Friday, May 23, 2014

TAFAKARI MAUZAUZA YA MUUNGANO WETU

Suala la muungano limejaa mauzauza mengi kiasi kwamba watawala wanashindwa kujibu maswali na hoja za msingi juu ya muungano huu.

Wanacho kifanya ni kuwatishia wananchi kuwa jeshi litachukua nchi au Sultan atarudi Zanzibar. Huu ni uongo na upotoshaji mkubwa.

Hili swa la muungano wa nchi zetu mbili lina leta maswali mengi kuliko majawabu.

Nitafanya uchambuzi kidogo wa muungano wetu huu batili. Kwa kifupi nchi inayoitwa Tanzania ni batili.

Ubatili wake unakuja pale ambapo ilianzishwa na mtu moja, Nyerere, bila kushirikisha upande wa pili ( Zanzibar na Bunge laki): hata waTanganyika hawakushirikishwa.

Ili Muungano uwe halali kisheria, ni budi hati ya muungano iwe ratified na Bunge la Zanzibar. Ukweli ni kuwa Bunge la Zanzibar halijawahi kupitisha hiyo hati.

Hadi leo hiyo hati haipo kwenye hansard ya Bunge la Zanzibar, Nyerere alitumia ubabe kuwalazimisha Zanzibar muungano; kwa kweli sijui malengo yake yalikuwa ni nini.?

Ubabe huu unadhihirika pale alipo lazimika kuiuwa Tanganyika na kutunga "decree" tatu baada ya yeye kukutana na Karume. Tunajua decree hutungwa na nchi iliyo chukuliwa na jeshi.

Nyerere kwa ubabe wake alibadirisha mambo ya Tanganyika kuwa ya muungano, mfano, nembo ya Tanganyika ikageuzwa ya muungano, office za Tanganyika zika geuzwa za muungano, Katiba ya Tanganyika ikawa ya muungano, mahakama kuu kuwa ya muungano nk.

Haya yote alifanya yeye binafsi kwa amri (decree) bila kuwashirikisha waZanzibar (Bunge la Zanzibar) wala waTanganyika. Huu ni udicteta.

Kwa history hii kama kuna mtu atakuwa anashangaa kwa nini waZanzibar wana chuki na Nyerere na Tanganyika; atakuwa close minded na hataki kuukabili ukweli.

Zanzibar ni nchi ambayo ilikuwa huru kabla ya muungano na sasa imesema haitaki huu muungano wa mauzauza. Utailazimisha muundelee kuungana nayo? Tuwe wakweli, wapenda haki na wahalisia.

The only way tutaweza kuishi kwa amani na Ndg zetu waZanzibar ni kuipa Zanzibar mamlaka kamili au kudisolve huu muungano batili. Serikali mbili au moja WONT WORK.

Tatu ndio jawabuOtherwise; muungano huu batili ni time bomb ambalo lina subiri kulipuka muda wowote
Kumbukeni; Zanzibar ni nchi kamili kama Kenya na Uganda; ilipata Uhuru wake kwa kumwaga damu, sio kama sisi tulipata kwa bwerere na ndio maana akili zetu hazitaki kukabili ukweli.

Zanzibar ina Rais wake na Kikwete leo hii akienda Zanzibar hana sauti; huenda kam mualikwa (mgeni). Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano Mizengwe Pinda huwa hakanyagi Zanzibar ( kuna mtu amewahi sikia Pinda kaenda Zanzibar kusimamia miradi ya maendeleo?). Hii inazihirisha pasi na shaka kuwa Pinda sio Waziri wa muungano, bali wa Tanganyika.

Tanganyika ipo ila watawala dharimu wa CCM wanaiogopa.
Leo hii Kikwete akienda Zanzibar hapigiwi mizinga 21; Dr. Shein ndio anapigiwa. Sasa hapo Mkuu wa nchi ni nani? Shein au Kikwete?

Lazima kama vijana wa kizazi kipya, tujifunze kudadisi na kusaka ukweli; sio kubuluzwa na haya MA CCM ambayo yameishiwa mbinu za kutawala na kubaki kutumia mabavu.

TAFAKARI.

No comments:

Post a Comment