Sunday, May 4, 2014

Ukawa wasisitiza serikali tatu

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amesema wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hawatorejea kwenye Bunge la katiba hadi wahakikishiwe kuwa kinachojadiliwa ni rasimu ya katiba inayotokana na mawazo ya wananchi.
AIdha amesema roho ya katiba hiyo ni sura ya sita inayoelezea kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu.
Alisema hawatokuwa sehemu ya kujadili na kupitisha rasimu inayokiuka misingi ya mawazo ya wananchi na kufuata matakwa ya CCM.
Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF, kinachofanyika jijini Dar es Salaam.
Alifahamisha kuwa mpango wa kulivuruga bunge hilo maalum la katiba ulianza zamani baada kupindishwa kanuni ili Rais Jakaya Kikwete alizindue bunge hilo mwisho.
Aidha vurugu zilitanguliwa na njama za kutaka kumpa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba muda mfupi wa kuwasilisha rasimu ya katiba.
Alielezea kusikitishwa na kitendo cha kubezwa kwa rasimu ya katiba iliyowahusisha watu wazito ambao wengi wao ni kutoka CCM na kuhoji hali ingekuwaje kama angekuwa Mwenyekiti wa tume hiyo.

No comments:

Post a Comment