Saturday, January 10, 2015

Mwenyekiti wa Chadema, atema Cheche kwa RC Njombe.

na Bryceson Mathias, aliyekuwa Njombe.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Njombe, Ally Mhagama (Dkt. Sagasaga), ametema cheche akisema, “Sitahudhuria Vikao vya Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi, iwapo ataendelea kujinadi, kama Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Vikao vya Maendeleo ya ‘Njombe tunayoitaka’.

Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kususia Kikao cha Nchimbi na Wafanya Biashara, alichoitisha, ili kujadili ‘Njombe tunayoitaka’ katika Ukumbi wa Kyando karibuni, Mhagama alisema, hatahudhuria Vikao vyake, kama atajinadi ni Kada wa CCM wakati ni Rais wa Mkoa.

“Iwapo Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi na Viongozi wengine serikalini, watajisahau na kuvaa Kofia ya Serikali na kuitisha Vikao, wakida ni vya Maendeleo ya Kijamii, kumbe ndani mwake, ni vya Kikada ili kuipigia Debe CCM, Katu Sitahudhuria”.alisema Dkt. Mhagama.

Mgomo wa Dkt. Mhagama, ulitokana na Mchango wake kuhusu Hoja ya Dkt. Nchimbi, kupigia Debe kuwa, kuna ajira 6,000 za Wachina zitakazotokana na Uchimbaji wa Madini mkoani humo, hivyo wakazi na hasa wafanya biashara Njombe, Walime Matunda kwa Wingi ili kuwauzia.

Mhagama alipinga Hoja hiyo akisema, alitarajia Serikali ya Mkoa itoe Dira kwa Serikali Kuu, iainishe ni Ajira Kiasi gani, 200 au 300, zitakazotengwa kwa wakazi hao, badala ya wao kuzunguka kwenye hiyo Migodi wakiuza Mapera na Machungwa kama watumwa, huku Wageni wakifaidi.

Licha ya Nchimbi kumpongeza, ila amechangia kwa Maneno Makali, alijikwaa kwa kuchomekea kauli kuwa, yeye (Nchimbi) ni mmoja wa Makada wa CCM, na hapo Mhagama, alisusia Kikao hicho na kusema si cha Maendeleo ya Njombe, bali ni cha kui-Imarisha CCM au kuidumaza Chadema.

Hata hivyo, baadhi ya Wafanya biashara waliohojiwa walisema, hawakuona Mashiko ya Kikao hicho, na wakampongeza Mwenyekiti huyo wa Chadema (Mhagama), kwa Mchango wa kuwatetea kuwa, wafanyabiashara wamekuwa wakigandamizwa wakirundikiwa Kodi nyingi, hivyo kikao hicho kilitakiwa kijadili unafuu, si kuwalaghai.

No comments:

Post a Comment