Sunday, January 11, 2015

CHADEMA imeng'ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

Na Yericko Nyerere
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Thamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini Arusha ambapo sasa rasmi ccm inakuwa chama cha upinzani Arusha, CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii kipo.

Izingatiwe kuwa oparesheni M4C Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchaguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama akina Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kutopata kata nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo lakini tupeane shule ya falsa ya siasa kidemorasia kwa ufupi ambayo ndio hutawala siasa za uwanda wa chama kinachojiandaa kushika dola.

Niseme kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapoamua kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa aliyevunja katiba,itikadi,itifaki na falsafa ya chama hicho, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua hata mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo stahiki cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kupata kushindwa kupata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya miezi sita hadi mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ndivyo vitakuwa vipimo vyake, kwa sasa yanayotokea yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati la chama na kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya ambao utafiti unaonyesha ni kundi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 18-26 ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura 2010. Lakini hata hawa waliojiandikisha yaani wenye kupiga kura sasa, idadi kubwa ya wapiga kura hao hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuuza shahada zao.

Pili Tume ya Uchaguzi, hii ni lazima juhudi za msksudi zitumike kuitoa mikononi mwa chama tawala, ni hatari kuiacha iendelee kuwa wakala wa ccm badala yakuwa tume huru.

Tatu Vyombo vya dola, hapa ndipo panahitaji mkakati mkuu wa kisiasa, jeshi la polisi ni lazima tukabiliane nalo na ieleweke vema kuwa ccm haitakoma kulitumia jeshi la polisi ama vyombo vya dola kwa ujumla mpaka siku inakata roho kabisa, hivyo njia mbadala ni muhimu sana tunapoelekea kushika dola hili la Tanzania mnamo octobar 25, 2015.

Kwanza uundwe mkakati wa uhusiano mwema na vyombo vyote vya dola nchini, hili linaweza kuwa gumu kidogo na linaweza kuifanya serikali ianze kupata mafua ya msimu na kujikuta tunaingia kwenye mgogoro unaoweza kutumiwa na wakware wa akili wa ccm kama akina Mwigulu na kufikiria uhaini, jambo la muhimu ni kuziangalia sheria za nchi hasa zinazoratibu vyama vya siasa na mienendo yake,

Mathalani kiongozi wa kisiasa kuzuru makao makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania na kusikiliza changamoto zinazowakabilli, hili halina zuio kisheria, ilimradi haendi kugawa kadi za chama hapo,

Ni lazima tuitazame upya sheria inayosema mtumishi wa umma asijihusihe na siasa, hii ni nzuru lakini iboreshwe ili iwe na tafsiri ya maslahi kwa nchi na hatimae taifa kuzaa siasa za kisasa na za kimaendeleo.

Wanamikakati warejee chini wawafanyie utafiti wa kisayansi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba, Chama lazima sasa kijikite kwa nguvu zote kwenye msingi (chadema ni msingi).

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu na uchaguzi mkuu ujao tutashinda!

Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu bali imeng'ara, kimkakati ni ccm ndio imepoteza.


No comments:

Post a Comment