Sunday, January 4, 2015

HONGERENI MASHUJAA WETU

Pamoja na kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Jordan Rugimbana lakini tunawatia moyo Mashujaa wetu watatu Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael mliofunga safarai Kutoka Geita mpaka Dar es Salaam ili kumfikishia Ujumbe Rais Jakaya Kikwete kutokana na kukerwa kwenu na Kukithiri Vitendo vya Rushwa, Matumizi mabaya ya Rasilimali za Taifa na Unyanyasaji wa Raia wasio na Hatia.
Kila Raia anayo Haki ya kuonyesha hisia zake au kufukisha ujumbe kwa watawala ili mradi asivunje sheria za nchi, lakini jambo la kushangaza vijana hawa wameonekana kama wanataka kuhatarisha usalama wa nchi kitu ambacho si sahihi. Kulikuwa na kila sababu kuwapa fursa ya kusikilizwa kama Raia wema. Muasisi wa Taifa Hili Baba wa Taifa aliwahi kuanzisha Matembezi kama hayo Mwaka 1967 ili kuunga mkono Azimio la Arusha ambapo washiriki walitembea kutoka Arusha hadi Dar es Salaam. Lakini hilo halikuwa jambo la kuhatarisha amani kwa sababu liliasisiwa na Chama Tawala. Jambo lolote linalofanywa na Wapinzani la kufikisha ujumbe kwa watala linaitwa ni la kuhatarisha Amani kitu ambacho si kweli. Kwa kweli tuna sababu ya kubadilika Watanzania ili tuweze kupiga Hatua.
Namaliazia kwa kusema HONGERENI MASHUJAA WETU KWA KUFIKISHA UJUMBE KWA WATAWALA.

No comments:

Post a Comment