozi wa CHADEMA katika ngazi ya Kanda. CHADEMA inalenga kuzipa kanda mamlaka na nguvu zaidi kwenye kuamua mambo ndani ya kanda zenyewe.

Mwisho ametoa rambirambi kwa katibu Mkuu wa CCM, Abrahaman Kinana, kwa msiba mkubwa wa Mh. Salmin Awadhi na wananchi wote wa jimbo la Magomeni kwa kuondokewa na Mwakilishi wao.

Imeandikwa na Bagasa

1 comment: