Sunday, November 16, 2014

MWANA-DIASPORA, LIBERATUS MWANG'OMBE ATOA USHAURI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WA SHULE YA SEKONDARI MONTFORT MBARALI MBEYA

Akiongea na watahiniwa wa kidato cha nne siku mbili kabla ya mtihani wa Taifa 2014 wa shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali, Mwana-diaspora kutoka Washington, D. C., Marekani, Liberatus Mwang'ombe "Libe" alianza kwa kusema, Montfort ni shule aliyo soma na anajisikia faraja akiyaona mazingira yale. Aliendelea kwa kusema, maamuzi ya mwisho ya kila binadamu yapo chini ya himaya yake. Alisema "huwezi kutegemea mtu baki au mwingine aongoze au arutubishe maisha yako, ni wewe binafsi unaweza kufanya tofauti kwenye maisha yako na kila binadamu ni kiongozi. Pia alisema anaamini kuwa kila binadamu ana ndoto zake kwenye maisha; alisema; "ni muhimu kujiwekea malengo ya ndoto zenu. Malengo ambayo yanatimilika, malengo ya kiuhalisia na malengo yenye muda maalumu." Aliendelea na kusema, "ndoto bila malengo itaendelea kuwa ndoto na kutimilizwa kwake kutaendelea kuwa ni ndoto tu." Mwisho Ndg. Libe aliwaomba wanafunzi hao wasimuangushe kwa kuweka malengo kwenye ndoto zao na kuhakikisha wanazitimiliza.
Mbali ya maongezi Ndg. Liberatus alichangia miundombinu ya elimu kwa wanafunzi hao
Moja ya wanafunzi akimshukuru Liberatus Mwang'ombe kwa msaada waliopokea.


Juu na chini Liberatus akiendelea kubadilishana mawazo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Monfort, Mbeya

No comments:

Post a Comment