Tuesday, December 23, 2014

CHADEMA Yamliza Waziri wa Kikwete kijijini kwake.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Desemba 14, kimewaliza Viongozi wa Chama cha CCM Mvomero akiwemo Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala, ambapo kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wameangukia Pua, kwa Vijiji vyao kuchukuliwa na Chadema.
Mbali ya Waziri Makala, wengine waliolizwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Jonas Van Zealand, Mwenyekiti wa Wilaya wa CCM, Abdalah Mtiga, Katibu Mwenezi wa CCM, Yusufu Kingu, Mwenyekiti wa Vijana (UVCCM), Pascal Boge.
Akizungumza na Tanzania Daima, Diwani wa Chadema Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, alisema, waliolizwa si Waziri Makala na Wenzake tu wilayani, bali Serikali yote ya Mji Mdogo wa Madizini, Viti vyote vimechukuliwa na Chadema, na Viongozi wa CCM wako mafichoni.
“Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtibwa, Aloyce Msigwa, Mwenyekiti UVCCM, Ponsian John, wamepigwa vijijini mwao, Khalifa Ahmed (Chadema), akinyakua Uenyekiti wa Kijiji cha Mji Mdogo wa Madizini, uliosababisha Viongozi wote wa CCM kujificha”.alisema Mwakambaya.
Licha ya Wananchi kushangilia Kuchaguliwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Lungo, Sifuni Mzava (CHADEMA), aliyekuwa TLP; Watu wa Mji Mdogo Madizini-Mtibwa na Turiani wa Vyama vya CCM, Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na Vyama vingine, walipohijiwa walisema,
“Kama Taifa linavyomuenzi Mwasisi, Mwalimu Julus Nyerere, bila Kujali Itikadi zetu, tumepiga Kura kumuenzi Diwani wetu, Marehemu Tusekile Mwakyoma (Chadema), aliyefariki kwa kuchomwa Kisu, kutokana na kukataa wananchi tusinyanyaswe na Mwekezaji wa Mtibwa”.
Awali ushindi wa Chadema, umeelezwa umetokana na Ushirikiano wa Watu, Viongozi wa Chadema akiwemo, aliyekuwa Mgombea wa Ubunge wa Mvomero, Matokeo Wordern, ambaye wanachadema wanadai ushindi wake ulichakachuliwa, ndio walikuwa chachu ya Ushindi huo.

1 comment: