Sunday, January 18, 2015

TAMKO JUU YA MAANDAMANO YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DODOMA

TAMKO JUU YA MAANDAMANO YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DODOMA

Kufuatia hali ya kusikitisha iliyowakumba wanafunzi wa CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) tarehe 14/01/2016, Sisi Wanafunzi wa CHADEMA Tawi la Chuo kikuu MWENGE tunatoa POLE kwa Wanafunzi wote waliokumbwa na kadhia hiyo. Aidha TUNALAANI matumizi ya nguvu yasiyo ya kawaida kutoka kwa Jeshi letu la polisi na hata kupelekea majeruhi kwa wanafunzi wenzetu. Hali hii imekuwa ikijitokeza mara kwa mara pindi Wanafunzi na Raia wa Nchi yetu wanapojitokeza barabarani kudai haki zao. Napenda ifahamike wazi kuwa maandamano yalikuwa ni ya Amani na hakuna mwanafunzi yeyote aliyejihami kwa silaha ama zana yeyote kiasi cha kuashiria uvunjifu wa AMANI kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu ikiwemo Utawala wa Chuo (UDOM).

PILI tumesikitishwa na kitendo cha kumfukuza chuo Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Ndg. MWAKIBINGA na kumsimamisha masomo Rais wa serikali ya Wanafunzi Ndg. MASATU.

Nguvu na jitihada za makusudi na upesi zilizotumiwa na Utawala wa Chuo kuwachukulia hatua Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi, laity kama zingeelekezwa katika kuikumbusha Serikali wajibu wake kwa wanafunzi wa Masomo ya Ualimu wa Sayansi ni dhahiri kuwa tayari stahiki zao zingekwisha kupatikana.

DHULUMA AMBAYO WATAWALA WAMEENDELEA KUIONYESHA KWA MASKINI WA KITANZANIA NI ISHARA TOSHA KUWA UKINGO UMEKARIBIA. NACHELEA KUSEMA MWAKA HUU WATANZANIA HATUNA BUDI KUUTAZAMA KAMA MWAKA WA KIHISTORIA PALE IFIKAPO OCTOBER, 31 2015 TUKIANZA NA APRIL, 30 2015 KWA KUIKATAA KATIBA INAYOPENDEKEZWA.

MWISHO tunaitaka Serikali kwa kipindi hiki kifupi walichobakiwa nacho kuacha KUCHEZA NA MAISHA YA WATANZANIA kwa vitu ambavyo haijajipanga. Laiti kama wangekuwa na mipango mizuri haya yote yasingejitokeza. “ELIMU NI JAMBO NYETI SANA”


IBRAHIM A. CHOTOLA

M/KITI CHADEMA TAWI LA CHUO KIKUU MWENGE

No comments:

Post a Comment